NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Friday, May 30, 2014

SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS LAANZA RASMI LEO JIJINI DAR ES SALAAM, WASHINDI WATANO KUTAFUTWA

Msimamizi wa Mashindano ya Tanzania Movie Talents, Bw Tony Akwesa akitoa maelekezo kwa washiriki waliojitokeza kwaajili ya shindano la Tanzania Movie Talents kwa kanda ya Pwani unaoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar Es Salaam
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mstari tayari kwa kuchukua fomu za ushiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents lililoanza rasmi leo Kwa Kanda ya Pwani.
Washiriki waliojitokeza kuchukua fomu za Shindano la Tanzania Movie Talents wakisoma fomu kwa umakini kabla ya Kujaza
Washiriki wakipewa maelekezo na Mmoja wa wafanyakazi wa Proin Promotions
Washiriki wakisoma fomu kwa makini
Wakielekezwa Kujaza Fomu za ushiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents.
Shindano la Tanzania Movie Talents limeanza rasmi leo Katika Kanda ya Pwani Ambapo usaili unaendelea kufanyika leo na kesho katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo Jijini Dar Es Salaam ambapo takriba washiriki zaidi ya 250 wameweza kuchukua fomu za ushiriki wa Shindano hilo
Shindano hili ni muendelezo wa shindano la kusana vipaji vya kuigiza ambalo limefanyika tayari kwa Kanda Tano za Tanzania yaani Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kusini na Kanda ya Kaskazini na sasa tunamalizia Kanda ya Pwani ambapo washindi watano watapatikana kwa Kanda ya Pwani na kila mmoja atajinyakulia kitita cha Shilingi Laki Tano taslimu.
Shindano hili limelenga kuibua vipaji vilivyojificha ambavyo havikuwahi kupata nafasi ya kuonekana. 
Baada ya Wasindi watano kupatikana kwa Kanda ya Pwani, washindi takribani 20 kutoka kanda zote sita za Tanzania watawekwa katika kambi moja Jijini Dar Es Salaam na watapewa mafunzo kutoka Kwa Walimu Wa Sanaa kutoka Chuo Cha Sanaa cha Bagamoyo na baadae kushindanishwa na hatimaye mshindi mmoja kupatikana na Kuibuka na zawadi nono ya Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Vilevile Washiriki kumi watakaopatikana katika fainali hiyo watakuwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions na watatengeneza filamu ya pamoja na hatimaye Kuweza kunufaika na Mauzo ya Filamu hiyo

NORWAY NA ZANZIBAR ZATILIANA SAINI UNENGWAJI WA WODI MPYA YA WATOTO

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jidawi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo Kikuu cha Helse Bergen kiliopo Haukelang Norway Dkt. Stener Kvinnsland wakitia saini makubaliano ya ujenzi wa Wodi mpya ya watoto eneo la Mnazi mmoja wakishuhudiwa na Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Ingunn Klepsvik alieva miwani. (Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).
Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Ingunn Klepsvik akizungumza na viongozi wa Wizara ya Afya waliongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jidawi mara baada ya utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa Wodi ya watoto eneo la Mnazi mmoja, utakaoghari bilioni moja na milioni miasita za kitanzania mpaka kumalizika kwake.
Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bi. Ingunn Klepsvik wakiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jidawi mara baada ya utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa Wodi mpya ya watoto Hospitali ya Mnazi mmoja.
(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

KINANA AITIKISA BABATI

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wakati akihitimisha ziara yake katika wilaya ya Babati yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali na kusikiliza kero za wananchi ili kuzipatia ufumbuzi, Mkutano huo umefanyika kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati ukihudhuriwa na maelfu ya Wananchi. PICHA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-BABATI
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wakati akihitimisha ziara yake katika wilaya ya Babati yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali na kusikiliza kero za wananchi ili kuzipatia ufumbuzi, Mkutano huo umefanyika kwenye uwanja wa Kwaraa mjini babati
 .
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiwahutubia wananchi kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati
Maelfu ya Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo
Polisi wakiwa wameimarisha ulinzi

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA CHI ZA NJE WA UTURUKI

Makamu wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Uturuki, Ahmet Dovutoglu, aliyeongozana na ujumbe wake wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo leo, Mei 30, 2014. Katika mazungumzo yao walisisitiza juu ya ushirikiano katika Nyanja mbalimbali baina nchi hizi mbili . Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya Kiserikali iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Uturuki, Ahmet Dovutoglu, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Mei 30, 2014. Picha na OMR

KATIBU MKUU KIONGOZI AKUTANA NA NCHI WASHIRIKA WA MAENDELEO JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akibadilishana mawazo na mabalozi na wawakilishi wa nchi washirika wa maendeleo kabla ya mkutano aliowaandalia leo Mei 30, 2014 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam kuzungumzia michango katika Kapu la Afya (Health Basket Fund) pamoja na mpango wa serikali wa kuiingiza sekta ya afya katika kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa saba kutoka kushoto) akiwa katika mazungumzo na mabalozi na wawakilishi wan chi washirika wa maendeleo katika mkutano aliowaandalia leo Mei 30, 2014 katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro hotel jijini Dar es salaam kuzungumzia michango katika Kapu la Afya (Health Basket Fund) pamoja na mpango wa serikali wa kuiingiza sekta ya afya katika kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN)
PICHA NA IKULU

KAMATI TENDAJI YA TAIFA YA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII TASAF, YAZURU KIBAHA, PWANI.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga (aliyesimama)akitoa ufafanuzi juuya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kwa walengwa wa Mpango huo(hawapo pichani).
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha mkoani Pwani Tatu Seleman(mwenye miwani) akiangalia moja ya mikeka iliyosukwa na walengwa wa Mpango waKunusuru Kaya masikini,PSSN, katika kijiji cha Vikuge kama njia mojawapo ya kukuzakipato cha wananchi.
Walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika kijiji cha Vikuge wilaya yaKibaha mkoani Pwani wakiwa katika mkutano uliohudhuriwa pia na wajumbe wa kamatitendaji ya TASAF (hawapo pichani) iliyotembelea kijiji hicho kukagua shughuli za Mpangohuo zinavyoendelea.
Karibu wageni hivi ndivyo anavyoelekea kusema Mkuu wa mkoa wa Pwani MwantumuMahiza(aliyeko mbele ya wajumbe) wakati alipowakaribisha wajumbe wa kamati tendaji yaTASAF iliyomtembelea ofisini kwake kabla ya kutembelea vijiji vya Vikuge na Misufinikukutana na walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini,PSSN.
Kaimu mwenyekiti wa kamati tendaji ya TASAF Abbas Kandoro (katikati) akisisitizajambo mbele ya Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza (aliyevaa kilemba) wakatiwajumbe wa kamati hiyo walipomtembelea mkuu huyo wa mkoa wa Pwani ofisini kwakekabla ya kutembelea vijiji vya Vikuge na Misufini katika wilaya ya Kibaha kukaguwashughuli za walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya masikini unaoratibiwa na TASAF,kushoto kwa Kandoro ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga
Kamati Tendaji ya Taifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, yazuru Kibaha, Pwani.
Wajumbe wa kamati tendaji ya Taifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii,TASAF wamefanyaziara katika vijiji vya Vikuge na Misufini katika wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani kuonanamna walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini na zinazoishi katika mazingirahatarishi,PSSN, wanavyonufaika na mpango huo.
Kabla ya kutembelea vijiji hivyo wajumbe wa kamati hiyo walikutana na mkuu wa mkoawa Pwani Mwantumu Mahiza ambaye alionyesha kuridhishwa kwake na namna TASAFinavyochangia jitihada za wakazi wa mkoa wake kupambana na umasikini.
Mkuu huyo wa mkoa wa Pwani amesema mabadiliko ya kujivunia yameanza kuonekanakatika nyanja za elimu, afya,makazi na hata uchumi hususani kwenye maeneo ambayoTASAF inatekeleza mpango huo wa PSSN.
Katika vijiji vya Vikuga na Misufini walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikiniwamebainisha kuwa mpango huo umesisimua kwa kiwango kikubwa shughuli zamaendeleo miongoni mwao huku wakibainisha kuwa hata uwezo wa kuwahudumia watotokwenda shule na kupata huduma za afya umeongezeka.
Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo tendaji ya TASAF, ABBAS KANDORO akizungumzana walengwa wa mpango huo amewataka kutobweteka na mafanikio waliyoanzakuyapata kutokana na mpango huo wa TASAF bali waendelee kuongeza juhudi katikauzalishaji mali ili hatimaye waweze kujikwamua kutoka katika dimbwi la umasikini.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga amebainisha kuwa taratibuzinakamishwa ili hatimaye watoto walioko katika kaya masikini ambao wamefaulukujiunga na masomo ya sekondari waweze kuhudumiwa kupitia Mpango wa kunusurukaya masikini kuanzia mwezi Julai mwaka huu.
Mwamanga amesema hali hiyo imetokana na Mfuko kubaini kuwa idadi kubwa ya kayamasikini zilizoingizwa kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini watoto waowameitikia wito wa kuhudhuria masomo kama mojawapo ya masharti na hivyo wengiwao kufaulu kujiunga na masomo ya sekondari lakini changamoto iliyoko ni uwezomdogo wa kaya husika kuwasomesha watoto hao katika ngazi ya sekondari.
Wajumbe wa kamati tendaji ya TASAF chini ya mwenyekiti wake mpya FlorensTuruka ambaye pia ni katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu leo na keshowanahudhuria kikao cha bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

RAIS KIKWETE AKUKATANA NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA BAN KI MOON

Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi alioongozana nao wakiendelea na maongezi katika mkutano na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bw. Ban Ki Moon uliofanyika katika hotel ya  
and his delegation meet and hold talks with U.N. Secretary General Ban Ki Moon at Royal York hotel in Toronto Canada this afternoon during the three days Summit on Maternal,Newborn and Child Health with the theme”Saving every woman and every child” at the invitation of their host Canadian Prime Minister Right Honorable Stephen Harper(photo by Freddy Maro)

BUNGE LASISITIZA JENGO LA GHOROFA 16 DAR LIVUNJWE

HAYO yamo katika taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Bunge limesisitiza kuwa jengo la ghorofa 16 lililoko katika Mtaa wa Indira Gandhi, Dar es Salaam ambalo liliagiza mwaka jana livunjwe, agizo hilo litekelezwe.
Aidha, imeishauri Serikali kutaifisha maeneo yote makubwa yasiyoendelezwa na kuyagawa kwa wananchi kwa matumizi mengine.
Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya (CCM) akisoma taarifa hiyo bungeni jana, alisema, “suala hili tuliliagiza katika bajeti iliyopita na tunazidi kusisitiza utekelezaji huu ufanyike mara moja.”
“Kamati inasikitikishwa kwamba agizo hili halijatekelezwa. Kamati inaiagiza Serikali kulifikisha suala hili kwa Rais haraka ili lipatiwe ufumbuzi kabla ya madhara kutokea,” alisema Bulaya.
Kuhusu ardhi, ilishauri Serikali kuondoa mianya inayotoa fursa na ushawishi mbovu kwa viongozi na watu wachache wasio na nia njema kwa maslahi ya Taifa, bali kujilimbikizia mali kwa maana ya Taifa kwa kutumia mgongo wa Serikali.
“Aidha, Kamati inaishauri Serikali kutaifisha maeneo yote makubwa yasiyoendelezwa na kuyagawa kwa wananchi kwa matumizi mengine,” alisema Bulaya.
Kuhusu Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Kamati iliishauri Serikali kupitia Wizara ya Fedha ione umuhimu wa kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa nyumba zinazojengwa na shirika kwa ajili ya kuuza kwa wananchi wa kipato cha chini na kati.
Pia, ilisema licha ya Serikali kuondoa VAT na ushuru wa Forodha kwa shirika NHC kwa vifaa vya ujenzi inavyoagiza nje, inaishauri kuliondolea pia shirika hilo VAT kwa vifaa vya ujenzi vinavyozalishwa nchini.
Aidha, imeitaka Serikali kulipa deni lililobaki la Sh 4,226,957,203.65 kwa NHC kutokana na madeni ya Wizara, Taasisi na Idara za Serikali.

TAARIFA YA MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LIMITED, DKT REGINALD MENGI, KWA UMMA

Mimi ni miongoni mwa Watanzania walio mstari wa mbele wanaomuunga mkono Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusisitiza kuwa rasilimali za asili zilizopo nchini ni mali ya Watanzania na ni lazima wawe wamiliki wakuu wa rasilimali hizo ikiwa ni pamoja na gesi asilia. Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliwahi kusema mwaka 1974 katika andiko lake la “Ujamaa ni imani” ukurasa wa 31, kwamba: “madini au mafuta yalio chini ya ardhi, n.k. vitu hivi ni mirathi ya wananchi wote”.
Katika miaka ya hivi karibuni dhana hii ya Watanzania kuwezeshwa na kumiliki uchumi wa nchi yao imetambuliwa na Serikali na Chama tawala kama ifuatavyo:
Sera ya Taifa ya Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004 inasema kwamba:

Aya ya 1.5 TAFSIRI YA WANANCHI
“Walengwa wa Sera ya Uwezeshaji ni Wananchi. Makampuni ya Wananchi ni yale ambayo yamesajiliwa Tanzania ambayo walengwa wanamiliki asilimia isiyopungua hamsini ya hisa zote za makampuni hayo. Sera ya Uwezeshaji itajumuisha wakulima, wafugaji, wavuvi, wafanyakazi na wafanyabiashara katika sekta mbalimbali na makundi mengine.” 

Aya ya 3.1 DIRA
“Uwezeshaji wa wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za uchumi ni sehemu ya Dira ya maendeleo ya Taifa kufikia mwaka 2025. Kufikia wakati huo, sehemu kubwa ya uchumi wa Tanzania inatarajiwa kumilikiwa na Watanzania wenyewe. 

Aya ya 4.1.2 TAMKO LA SERA
“Jitihada za kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za uchumi nchini ni muhimu ziendane na ukuaji wa uchumi unaojumuisha na kunufaisha Watanzania wengi, kuongeza vipato vyao pamoja na kuinua hali zao za maisha.”
Nayo Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Kiuchumi ya mwaka 2004 (National Economic Empowerment Act, 2004) katika utangulizi inasema:
“Economic empowerment is a central means for bringing about economic growth and social justice among our people that is necessary for the promotion of peace, tranquility and social stability that has characterized our society.” 

Tafsiri yake ni kama ifuatavyo:
“Uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi ni njia kuu ya kukuza uchumi na kuleta haki miongoni mwa jamii, mambo ambayo ni ya lazima katika kudumisha amani, utulivu na mshikamano, ambayo ni tunu ya asili ya jamii yetu.” 
Chama tawala, CCM katika “Mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka ya 2010 hadi 2020” kimetamka kwamba:

Aya ya 84 UWEZESHAJI WA WANANCHI KIUCHUMI
‘’Chama Cha Mapinduzi katika sera zake za msingi kama zilivyoainishwa katika Mwelekeo wa Sera za CCM katika Miaka ya Tisini na Mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka 2000-2010, kimetamka bayana kwamba, mkakati mkuu wa uwezeshaji wa kiuchumi wa wananchi ni ule unaohakikisha kwamba wananchi wenyewe wanamiliki na kuendesha uchumi wa nchi yetu ama mmoja mmoja, kwa kupitia vyama vyao huru vya ushirika wa aina mbalimbali au kwa kupitia makampuni ya wananchi ya ubia ambamo maelfu ya wananchi watanunua hisa”

Aya ya 103
“Wakati umefika wa kuweka mazingira bora ya upendeleo kwa Watanzania, kama inavyofanyika katika nyanja za kimataifa kwa mfano katika utoaji wa kandarasi za ujenzi, manunuzi n.k. Kuwapendelea Watanzania katika ajira na biashara nchini ni njia mojawapo ya kuwawezesha kiuchumi.”
Kwa msingi huo nimekuwa nikiishawishi Serikali kutekeleza sera na sheria ya uwezeshaji ili kuwashirikisha Watanzania kikamilifu katika uchumi wa Taifa, na kwa sasa hasa katika uchumi wa gesi asilia, ili kudumisha amani na utulivu katika nchi yetu.
Jitihada zangu zimekuwa zikipingwa na kiongozi wa moja za Wizara za Serikali na amekuwa akitumia mbinu na visingizio mbalimbali. Naamini kwamba usambazwaji wa uzushi unaofanyika sasa ni mwendelezo wa mbinu hizo chafu. Mtanzania yeyote hastahili kuwa kwenye uongozi katika ngazi yoyote kwa staili ya kudharau na kutukana Watanzania akidhani kwamba kwa kufanya hivyo atajijengea umaarufu. Jambo ambalo Watanzania wengi wanajiuliza ni kwamba ujeuri tunaoushuhudia unatokana na ulevi wa madaraka au ulevi wa fedha ama vyote viwili? 
Rai yangu kwa Watanzania ni kupuuza uzushi unaosambazwa, na kwamba wasikubali kuondolewa kwenye hoja ya msingi ya kutaka kujua namna serikali yao itakavyotekeleza sera na sheria ya uwezeshaji ili kuhakikisha kuwa inawashirikisha katika mchakato mzima wa uchumi wa gesi asilia, kuanzia hatua ya utafutaji na uchimbaji (up-stream) hadi uchakataji na usambazaji (midstream and downstream). 
Na kwa wale wanaotumiwa na kiongozi huyo ningependa kuwasihi wawe na uzalendo na mapenzi kwa nchi yao na wakatae kutumiwa kwenye mambo ya uongo yasiyo na tija kwa taifa letu.
Kinachonipa faraja katika juhudi zangu za kutetea maslahi ya Watanzania ni maneno ya Mhe. Rais Dkt. Kikwete aliyoyasema mnamo mwaka 2009 kwamba: 
“Midomo ya Wanadamu imeumbiwa kusema na wakati mwingine wanasema wanachokifikiria wao hata kama huo siyo ukweli, lakini watauamini, wataueneza uongo huo na watakuhukumu kwa uongo wao.” 
Dkt Reginald Mengi
28 Mei, 2014

KESI YA ZITTO KABWE DHIDI YA BARAZA LA WADHAMINI LA CHADEMA,DKT. SLAA KUSIKILIZWA JULAI 31

 
Na Mwene Said
MAHAKAMA Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imepanga kusikiliza mapingamizi ya awali ya pande zote mbili katika kesi iliyofunguliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe dhidi ya Baraza la Wadhamini la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Katibu Mkuu, Willbrod Slaa, Julai 31, mwaka huu.
Mheshimiwa, Jaji John Utamwa alisema kesi ilipangwa jana kwa ajili ya kutajwa na kwamba itasikilizwa mapongamizi ya awali ya pande zote mbili Julai 31, mwaka huu.
Hata hivyo, wakati kesi hiyo ikitajwa jana, alikuwepo wakili Peter Kibatala wa Chadema lakini Zitto na wakili wake hawakuwepo mahakamani.
Katika Kesi hiyo, Zitto anaiomba mahakama kuiamuru kamati kuu na chombo chochote kisijadili uanachama wake hadi rufaa yake itakaposikilizwa katika Baraza Kuu la Chama.Aidha, mbali na kesi hiyo ya msingi, Jaji John Utamwa alisikiliza maombi ya Zitto akiitaka itoe zuio la muda la kutojadiliwa uanachama wake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Mahakama ilikubali katika uamuzi wake iliamuru Zitto asijadiliwe chochote kuhusu uanachama wake.
Aidha, Zitto ameiomba mahakama imwamuru, Dk. Slaa kumkabidhi nakala za taarifa na mwenendo mzima wa vikao vilivyomvua uongozi ili akate rufaa katika ngazi ya juu ya chama hicho.
Zitto kupitia wakili wake Albart Msando aliomba mahakama itoe zuio la muda la Kamati Kuu na vikao vingine vya chama kutojadili suala la uanachama wake hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

ROSTAM AZIZI KATIKA MSIBA MKUBWA

ALIYEKUWA mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, (CCM), amefiwa na baba yake Aziz Abdulrasool (73) jijini Dar es Salaam jana asubuhi. Akizungumza nyumbani kwa marehemu Oysterbay jana, mtoto wa pili wa marehemu, Akram Aziz, alisema baba yake alifariki saa 12 asubuhi ikiwa ni saa mbili tu baada ya kurudishwa nchini kutoka Ufaransa alikuwa anatibiwa. “Baba amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani,tumemrudisha nchini jana saa 10 alfajiri kutoka Ufaransa, lakini ilipofika saa 12:30 alifariki dunia. 

“Baada ya kugundulika kuwa na saratani, alianza matibabu Nchini Ufaransa na Kurudi hapa Nyumbani…Mara ya mwisho baba alipelekwa nje miezi miwili iliyopita, lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya akaomba tumrudishe nyumbani ili awe karibu na ndugu na mafariki zake,”alisema Akram. 
Marehemu alizikwa jana katika makaburi ya Kisutu, saa 10 jioni jijini Dar es Salaam na amewacha wajane watatu,watoto 17 na wajukuu nane.

MELI YA JAPAN ILIYOLIPUKA BANDARINI.

Mlipuko mkubwa umetokea kwenye meli kubwa ya mafuta nchini Japan katika Pwani ya Kusini Magharibi mwa bandari ya Himeji na kusababisha mtu mmoja kati ya wanane waliokuwa ndani ya meli hiyo kupotea huku wengine wanne wakijeruhiwa vibaya.
Moto mkubwa ulilipuka katikati ya bahari ambapo meli hiyo yenye uzito wa tani 998 iliyokuwa ikitokea mji wa Hiroshima kuachwa ikielea ndani ya maji baada ya ajali hiyo na baadae kufatwa na meli za kupambana na majanga ya moto.
Watu saba wameokolewa katika ajali hiyo mbaya, wanne wakiuguza majeraha ya moto kwa mujibu wa shirika la habari la NHK, ambapo kapteni wa meli hiyo amesema uchunguzi kumtafuta mtu mmoja aliyepotea bado unaendelea.
Afisa usalama katika Pwani hiyo Koji Takarada amesema chanzo cha mlipuko huo bado hakijajulikana ambapo shirika la habari NHK limeripoti kuwa wafanyakazi wa meli hiyo walikuwa wakifanya kazi chini ya meli wakati mlipuko unatoke.

SAFI SANA NKAMIA, KUNA HAJA GANI YA KUJIITA `SIMBA` WAKATI UWEZO WAKO NI KAMA `SUNGURA`

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
SERIKALI kupitia wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo inatarajia kuliagiza shirikisho la soka Tanzania kuachana na mpango wake wa kubadili jezi na jina la timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Naibu waziri wa wizara hiyo, Juma Suleiman Nkamia, mwanahabari kitaalum na mtangazaji wa zamani wa michezo TBC, amesema hakuna haja ya kubadili jina, kikubwa ni kuubadilisha mchezo wenyewe ili twende sambamba na dunia ya sasa.
Hata hivyo, Nkamia alisema serikali inaendelea na jitihada zake za kujenga na kuimarisha miundombinu ya michezo kulingana na uwezo wake.
Watu walisema mapema kuwa TFF kwasasa hawana haja ya kuhangaika kutafuta jina jipya kwa timu ya taifa hususani jina linalotisha kama ilivyo kwa nchi za Magharibi.
Ukisikia majina ya nchi kama Ivory Coast, Nigeria, Senegal, Morroco, Cameroon na nyinginezo, lazima uhofie kabla ya kukutana nazo.
Tembo wa Afrika (Ivory Coast) , Simba asiyefugika (Cameroon), Simba wa Teranga (Senegal), kweli ni majina yanayovutia na kuogopesha, lakini ukweli ni kwamba mataifa haya kweli yako vizuri kisoka.
Huo ndio ulikuwa mwonekano wa jezi ya Taifa stars kabla ya kubadilishwa siku za karibuni
Majina yao yanatisha na wanatisha kweli wakiingia uwanjani. Kwahiyo majina yao yanasadifu uwezo wao uwanjani.
Inapokuja kwa nchi kama Tanzania, kuna haja gani ya kuhangaika kutafuta jina la kutisha wakati timu yenyewe imedoda kwa miaka mingi.
Leo hii unaona Taifa Stars halifai, kwani ukitafuta jina linalotisha litakusaidia nini wakati wewe hutishi.
Kuna mambo mengi ya kufanya katika soka letu kwasasa na jukumu kubwa ni kutafuta mfumo mzuri wa soka la vijana na kuboresha miundo mbinu.
Tunategemea kwasasa viongozi wahangaike na ujenzi wa vituo vya michezo, vyuo vya michezo ili kulijenga soka la vijana kama walivyofanya Nigeria, Ivory Coast, Ghana na kwingineko.
Msingi wa mpira unajengwa katika soka la vijana na sio kuhangaika na vitu vidogo kama kubadilisha jina la Taifa stars na mipango kama maboresho ya Taifa Stars. Mipango ya muda mfupi haifai, njia za mkato kama hizi hazina maana kwasasa.
Serikali ipo sahihi inaposema hakuna haja kabisa ya kubadili jina na wadau wengi wanaamini hilo.
Kuna haja gani mtu kujiita Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, wakati kiwango chake hakisadifu jina.
Watanzania tunapenda kujipachika majina ya watu maarufu, lakini hatufanyi jitihada za kutafuta kuelekeana na majina yenyewe.
Utashangaa mtu wanayemwita Ronaldo au Messi anavyojihangaisha na mambo ya `kipuuzi`. Hana jitihada yoyote wala haendani na jina lenyewe.
Kuna haja ya kuachana na utamaduni wa kupachikana au kujipachika majina makubwa ambayo hatuwezi kuyabeba.

AL-MERREIKH KUKINUKISHA ROBO FAINALI CECAFA NILE BASIN CUP LEO, MBEYA CITY KESHO HAPATOSHI

Kocha bora wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014, Juma Mwambusi (kulia)
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
ROBO fainali ya michuano ya CECAFA Nile Basin Cup inayoendelea kushika kasi nchini Sudan inatarajia kuanza kuunguruma leo jioni mjini Khartoum kwa mechi mbili kupigwa katika uwanja wa Merreikh.
AFC Leopard waliomaliza wa kwanza katika kundi B kwa kukusanya pointi 9 (ushindi wa asilimia 100) watakabiliana na Defence ya Ethiopia majira ya saa 12:30 jioni kwa saa za Sudan.
Usiku saa 2:30, wenyeji Al-Merreikh walioshika nafasi ya kwanza kundi A Kwa kujikusanyia pointi 7 watakuwa na kibarua cha kufa mtu dhidi ya Academie Tchite ya Burundi.
Robo fainali za pili zitaendelea kesho jumamosi (Mei 31) ambapo mechi ya kwanza itakayoanza saa 11:30 jioni itakuwa baina ya wagonga nyundo wa Mbeya, Mbeya City fc dhidi ya Victoria University ya Uganda.
Wawakilishi hao wa Tanzania walimaliza hatua ya makundi kwa kushika nafasi ya pili kundi B baada ya kujikusanyia pointi 4 katika michezo mitatu.
Mbeya City walianza kampeni zao kwa kuwafunga Academie Tchite mabao 3-2, mechi ya pili wakalala kwa mabao 2-1 dhidi ya AFC Leopard na mechi ya mwisho walitoka suluhu na Entincelles.
Ushindi katika mechi hiyo ni muhimu kwa kocha Juma Mwambusi kwani kucheza nusu fainali itakuwa historia nzuri ikizingatiwa ni mara yao ya kwanza kucheza michuano mikubwa ya kimataifa.
Hata kama walishiriki mapinduzi Cup mwanzoni mwa mwaka huu visiwani Zanzibar na kukutana na timu za nje ya nchi, michuano ya Nile Basin Cup inashirikisha timu nyingi za kigeni.
Kwa maana hiyo, Mbeya City wanahitaji ushindi ili kuwafurahisha watanzania wanaowaombea dua kila kukicha.
Mechi ya pili itaanza majira ya saa 2:00 usiku kwa kuwakutanisha Al-Shandi dhidi ya Malakia FC.

MADOGO WA U15 TANZANIA WASHIKA NAFASI YA PILI AYG

Na Boniface Wambura, Dar es salaam
TANZANIA imeshika nafasi ya pili kwenye Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) kwa upande wa mpira wa miguu kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 baada ya jana (Mei 29 mwaka huu) kuilaza Afrika Kusini mabao 2-0.
Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa SSKB jijini Gaborone ambapo kwa matokeo hayo Tanzania imetwaa medali ya fedha baada ya kushika nafasi ya pili. Nigeria ndiyo ilishika nafasi ya kwanza na kutwaa medali ya dhahabu.
Tanzania imemaliza ikiwa na pointi kumi ambapo ilishinda mechi tatu, sare moja na kupoteza moja mbele ya Nigeria.
Katika mechi ya kwanza ilitoka sare ya bao 1-1, ikawafunga Botswana 2-0, Swaziland wakachapwa 3-0 na baadaye kuwafunga Afrika Kusini 2-0. Timu ya Tanzania inayofundishwa na kocha Abel Mtweve ilifungwa na Nigeria mabao 2-0.
Wachezaji 16 waliounda kikosi hicho cha Tanzania katika michezo hiyo inayomalizika leo (Mei 30 mwaka huu) ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos Manguli, Amri Nyuki, Amede Amani, Baraka Rashid, David Uromi, Goodlove Mdumule, Hance Msonga, Kelvin Kamalamo, Makalius Amrin, Nasson Chanuka, Paulo Ngowi, Petro Shaban, Rajab Mohamed na Thomas Chindeka.
Nchi nyingine zinazoshiriki michezo hiyo kwa upande wa mpira wa miguu ni Afrika Kusini, Botswana, Nigeria, Mali na Swaziland wakati Gabon na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) zilijitoa dakika za mwisho.

ZILIZOSOMWA ZAIDI