MKURUGENZI mkuu wa FBI James
Comey amesema kitengo chake kimemtambua mtu ambaye huficha sura yake ambaye ni
muuaji,ambaye pia huoneshwa wakati akiwachinja mateka watatu kwenye video inayo
nadi wanamgambo wa dola ya kiislam IS.
Pamoja na hayo Bwana
Comey amegoma kuutaja uraia wa mtu huyo ama hata kutaja jina lake,ingawa
imeshajulikana lafudhi ya mtu huyo kuwa ni mwenye asili ya mji wa London, na
Comey amesema kwamba utambuzi wa mtu huyo umefanikishwa kwa msaada mkubwa wa
marafiki wa kimataifa.
Muuaji huyo wa
waandishi James Foley na Steven Sotloff pamoja na mfanyakazi wa kujitolea David
Haines walipigwa picha ya video na kuwekwa kwenye mitandao na wanamgambo hao wa
dola ya kiislam na kusaidia kufanya maamuzi juu ya mipango ya wapiganaji wa
jihad.
0 comments:
Post a Comment