Friday, April 18, 2014

RONALDO KUIVAA BAYERN-MUNICH

Ronaldo
MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ana matumaini ya kurejea Jumanne dhidi ya Bayern Munich katika mechi yao ya kwanza ya nusu fainali. 
"Nina furaha sana. Nilitaka kucheza na kuisaidia timu (dhidi ya Barcelona) lakini wachezaji wenzangu walifanya kazi nzuri. Nazidi kuwa fiti sasa, sisikii maumivu yoyote. Huenda nikarejea dhidi ya Bayern au katika mechi ya marudiano nao."
Mwanasoka Bora huyo wa FIFA, alikosa michezo kadhaa ikiwamo wa Fainali ya Kombe la Mfalme wakati Real Madrid ikiizamisha Barcelona kwa kuifunga mabao 2-1, huku yeye akiwa jukwaani kabla ya kujumuika pamoja klushangilia taji hilo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI