Na Hilali Ruhundwa
TUME ya mchakato wa mabadiliko ya katiba mpya nchini
imeshauriwa kutumia ripoti ya katiba na sharia ya chama cha sharia cha
wanawake nchini ili kuzingatia masuala ya jinsia na haki zake.
Chama
cha sheria cha wanawake Tanzania, kimeitaka tume ya mabadiliko ya katiba
nchini, kuhakikisha kuwa inawashirikisha wananchi wote hasa wa
vijijini, ili kutoa maoni ya ulingano wa kijinsia katika katiba hiyo.
Hayo
yamebainishwa na mratibu wa jinsia wa chama cha sheria cha wanawake
nchini Debora Mushi, wakati wa uzinduzi wa ripoti ya katiba na sheria ya
chama hicho, na kusema kuwa miongoni mwa mambo yaliyomo katika ripoti
hiyo, yanaweza kutumiwa na tume ya mabadiliko ya katiba mpya, ili kutoa
katiba yenye ulingano wa kijinsia.
Ameongeza kuwa haki zote za
makundi hayo, ni muhimu ziingizwe ktk katiba mpya, ikiwemo haki za
wanawake na makundi mbalimbali, sanjari na kuweka ukrasa maalum,
unaoonesha utekelezaj wake.
Jamhuri ya muungano wa Tanzania, ipo
katika ukusanyaji wa maoni ya wananchi, kuhusu mchakato wa uundwaji wa
katiba mpya, ambapo hivi karibuni, waziri mkuu wa Tanzania Mizengo
Kayanza Peter Pinda, amesema kuwa zoezi hilo linaendelea vizuri, na
kwamba kufikia mwaka 2014, itapatikana katiba mpya iliyotokana na
wananchi.
Friday, November 9, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ZILIZOSOMWA ZAIDI
-
NYOTA wa muziki nchini Tanzania Ray C pamoja na TID wameingia katika mtafaruku mkubwa kupitia mtandao wa Instagram baada ya kupishana ka...
-
Bondia Pacquiao amerejia nyumbani Ufilipino baada ya kufanyiwa upasuaji wa bega huko Marekani ambapo pamoja na kushindwa Floyd ...
-
MWANADADA kutoka Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amefunguka kuwa anaumia kuona listi ndefu ya Wabongo wanaosubiri kunyongwa nchi ...
-
RECHO: Hapa ndipo yalipoanza kuandaliwa na kuzikwa kwenye makazi yake mapya mbinguni. Shimo dogo ni kaburi ya mtoto wake aliyefariki muda...
0 comments:
Post a Comment