Jopo maalum la watalaamu wa masuala ya tabia nchi la Umoja wa Mataifa limechapisha ripoti yake ya karibuni inayoonya kuwa muda unazidi kuyoyoma wa kupunguza kiwango cha joto duniani kufikia nyuzijoto mbili.
RIPOTI hiyo inasema kiwango cha sasa cha gesi ya kaboni ni tishio la kutokea janga katika siku za usoni.
Watalaamu hao wamesema serikali zinaweza kudhibiti ongezeko la joto duniani, lakini zinastahili kuchukua hatua sasa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema ripoti hiyo imetolewa wakati ulimwengu ukiwa haujajiandaa vilivyo kwa athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi, hasa nchi maskini na zinazokabiliwa na kitisho kikubwa ambazo huchangia kiasi kidogo kwa tatizo hili.
Ripoti hiyo imeonya kuhusu matatizo ya usalama wa chakula, kuangamia familia tofauti za wanyama na uharibifu wa mazingira ambayo yana tegemewa na mwanadamu.
0 comments:
Post a Comment