NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Tuesday, February 24, 2015

HUDDAH MONROE ACHAFUA TENA HALI YA HEWA, MASHABIKI WAMCHANA BAADA YA KUTUPIA PICHA YA UTUPU AKIWA KITANDANI! (18+YRS)

Huddah Monroe ameshajikubali kuwa ni ‘good girl gone bad’ na ndio maana haoni tatizo kuweka picha akiwa kitandani kama alivyozaliwa.
Mrembo huyo wa Kenya amepost picha kwenye akaunti yake ya Facebook akiwa kitandani huku akiwa amejifunika na shuka sehemu ndogo tu ya mwili wake kuficha sehemu ny*ti.
Mashabiki wake hawakusita kumchana.
“Dnt you fear God?oh I like your beauty and en everything mash Allah but this idea of being naked subhanallah stop it.You are a good girl hudda you can change if you want,” aliandika Shankaroon A. Mohammed.
“Wajameni u mean ur whoring for real?? Oh my… please stop proving ppl right n be decent now that uv achieved what u wanted… n be quiet, if not for anything else then respect your clientèle. This is wrong,” ameandika Brenskie La’femme.

Sunday, February 22, 2015

AMBER ROSE AMJIBU KANYE WEST: ALIPOOGA MARA 30 ILI KUWA NA KIM BAADA YA KUACHANA NAYE

 
KWENYE mahojiano na kipindi cha ‘BreakFast Club’ Kanye West alimkejeli mpenzi wake wa zamani Amber Rose kwa kusema alibidi aoge mara 30 baada ya kuwa naye ili Kim kardashian awe naye.
Kanye West alisema “Kim k angekubali kuwa na mimi kabla ya Amber basi nisinge kuwa na Amber Kabisa, ni ngumu kwa mwanamke kuwa na mwanaume aliyewahi kuwa na mahusiano na Amber, nilibidi nioge mara 30 ili Kim K anikubali”.
Amber amejibu kupitia twitter yake nakusema …

KANYE WEST AFUNGUKA KUHUSU ALBUM MPYA LICHA UBORA WA MUZIKI WAKE KUWEKWA KIKAANGONI

Kwenye interview na kipindi cha ‘BreakFast Club’ kwenye kituo cha Power 105.1 Kanye West amesema “Album yake mpya imekamilika kwa asilimia 80 tu mpaka sasa, na anajaribu kuimalizia na kuwapa watu”.
Kuna uwezekana ikatoka kwa mtindo wa kushtukiza kama ilivyotoka album ya Drake na Beyonce

LULU AINGIA KATIKA 'TOP 10' YA WAIGIZAJI WA KIKE WENYE MVUTO AFRIKA! *PICHAZ*

Tasnia ya filamu Afrika inakuwa kila siku kiasi kwamba zile ndoto za kufanya kama wenzetu wa 


Hollywood
   (Marekani) na Bollywood (India) huenda siku moja zikatimia.

Kama ilivyo Hollywood na kwingine kwenye waigizaji wa kike wenye mvuto, wapo pia waigizaji wa kike Afrika ambao ni ‘visu’.Leo hii ikihitajika Top 10, kila mmoja atakuwa na yake lakini mtandao wa umefanya kazi ya kuorodhesha waigizaji 10 wa kike wenye mvuto kama ifuatavyo;

10. Elizabeth Michael ‘Lulu’


Binti huyu ana umri wa miaka 21 lakini ni mrembo na anayejiamini. Ni binti kutoka Tanzania mwenye kipaji cha kuigiza kiasi cha kuwa tishio kwa wakongwe. Ni kweli huwa anatumia ‘make up’ lakini hata akiwa hajatumia wala kuvaa ‘mawig’, bado anaonekana ni mwenye kuvutia.

9. Omotola Jalade Ekeinde.


Ni mmoja wa mastaa wa kike nchini Nigeria mwenye mvuto wa aina yake. Kwa sasa ana umri wa miaka 37 na watoto wanne lakini bado anaonekana mrembo kiasi cha baadhi ya mashabiki wake kumuita Omosexy.Kutokana na kipaji alicho nacho, amejikuta akiwa na mashabiki wengi katika Bara la Africa na kwingineko duniani. Mbali na uigizaji pia ni mwanamitindo na mwananamuziki.

8. Chinyere Yvone Okoro


Huyu ni muigizaji anayetokea nchini Ghana. Katika orodha ya waigizaji wa kike waliomo nchini humo, mrembo huyu amebaki kuwa tishio na imemfanya kuingia katika orodha hii ya wasanii wa kike wakali Afrika.

7. Jackline Wolper.


Huyu ni muigizaji kutoka Tanzania mwenye mvuto wa aina yake. Kwa mujibu wa maelezo yake, uzuri alionao unatokana na mfumo mzuri wa kula aliojiwekea. Anakula sana mbogamboga, matunda na maji mengi, hali inayomfanya autunze urembo alionao.

6. Genevieve Nnaji.


Ana umri wa miaka 36, anatokea Nigeria. Mwanadada huyu anatajwa kuwa na mvuto wa aina yake kiasi cha kupata usumbufu kutoka kwa wanaume kibao.Ameigiza filamu nyingi na zote amezitendea haki kutokana na namna anavyouvaa uhusika.

5. Jackie Appiah Agyemang.


Amezaliwa miaka 32 nchini Canada lakini amekulia nchini Ghana. Ni binti mrembo na mwenye kipaji ambaye aonekanapo kwenye televisheni, huthibitisha kwamba kuna kitu cha ziada alichojaaliwa na Mungu.

4. Nadia Buari.


Huyu ni msanii kutoka Ghana aliyezaliwa miaka 30 iliyopita. Licha ya umri kusogea, hachuji kwa uzuri. Amecheza filamu nyingi na kadiri siku zinavyokwenda ndivyo anavyozidi kuwa tishio kwenye tasnia ya uigizaji.

3. Ini Edo.


Hivi unaanzaanzaje kumuacha mrembo huyu pale unapotaja medemu wakali kwenye tasnia ya filamu Afrika? Naamini huwezi, labda uwe na chuki zako binafsi.Ana umri wa miaka 31 na ana uzuri wa asili unaomfanya atumike kwenye filamu nyingi za Nigeria.

2. Stephanie Okereke Linus.


Huyu ni binti kutoka Nigeria ambaye wengi wanamtaja kuwa muigizaji mwenye mvuto kuliko wote Afrika. Ana miaka 33, aliwahi kushiriki mashindano ya urembo nchini Nigeria na kuibuka mshindi. Kuanzia hapo amekuwa gumzo kwa uzuri wake na amekuwa akitumika sana kwenye filamu nyingi.

1.Rita Dominic.


Wafuatiliaji wa filamu za Nigeria watakuwa wanamjua vizuri binti huyu. Ana miaka 40 lakini bado anadai. Kila sehemu ya mwili wake ina muonekana wa kiurembo.



Angalia midomo yake, angalia macho na ngozi yake. Hakika ni kati ya waigizaji wa kike Afrika wenye mvuto wa aina yake.

AMBER ROSE ALIPOACHIA *PICHAZ* ZA KU#BREAKTHEINTERNET TENA! (+18YRS)

 Mwanamitindo aliyekuwa mke wa rapa Wiz Khalifa Amber Rose ’31’ amerudia tena mtindo wake wa ku BreakTheInternet kwa kuweka picha zake akiwa kwenye pozi tofauti.
Mara ya kwanza Amber kufanya hivi ilikuwa August 2014 wakati album ya mume wake Wiz Khalifa ‘Blacc Hollywood’ ilivyoshika namba moja kwenye chati za Billboard hot 200.




MSHUHUDIE ANAYEDAIWA KUWA MKUU MPYA WA WILAYA MOJA NCHINI…NI SHIIIIDAH *PICHAZ*

Jana Siku Nzima Msichana huyu anayejulikana kama Nice Chande ama @mwakalicious24 amepaishwa sana kwenye mitandao ikisemekana kuwa Rais kamchangua kuwa Mkuu wa Wilaya 
Watu wengi waliguswa hasa kutokana na umbo lake matata ....Bado hatujapata ukweli wa jambo hili lakini haraka haraka nimeangalia majina ya wakuu wa Wilaya wapya sijaona jina lake labda awe anatumia jina jingine ...Jionee Picha zaidi Hapa Chini:



WATOTO WA KIZENJI KULA BATA KATIKA KIWANJA HIKI CHA KUFURAHISHA WATOTO TIBIRINZI *PICHAZ*








Picha za baadhi ya Mapembea, ambayo yameshafungwa katika Kiwanja cha kufurahishia Watoto Tibirinzi Kisiwani Pemba.
 Picha na MARYAM SALUM-PEMBA

TAARIFA: SEHEMU ULIPO MSIBA WA MEZ B & SIKU ATAKAYOZIKWA MKOANI DODOMA

MSIBA wa Ndugu yetu Mez B upo Maeneo ya Kisasa hapa Dodoma!!!Nashukuru kwa Ushirikiano wa Wasanii Wakongwe hapa Dodoma #‎MakoleHexagon#‎MazichiReality na wengne wote Mnaoshiriki Vyema Kutupatia Habari, wakiwemo wana Familia Wa Mez B na Team nzima ya #‎ChembaSquard....Mazishi ya Ndugu yetu ni Juma Tatu.....Hopeful Kwa Mlio Dodoma Mnaendelea Kupata taarifa zaid kupitia  Boss Ngas Tz na 97.7 Nyemo Fm,vile vile kwa mlio mbali basi ndo tunajuzana kama hivi!!!
NOTE: Marehem Mez B amefariki Nyumbani kwao, asubuh saa tano, mara baada ya kuomba aandaliwe chai,hvyo wakati ndgu yke anamuandalia chai,anaingia ndani hv, kutoka nje anamkuta Mez B kakakamaa na Tayari alkua Ameshafariki!!…..!
R.I.P MEZ B.

ICHEKI BRAND NEW VIDEO YA BARNABA & VANESSA MDEE - SIRI

Thursday, February 19, 2015

TUDD THOMAS KUWASIMAMISHA TENA DIAMOND PLATNUMZ NA NAY WA MITEGO *PICHAZ*

TUDD Thomas ndiye producer atakaye simamia kazi mpya ya wasanii Diamond Platnumz na Nay wa Mitego, Walikesha usikuwa wa kuamkia 19 Feb 2015. Wimbo utafanyika Surround Studios.

T.I AMFUNGUKIA MPENZI WA ZAMANI WA IGGY AZALEA KUTAKA NUSU YA PESA ZAKE


RAPA T.I. anayepewa hishima ya kumgundua msanii Iggy Azalea amesema mpenzi wa zamani wa Iggy ‘Jefe Wine’ hana haki ya kupata pesa yeyote kutoka kwa Iggy na muziki wake.
T.I. amesema ataacha tatizo la Iggy Azalea lishughulikiwe na wanasheria wake ila haoni sababu ya kijana huyo kupewa pesa za Iggy au kupokea malipo yeyote.
Siku chache nyuma TMZ iliripoti kuwa mpenzi wa zamani wa Iggy Azalea anasema walifunga ndoa mwaka 2008 na anashahidi ambaye ni daktari walioenda kumuona pamoja walivyokuwa mke na mume. Jefe anataka nusu ya pesa za Iggy Azalea.
Mwezi wa kumi mwaka jana Jefe alitaka talaka kutoka kwa Iggy na kusema waliishi kama mume na mke huko Texas toka September 2008.

ICHEKI BRAND NEW VIDEO YA STEVE RNB - ‘POLE POLE’


Hi video mpya ya Steve Rnb inaitwa Pole Pole, video imetayarishwa na Urban Videos

HUDDAH THE BOSS CHICK ATOA USHAHIDI WA KADI YA RANGE ROVER ANAYOIMILIKI *PICHAZ*

HUDDAH The Boss lady wa Kenya aliyewahi kushiriki BBA amewanyamazisha wale walioponda kuwa gari amepewa tu atembele ni kwamba sio yake kwa kuweka wazi kadi ya gari yenye jina lake.

CHEKI BRAND NEW VIDEO YA JAGUAR - HUU MWAKA


JINSI MWANAMKE ALIVYOMUUZA MAMA YAKE MDOGO RUVUMA


kivuli
Unaweza kujiuliza mara mbilimbili inakuaje mpaka mtu anapata ujasiri wa kumuuza mama yake mdogo? tena aliekamilika?

1. Mwanamke mwenyewe alieamua kumuuza mama yake mdogo, anaitwa Sophia Yasin Chambo (30) na ilikua February 17 2015 saa nane mchana maeneo ya Lizaboni, alikwenda nyumbani kwa Mfanyabiashara wa eneo hilo na kumwambia anahitaji kufanya nae biashara ili azidi kuwa tajiri.
2. Alimwambia anae mama yake mdogo na angehitaji kumuuza kwake ili amfanye kama zindiko biashara izidi kumuingizia pesa, alikubaliana kwamba atampeleka Mama mdogo akiwa kwenye gunia baada ya kumuua lakini Mfanyabiashara akasema anamtaka akiwa hai.
3. Walikubaliana bei ni Milioni 6.5 kutokea kwenye Milioni 10 aliyoanzia, kesho yake kweli Sophia alikwenda kumchukua mama yake mdogo aitwae Anita Kasim Mbawala mwenye umri wa miaka 40.
4. Unajua alimwambia nini mama Mdogo ili kumshawishi waende wote?? >>>> ‘Mama mdogo twende kuna sehemu Mwanaume amekupenda anataka kuishi na wewe, alikuona Iringa’ Mama mdogo akakataa na kusema hajawahi kuishi Iringa, baada ya kuona kagoma akamdanganya kuna watu wanataka akawafanyie kazi watamlipa vizuri sana ambapo mama mdogo alishawishika.
5. Walipofika Lizaboni kwa Mfanyabiashara Sophia alikamatwa sababu taarifa zilishawafikia Polisi tayari na mpaka sasa anaendelea kuhojiwa, upelelezi bado unaendelea na ukikamilika atafikishwa Mahakamani kutokana na biashara hii haramu ya kuuza binadamu.

PAUL MAKONDA AWAJIA JUU WANAOPONDA KWA KUTEULIWA KUWA MKUU WA WILAYA


Makonda ang’aka
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni , Paul Makonda (pichani) amesema wanaobeza uwezo wake kiutendaji baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo, wasubiri waone atakavyokuwa.
Aidha, ameweka wazi kile anachoamini anashutumiwa na kubezwa na watu kuhusu uteuzi huo na kusema wanaofanya hivyo, wanafahamu kwamba masuala yao kadhaa ndani ya wilaya hiyo yanayokwenda kinyume na taratibu, hayatafanikiwa.
Akiendelea kujibu wanaoshutumu uteuzi wake kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, alisema kwa sasa hawezi kutoa ahadi ni nini atafanya isipokuwa, anasubiri kuingia ofisini.
Akihojiwa katika kipindi cha asubuhi cha Redio ya Clouds, alisema pia anamsikiliza Rais atakachomwambia afanye kwa kuwa yeye ni mwakilishi wake wilayani humo.
Akizungumzia kuhusu taarifa za kupata nafasi hiyo kuwa gumzo katika jiji kuliko wakuu wengine wa wilaya, alisema inaonesha ni kwa jinsi gani watu wanatambua utendaji wake.
Alisema alipata taarifa za uteuzi huo wakati akitoa mada katika kikao cha kazi cha Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na kushangaa watu wakipeana taarifa.
“Kuna watu wanabeza uteuzi wangu kwa kuonekana nimepewa wilaya kubwa. Nataka kuwaambia wasubiri waone tu,” alisema na kutaka Watanzania kuacha tabia ya kumjadili mtu au jambo bila kufahamu vizuri.
Alisisitiza kuwa Watanzania wamekuwa na tabia ya kushabikia jambo wasilolijua au mtu wasiyemjua kwa kufuata mkumbo; jambo ambalo siyo zuri ni vyema kufahamu kwanza ndipo uweze kusema.
Akizungumzia baadhi ya vyombo vya habari vilivyotoa taarifa za uteuzi wake kwa kumdhihaki, alisema wamefanya hivyo kwa maslahi yao ya kuuza.
Pia alielezea uteuzi wake umekuwa gumzo, kutokana na uwezo wake wa kazi katika UVCCM pamoja na uwezo wake kwenye Bunge Maalumu la Katiba.
Uteuzi wa Makonda ambao umefanywa na Rais Kikwete, unaonesha kuwashitua wengi; hali ambayo imefanya watu wengi kumbeza hasa kupitia mitandao ya kijamii.
Baadhi ya wanaobeza, wanadai kwamba Makonda hana sifa ya kuongoza wilaya kubwa kama Kinondoni, ambayo ina changamoto na migogoro mingi ya ardhi.
Makonda ambaye ni Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa UVCCM, jina lake limekuwa kubwa hivi karibuni baada ya kutuhumiwa kushiriki kuvuruga mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, tuhuma alizokanusha.
Pia, kujitokeza kwake hadharani kumpinga mmoja wa watu wanaotajwa kuwania urais, kuliongeza jina hilo kuwa maarufu. Maisha ya Makonda pia ambaye baada ya kushindwa Umakamu Mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM, alitoa shutuma kuhusu uchaguzi huo na baadaye alirejeshwa ndani ya umoja huo kwa kupewa nafasi anayoshikilia sasa ya ukatibu wa uchipukizi na uhamasishaji.


MTU MWEUSI ALIYEBAGULIWA ATAKA HAKI


MTU aliyezuiliwa kuingia Paris Metro train na mashabiki wa timu ya mpira ya Chelsea kwa sababu ya ubaguzi wa rangi ametaka waadhibiwe.
Mtu huyo mwenye miaka 33 anayeitwa Souleymane S aliambia gazeti la Le Parisien:
“Hawa watu, hawa mashabiki wanapaswa kufungwa".
Video ilionyesha mtu huyo akizuiliwa kuingia kwenye Metro na akisukumwa na mashabiki hao.
Watu walisikika wakiimba: "Sisi ni wabaguzi wa rangi na hivyo ndivyo tupendavyo".
Kanda hiyo ya video ilitolewa na gazeti la the Guardian lililotoa ripoti kuwa tokeo hilo lilifanyika Richelieu-Drouot katika mji mkuu wa Fance siku ya Jumanne kabla mechi ya Champions Legue.

ISIKILIZE NA UIPAKUE NYIMBO YA IYANYA FT. DIAMOND - NAKUPENDA (I LOVE YOU)


Iyanya
Mara ya kwanza ilikua ni zamu ya Iyanya kushirikishwa na Diamond Platnumz lakini time hii ni zamu ya Diamond kushirikishwa na Mnigeria huyu staa wa hit single ikiwemo ‘Mr. Oreo
Iyanya ameamua kuiita hii single jina la Kiswahili ‘Nakupenda’ (I Love you) ambayo unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play hapa chini...!



CHUKUA HII MDADA: MADHARA YA KUCHORA TATTOO KIAFYA


TATTOO ni moja kati ya pambo kama mapambo mengine kama vile uvaaji hereni,cheni au kusuka.Wanawake huchora tattoo sehemu tofauti tofauti za mwili kutokana na mapenzi yake kwa mfano wengine hupenda kuchora shingoni,pajani,mkononi na kwabaadhi ya watu huthubutu kuchora hata katika sehemu zao za siri bila hata haya umeanika uchi wako kwa tattoo artist eti akuchore hapo sirini ,jamani watu wanahatari.
Kwa mdada wa kitanzania kwa hali ya kawaida kuchora tattoo sio jambo la kawaida sana kutokana na ukweli kwamba huu si utamaduni wetu bali ni utamaduni wan chi za kimagharibi kama vile Marekani,Uingereza na nyinginezo,ndio maana katika maeneo mengi hapa nchini kwetu ikitokea umemwona mdada amechora tattoo lazima utashtuka na kuna fikra hasi/mbaya zinakujia akilini juu ya tabia ya dada yule hata kama hunauhakika kama anatabia nzuri au mbaya, sijui kama hali hii imeshawahi kukutokea.
Uchoraji wa tattoo kwa mdada wa kitanzania si jambo la kujisifu wala si la kuona fahari eti utaonekana mjanja au mtu unayekwenda na wakati kwani katika jamii yetu hili si jambo lililozoeleka hivyo kwa kiasi kikubwa utakuwa unakutana na changamoto kadhaa achilia mbali matatizo ya kiafya ambayo unaweza kupata kama vile magonjwa ya kansa ya ngozi.
Miongoni mwa changamoto utakazokutana nazo ni kama vile kuhusishwa au kudhaniwa kuwa ni Muhuni na mtu mwenye tabia chafu ambaye hustahili kuigwa katika jamii.Watu watakuchukulia kama mtu uliyeshindikana hata kama katika hali halisi hauna hizo tabia kabisa,hivyo kama umejichora tattoo usije ukashangaa wanajamii wasipokupa ushirikiano wa kutosha katika baadhi ya mambo kwani unaonekana tofauti na wanajamii wengine wa kawaida.
Wanaume wenye maadili na hadhi ya kiafrika hakika hawatakuwa karibu na hata huwezi kumshawishi chochote kuingia katika uhusiano na mdada aliyejichorachora tattoo kwani huamini kuwa wewe ni muhuni na mchafu wa tabia,hivyo utapata changamoto kuolewa au kuwa katika uhusiano na watu wenye malengo ya kutengeneza familia badala yake utajikuta unaingia katika uhusiano na mwanaume mwenye akili za kimagharibi kama wewe ambaye si muoaji au mwenye tabia za ajabu ajabu ambao wamezoeleka kuitwa pasua kichwa.
Hivyo mdada wa kitanzania Urembo sio lazima ujichorechore tattoo kwani si sehemu ya utamaduni wetu,binti wa kiafrika hujitunza,hujithamini na kuheshimu watu wengine na ndio maana hata hao wazungu huwa wanawapenda sana wanawake hawa kuliko hata wazungu wenzao ambao wamejawa na tabia za ajabu ajabu zisizoweza hata kuvumilika na mzungu mwenzie 

HALI YA HEWA ILIVYO HUKO AMBONI, TANGA *PICHAZ*


 

ZILIZOSOMWA ZAIDI