Watengenezaji wa magari aina ya Toyota nchini Japan wameeleza kuwa kumekua na ongezeko kubwa la mauzo ya magari hayo nchini china mwezi uliopita.
KAMPUNI hiyo ya Toyota ambayo imeingia ubia na makampuni makubwa ya china kama FAW GROUP pamoja na Guanzhou Automobile wamepata ongezeko la asilimia 27.1 mwezi oktoba ndani ya mwaka mmoja.
Mauzo hayo ya kampuni ya Toyota yame ongezeka kwa asilimia 13 kufikia mwezi wa kumi tofauti na mwaka 2013.
Kampuni hio kubwa ya utengenezaji wa magari imesema kuwa inatarajia kuuza magari milioni moja kwa mara ya kwanza mwaka huu 2014.
Mwaka jana hali ilikua tofauti ambapo Toyota ili uza magari 917500.
Hata hivyo ndani ya mwezi septemba mauzo yalipanda kwa asilimia 2.5 toka mwaka mmoja upite ambalo ni ongezeko dogo ndani ya miezi 19.
chama cha uzalishaji wa magari cha china CAAM Kina tabiri kuwa soko hilo litakua kwa asilimia 8.3 mwaka huu toka lipande kwa asilimia 14 mwaka jana.
Ikumbukwe pia Toyota wameweza kuongoza kwa vichwa vya habari vikiashiria matatizo ya magari 1750000 duniani kote juu ya ubovu wa mfumo wa mafuta wa magari hayo.
0 comments:
Post a Comment