MMILIKI wa kampuni ya Microsoft Corporation, Bill Gates ameendelea kuuthibitishia ulimwengu kwamba haogopi kuwekeza pesa yake kwenye biashara yoyote Duniani.
Ni mmoja ya watu wanaofadhili miradi mikubwa ya kilimo Afrika, leo kuna hii story ambayo kama ingekuwa Bongo mtu anawekeza upande huu ni wachache ambao wangemuunga mkono.
Picha na video zimeenea mitandaoni, Gates kaamua kugeukia huu mradi wa maji safi ya kunywa ambayo yametengenezwa kutokana na kinyesi cha binadamu.
Mikakati ya Gates ni kushirikiana na Kampuni hiyo kusambaza mitambo hiyo katika nchi mbalimbali maskini ikiwemo Senegal muda mfupi baada ya majaribio yake kukamilika.
Teknolojia hiyo imeungwa mkono na shirika la WaterAid ambalo limesema kuwa litasaidia sana katika maeneo ya mengi yenye ukame ambapo kulingana na shirika hilo watu millioni 748 hawana maji safi ya kunywa.
0 comments:
Post a Comment