Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta amesema anapokea meseji za simu zaidi ya 50 kwa siku za kumtukana na kusisitiza ataendelea kupambana kuhakikisha Katiba inayopendekezwa inapatikana.
SITTA alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma jana wakati akielezea
kutoridhishwa kwake na kile alichodai ni namna hukumu ya kesi
iliyofunguliwa na Saed Kubenea inavyopotoshwa na wanaomchukia.“Kuna
baadhi ya vyombo vya habari wananichukia mimi binafsi. Wasichanganye
chuki hizo na mchakato wa Bunge Maalumu,” alisema Sitta na kuongeza;
“Mimi napokea matusi kila
siku. Meseji zisizopungua 50 viongozi wa Chadema wameweka namba zangu
katika tovuti nitukanwe kila siku hilo mimi niko tayari na mnaniona niko
safi tu wala sihangaiki nalo.”
“Lakini sasa Bunge Maalumu ni chombo cha kikatiba, kiko tofauti na
mwenyekiti wake. Huwezi kuliadhibu Bunge Maalumu kwa sababu hupendi sura
ya mwenyekiti wake,” alisema.
Sitta alienda mbali zaidi na kusema, “Kwa hiyo wale wanaoendeleza
hayo mapambano tuendelee na tutaendelea kupambana, lakini kazi ya Bunge
Maalumu itaendelea na ndugu zangu Watanzania mjue tunaandaa Katiba safi
na rafiki kwa wananchi na itapatikana.”
Sitta alisema baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo ya kesi ya Kubenea
dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kumekuwa na tafsiri
alizosema ni potofu.
Baada ya maelezo hayo alimpa ruksa AG, Jaji Frederick Werema kutoa ufafanuzi.
Jaji Werema alisema
Mahakama Kuu, katika kutafsiri kifungu cha 25(1) (2) inakiri kwamba
kuna tofauti kati ya kifungu kilichoandikwa Kiswahili na kile
kilichoandikwa Kiingereza.
Alisema Mahakama Kuu katika hukumu hiyo imesema mamlaka ya kuandika
Katiba Mpya ina maana ni mamlaka ya kuandika na kupitisha katiba
inayopendekezwa kwa ajili ya kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya
kupigiwa kura ya maoni.
Takukuru yalitesa Bunge
Wakati hayo yakiendelea suala la kuingizwa ama kutoingizwa kwenye
katiba, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), linaonekana
kulitesa Bunge la Katiba baada ya kamati 10 kati ya 12 kulirejesha tena
jana.
Rasimu iliyowasilishwa bungeni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ililiacha suala hilo kwa maelezo kuwa siyo moja ya mambo ya Muungano na msimamo huo ukaungwa mkono na Kamati ya Uandishi ya Bunge hilo.
0 comments:
Post a Comment