Monday, November 3, 2014

BOMU LAUA WATU 55 PAKISTAN

Watu 55 wameuawa katika shambulizi la bomu la kujitoa mhanga nchini Pakistan karibu na mpaka na India, ikiwa ni shambulizi baya zaidi la kigaidi kuwahi kutokea nchini humo katika miaka ya karibuni. 
MLIPUKO huo ulitikisa umati wa watazamaji waliokuwa wakiondoka baada ya sherehe za kila siku za kufunga mipaka.
Makundi kadhaa, likiwemo la Taliban, yamedai kuhusika na shambulizi hilo ambalo liliwajeruhi zaidi ya watu 120, lililotokea karibu na kivuko pekee cha mpaka kati ya Pakistan na India cha Wagah mashariki ya mji wa mashariki mwa Pakistan, Lahore.
Shambulizi hilo lilitokea baada ya kukamilika sherehe maalumu za kijeshi za "kushusha bendera" ambazo huwavutia maelfu ya watazamaji kila siku na ni maarufu sana kwa watalii.
Hili Ni shambulizi kubwa kuwahi kuuwa watu wengi zaidi Pakistani tangu bomu la kujitoa Muhanga lililotokea kanisani Kaskazini Magharibi mwa mji wa Peshawar na kuuwa watu 80 mwezi september mwaka uliopita.

Pakistan inakumbwa na uasi wa ndani unaofanywa na kundi la Taliban ambao umesababisha mauaji ya maelfu ya watu katika miaka ya karibuni.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI