MSANII
wa siku nyingi katika tansia ya filamu Bongo, Salama Salmin ‘Sandra’
amefunguka kuwa tangu ameanza kujihusisha na mambo ya sanaa hajawahi
kuwa na bwana ndani ya klabu ya Bongo Movies na wala hajawahi kutoa
rushwa ya ngono kwa ‘dairekta’ kama ilivyo kwa wengine.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Sandra alisema kuna baadhi ya
wasanii wanafikiri kuwa na mwanaume ndani ya Klabu ya Bongo Movie ndiyo
kutimiza ndoto zao kumbe ni kujidharaulisha tu.
“Sina
bwana wala sijawahi kutoa rushwa ya ngono kwa ‘dairekta’ na sifikirii
kufanya hivyo kamwe, maana ni kujishushia heshima yangu wakati mimi ni
mke wa mtu na wala siwezi kunadi mwili wangu,” alisema Sandra.
0 comments:
Post a Comment