Rais Jakaya Kikwete akiwa na wafanyakazi wa CCBRT na Vodacom. |
Hayo yameabainika baada ya rais jakaya mrisho kikwete kutembelea ujenzi unaoendelea katika hospitali ya CCBRT, ujenzi uliofadhiliwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom.
Taarifa zaidi na Abdallah salehe
Rais kikwete alipata fursa ya kutembelea wagonjwa katika hospitali hiyo ambayo imekuwa ikitoa msaada kwa wagonjwa wenye maradhi ambapo juhudi ya waganga na wauguzi inaonekana waziwazi kutokana na mchango wao wanaouto ikiwepo roho ya huruma kwa wagonjwa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya CCBRT wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa hatari wa fistula pamoja na magonjwa mengine sugu.
Moja kati ya maradhi yanayoonekana kumfedhehesha mwanamke ni pamoja na ugonjwa wa fistula, ugonjwa ambao hakika unaoneka kumyima raha mwanamke na kufikia hatua ya kutengwa na jamii.
Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali mtoto mmoja katika hospitali hiyo ya CCBRT |
Rais kikwete pia alipata fursa ya kutembelea majengo mapya yanayojengwa kwa kushirikiana na kampuni ya vodacom, ujenzi ambao utaweza kusaidia kupokea idadi kubwa ya wagonjwa.
Bi. Janeti Mbene |
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Bw. Renemeza, akapata fursa pia ya kuelezea jinsi ujenzi huo umpya.
0 comments:
Post a Comment