UMOJA wa Afrika (AU) umetoa wito wa kupelekwa misaada zaidi ya kibinadamu nchini Somalia kufuatia mapigano ya hivi karibuni nchini humo.
AU imesema kuwa misaada zaidi inapaswa kupelekwa Somalia kwa kuwa hali ya kibinadamu imezorota kufuatia mapigano ya hivi karibuni kati ya askari wa kulinda amani wa umoja huo na wapiganaji wa kundi la as Shabab yaliyo pelekea watu wengi kuuawa na raia 46,000 kuwa wakimbizi.
Mapigano hayo yamepelekea kukombolewa wilaya 13 za kusini na katikati mwa Somalia zilizokuwa zikidhibitiwa na kundi hilo.
Kwa mujibu wa serikali ya Mogadishu, imekuwa vigumu kufika katika asilimia 70 za wilaya za Kusini na katikati mwa Somalia kwa njia ya nchi kavu kutokana na ukosefu wa usalama.
Somalia inahesabiwa kuwa miongoni mwa maeneo yenye migogoro mibaya zaidi ya kibinadamu duniani.
0 comments:
Post a Comment