Thursday, January 8, 2015

JESHI LA KONGO LAUNGANA NA UN KUPAMBANA NA WAASI WA FDLR

UMOJA wa Mataifa umesema Rais Joseph Kabila ameahidi kuwa jeshi lake litaungana na la UN katika operesheni dhidi ya waasi wa FDLR.
kikosi cha wanajeshi elfu 20 wa umoja huo watashirikiana na wale wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika kampeni zilizopangwa kuanza karibuni dhidi ya waasi wa Kihutu wa Rwanda.
Wanamgambo wa Kihutu, wanaojulikana kama FDLR, wamekuwa wakilitumia eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kama kambi yao ya kufanya mashambulizi dhidi ya serikali ya nchi jirani ya Rwanda.
Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Kongo (MONUSCO) tayari kimeanza kujitayarisha kwa ajili ya kufanya mashambulio makubwa dhidi ya waasi wa Rwanda wa FDLR walioko mashariki mwa Kongo baada ya waasi hao kushindwa kujisalimisha katika muda waliopewa.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI