Tuesday, January 20, 2015

‘WEMA ANIACHIE BOB JUNIOR WANGU' - BOZI


UBUYU! Siku chache baada ya kuripotiwa kwa tukio la staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu kunaswa kimalovee na Rais wa Masharobaro, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’, mwigizaji chipukizi, Bozi ameibuka na kudai ‘Wema niachie Bob Junior wangu’.
Kwa mujibu wa chanzo cha GPL, mara baada ya habari hiyo kuruka hewani kupitia gazeti tumbo moja na hili, Amani la wiki iliyopita, mrembo huyo alipoziona picha za wawili hao alipoteza fahamu.
Akizungumza na GPL huku akiangua kilio, Bozi alisema kuwa katika siku alizowahi kuumia ni siku hiyo alipoona Wema ametoka kwenye gazeti na mpenzi wake huyo.
Bozi alifunguka kwamba, alimbana Bob Junior kwa maswali lakini jamaa huyo hakutaka kumweka wazi kama yeye na Wema wanatoka.
#GPL

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI