Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mh Dkt Fenella Mukangara akisoma hotuba fupi wakati wa hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd kwaajili ya Kuzindua Huduma ya Kuuza Filamu zake kupitia Mtandao. Akiongea na wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Southern Sun iliyopo Jijini Dar Es Salaam, Waziri ameisifia Kampuni ya Proin Promotions kwa kuweza kujitanua zaidi katika kutafuta soko la filamu zetu za kitanzania kuliko kutegemea kuuza DVD peke yake.
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mh Dkt Fenella Mukangara (Wa Kwanza Kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Bodi ya Filamu Tanzania Ms Joyce Fissoo(katikati) na Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin Mh Johnson Lukaza wakati waziri Mukangara akiwasili katika hoteli ya Southern Sun kwaajili ya Uzinduzi wa Huduma ya Kuuza Filamu za Kitanzania za Proin iliyoandaliwa na Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Filamu Tanzania ya Proin Promotions.
Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza akisoma hotuba fupi kwa Mgeni rasmi ambae pia Ni Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mh Dkt Fenella Mukangara wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kuuza filamu za Proin mtandaoni.
Mheshimiwa Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akisoma hotuba fupi mbele za waandishi wa habari na wageni waalikwa waliohudhuria hafla fupi ya Uzinduzi wa Mpango wa Kuuza Filamu za Proin Mtandaoni.
Mheshimiwa Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara (Wa pili kulia) akiangalia Moja ya treila ambayo ipo katika mtandao wa kununulia filamu za Kampuni ya Proin Promotions Ltd kupitia runinga kubwa kabla ya kuweza kuinunua filamu hiyo kupitia mtandao.Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Filamu Tanzania (Wa Kwanza Kulia) Mh Joyce Fissoo na Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin (Wa Kwanza Kushoto) Johnson Lukaza na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba.
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akisikiliza kwa makini hituba iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin, Mh Johnson Lukaza (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa kuuza filamu za kitanzania kupitia Mtandao.Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Bodi ya Filamu Tanzania, Mh Joyce Fissoo na Nyuma ni Mwesiga Lukaza
Kelvin Twisa Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano kutoka kampuni ya Simu za Mikononi ya Vodacom akiteta jambo na wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa kuuza filamu za Kampuni ya Proin Kupitia Mtandao
Muigizaji Emmanuel Muyamba Akiteta jambo na Mkurugenzi Wa Bodi ya Filamu Tanzania, ms Joyce Fissoo wakati wa hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa filamu za kitanzania uliozinduliwa na kampuni ya Proin Promotions Leo katika hoteli ya Southern Sun
Simon Mwakifamba akiagana na Mheshimiwa Waziri Mukangara
Aliyekuwa Host wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Elizabeth Michael almaarufu Lulu akiteta Jambo na Mmoja wa washiriki wa TMT 2014 Isalito Isaya wakati wa hafla hiyo fupi ya uzinduzi wa kuuza filamu za Kampuni ya Proin kupitia Mtandao
Naibu Balozi wa Rwanda akiteta Jambo na Wageni waalikwa katika uzinduzi huo uliofanyika katika hoteli ya Southern Sun
Wadau
Wafanyakazi wa Kampuni ya Proin Promotions wakipata u canon wa Lukaza Blog wakati wa Hafla fupi ya Uzinduzi wa Kuuza Filamu za Kitanzania Kupitia Mtandao.
Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
0 comments:
Post a Comment