Friday, April 18, 2014

JUMUIYA YA MUZDALIFAT YASHIRIKIANA NA TAASISI YA I.H.H KUWAPA SADAKA WATOTO YATIMA

Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifat(Muzdalifat Islamic Charitable) wakishirikiana na Taasisi ya I.H.H kutoka uturuki,wakichuna mbuzi waliokwisha kuchinjwa kwa ajili ya sadaka kwa Watoto yatima hafla iliofanyika huko Kisauni nje ya Mji wa Zanzibar. 
Wawakilishi kutoka Taasisi ya I.H.H ya Uturuki wakisalimiana na wanafunzi chekechea wa Skuli ya Muzdalifat mara baada ya kushuka kwenye gari huko Kisauni nje ya Mji wa Zanzibar.
Wawakilishi wa Taasisi ya I.H.H kutoka Uturuki wakigawa sadaka ya Unga, Mchele, Mafuta ya kupikia pamoja na Nyama kwa Watoto Yatima katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.
Wawakilishi wa Taasisi ya I.H.H,kutoka Uturuki wakiendelea kugawa sadaka ya Vitu mbalimbali ikiwa pamoja na Unga wa Ngano, Mchele, Mafuta ya kupikia na Nyama kwa Watoto mayatima walio katika maeneo mbalimbali Zanzibar. 
Picha na Yussuf Simai - Maelezo Zanzbar.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI