Utafiti huo unaonyesha kuwa wanawake wanaonenepa maishani bila ya kuwa waangalifu wanajiweka katika hatari ya kupata Saratani.
WATAFITI kutoka chuo Kikuu cha London wanasema kwamba wanawake walio
kati ya umri wa miaka 24-28 ambao huendelea kunenepa kila baada ya miaka
10, wako katika hatari zaidi ya kupata Saratani ya Matiti baada ya
kupitisha umri wa kuzaa.
Sasa je ni nini ishara ya mwanamke kunenepa? Watafiti wanasema vipimo
vya sketi yake vinaweza kukusaidia kujua ikiwa uko katika hatari ya
kpatwa Saratni ya Matiti au la.
Kila unapogundua kuwa sketi yako inaendelea kuwa ndogo kiunoni, basi
inakubidi ujue kuwa mwili wako unaongekeza kwa unene. Na pia ni rahisi
kwa wanawake kukumbuka kipimo cha sketi kuliko kitu kingine chochote.
'Mfumo wa maisha'
Akizungumzia utafiti huo, Simon Vincet kutoka shirika la kupambana na
saratani ya Matiti la Breakthrough Breast Cancer, alisema kuwa saratani
ya Matiti miongoni mwa wanwake inaweza kupunguka ikiwa watu
watabadilisha mfumo wa maisha kwa kujiuzia kunenepa kupita kiasi na
kufanya mazoezi sana.
Utafiti huu unaangazia njia rahisi sana kwa wanawake kuwa waangalifu kuhusu unene wa miili yao.
Kuangalia kipimo cha sketi kati ya wanawake walio kati ya miaka 24 na 28
wenye miaki katikati ya 20 na zaidi wanaweza kuwa na njia rahisi ya
kufuatilia uzito wa miili ya Unene wa kupita kiasi unajulikana kwa
sababu ni hatari kubwa inayochangia katika ugonjwa wa saratani , hususan
mafuta ya yaliyoko tumboni.
Prof Usha Menon wa shirika lakupambana na satratani ya matiti, ndiye
aliyeongoza utafiti huo na kuambia BBC kuwa "Kama kipimo cha sketi
kinaweza kuthibitishwa na wengine kama kigezo cha wanawake watu wazima
kuapa Saratani, basi hii itakuw anjia nzuri na rahisi ya mtu kuwa
mwangalifu ili asinenepe kupita kiasi.
'Changamoto'
Watafiti hao walisema utafiti wao ulikuwa na changamoto kadhaa kwamba
uliangazia zaidi wanawake kukumbuka vipimo vya sketi zao tangu tangu
wawe na umri wa miaka 20
Lakini ikiwa matokeo ya utafiti huo yatathibitishwa, itakuwa njia rahisi
kwa wanawake kuelewa hatari zinazowakabili hasa wanapoendelea kunenepa.
Tom Stansfeld kutoka shirika la utafiti wa Saratani nchini
Uingereza,anasema utafiti huo unaweza kuaminika lakini unazingatia zaidi
wanawake kukumbuka vipimo vya sketi walizovalia miaka ya zamani.
Utafiti unasema kuwa baadhi ya mambo muhimu ambayo mwanamke anaweza
kufanya kupunguza tisho la kuugua Saratani ya Matiti , hasa baada ya
kupitisha miaka yake ya kuzaa ni pamoja na kufanya mazoezi , kula vizuri
na kupunguza ulevi.
Kupunguza unene ni njia moja wapo ya kupunguza tisho la kupata Saratani
baada ya kupitisha miaka ya kuzaa na kuangalia vipimo vya sketi za
wanawake kuwahamasisha wanawake.
0 comments:
Post a Comment