Thursday, January 8, 2015

MAREKANI KUPAMBANA NA UKIMWI, AFRIKA: TANZANIANDANI

KATIKA kupambana na ugonjwa wa Ukimwi Barani Afrika Marekani inatarajia kutoa madawa ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi kwa zaidi ya watoto laki tatu wanaoishi na virusi vya ugonjwa huo.
Serikali kupitia Taasisi na mashirika mbalimbali hapa nchini zimekuwa zikifanya jitihada kubwa kukabiliana na janga la ukimwi kwa kutoa elimu kwa wananchi ikiwa ni pamoja na matumizi ya dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.
Nchi mbalimbali zimeonesha kuguswa na ugonjwa huo ambapo Marekani ni miongoni mwa nchi zinazotarajia kutoa madawa kwa watoto wanaoishi na maambukizi ya ugonjwa huo barani Afrika
Nchi hiyo imetangaza kwamba madawa hayo yatatolewa katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, barani Afrika, katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Hatua hiyo ni sehemu ya mpango wake wa dola milioni mia mbili zilizoandaliwa kwa ajili ya kupambana na virusi vya ukimwi na ukimwi.
Balozi wa Marekani, Deborah Birth amesema mpango huo utalenga pia kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Umoja wa Mataifa umesema asilimia 95 ya watoto walioambukizwa virusi vya ugonjwa wa ukimwi wanaishi katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI