Thursday, January 8, 2015

WANNE WAFA AJALI YA BASI IRINGA!! *PICHA*

ZAIDI ya watu 4 wamefariki na wengine kujeruhiwa baada ya basi la abiria kutoka Mbeya kwenda Dodoma kugongana na Lori katika kijiji cha Ibetelo eneo la Nyororo wilayani Mufindi mkoani Iringa. 
Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa Ramadhani Mungi amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 4.45 asubuhi na kuhusisha basi mali ya kampuni ya Fanuel Express yenye namba za usajili T919 kugongana uso kwa uso na lori lenye namba za usajili T122 ALW mali ya kampuni ya Transisco lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda nchi jirani. 
Amesema watu wawili waliokuwa ndani ya basi wamefariki papo hapo na wote waliokuwa ndani ya lori wanahofiwa kufa, ambapo hadi kufikia majira ya saa 7 mchana, watu wawili ndani ya lori walikuwa wamethibitika kufariki kufanya waliokufa kuwa wanne hadi kufikia saa 7 mchana,
Zoezi la kuondoa miili iliyokuwa ndani ya lori linaendelea ambapo amesema kuwa huenda idadi hiyo ya waliokufa ikaongezeka. 
Akielezea mazingira ya ajali hiyo, Kamanda Mungi amesema kuwa basi hilo lilikuwa likijaribu kulipita basi lililokuwa mbele yake katika eneo ambapo palikuwa na lori lingine lililoharibika, wakati huo huo lori lililohusika katika ajali hiyo lilikuwa likikwepa lori lililoharibika pamoja na basi hilo, ndipo magari hayo yalipogongana uso kwa uso katika jitihada za kukwepana.
Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Mafinga.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI