Wednesday, September 3, 2014

HUWEZI AMINI, HUU NDIO UTAJIRI WA MAJUMBA YA KIFAHARI YA MCHEZAJI MRISHO NGASA, JIONEE MWENYEWE HAPA!

SASA ni miaka nane tangu aanze kucheza soka ya ushindani mwaka 2005 katika klabu ya Kagera 
Sugar ya Bukoba, lakini kwa namna alivyopanga vyema karata zake, Mrisho Khalfan Ngasasa anafurahia maisha ya mpira. Huwezi kumuita tajiri, lakini huwezi kuacha kumpa heshima miongoni mwa wachezaji wa kizazi chake, kwamba amewaacha mbali. 
Amecheza klabu nne katika Ligi Kuu tu, baada ya Kagera Sugar ni Yanga SC mwaka 2007 hadi 2010, Azam 2010 hadi 2012 na sasa amerejea Jangwani.
Ngassa akiwa na bibi na babu
Ngassa katika kaburi la shangazi yake
Ngassa na watoto wake.

“Katika gari zangu nane, gari tatu za biashara, 
mbili ni zangu mwenyewe za kutumia, moja ya 
shughuli za nyumbani wakati wote na mbili 
nimewagawia baba na mama kila mmoja na yake,”.
 Ngassa anasema baada ya kustaafu soka atajitanua
 zaidi kibiashara, kwani ndoto zake ni kutoka kuwa
 mwanasoka nyota hadi mfanyabishara mkubwa.   
 “Mimi ujuzi wangu ni soka. Baada ya hapa 
sitegemei kurudi shule kusomea chochote, 
nitafanya biashara. Nimekwishaanza 
kufanya utafiti wa biashara za kufanya,”.
 “Sitarajii kufanya biashara za kibishoo za 
kuigana igana sijui kufungua saluni au maduka
 ya nguo. Mimi nitafanya biashara kubwa na 
siku moja nitatatambulika kama mwanasoka 
wa zamani na mfanyabiashara mkubwa, 
tayari nina mashamba kama matatu, hapo
 nazungumzia kilimo, ambacho kwa sasa ni  
biashara kubwa,”anasema Ngassa.

Nyumba nyingine ya Mwanza
Moja ya gari za kutembelea za Ngassa ikiwa katika nyumba ya Dar es Salaam, Yombo.
Nyumba ya Bwiru ni marumaru tupu
Ngassa akiwa na watoto

Pamoja na kufanikiwa uwanjani na katika maisha katika upande 
wa kuwekeza, Ngassa hakuwa mvivu pia katika ujenzi wa 
familia, hadi sasa akiwa na umri wa miaka 25, ana watoto wawili,
 ambao ni Farida (5) na Farkhiya (3). Ngassa anawajali sana 
watoto wake na wote anaishi nao mwenyewe, ingawa ametengana
 na mama yao, kwa sasa akihakikisha wanapata malezi bora,
 ili wakue vizuri. Baada ya kumaliza kuitumikia timu ya soka ya
 taifa ya Tanzania, Stars katika mechi za kuwania kucheza 
Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), 
Ngassa ameenda likizo Mwanza tangu Jumatatu na
 anatarajiwa kuripoti kazini, Yanga SC Jumapili. Ngassa
 alijaribu sana kuibeba Stars akitoa krosi ya bao lililofungwa
 na Amri Kiemba na kukaribia kufunga mara mbili, lakini 
Tanzania ikalala 3-1 mbele ya Uganda mjini Kampala na 
kutolewa CHAN.  Amekubali matokeo na kwenda kusalimu wazazi, 
ndugu, jamaa na marafiki baada ya mwaka mzima wa kuwa
 kazini Dar es Salaam. Akiwa huko, Ngassa alitembelea bibi 
na babu zake, ndugu, jamaa na marafiki hadi vijijini na pia 
kuzuru kaburi la shangazi yake aliyefariki mwezi mmoja 
uliopita yeye akiwa ametingwa na majukumu ya kitaifa. 

Gari lingine la Ngassa 

Ngassa aliwatemebelea watoto na kuwazawadia mipira ili 
wacheze soka, akiwahamasisha kujibidiisha na wao watakuwa 
kama yeye siku moja, kwani hata yeye aliaanzia kama wao.
 Mjini Mwanza, Ngassa ni kama mfalme, anapendwa mno
 kutokana na mfumo wake wa maisha, siku zote ni kijana 
mwenye nidhamu, adabu na utii- na asiyesahau asili yake. 
Likizo yake hii ya sasa amekwenda hadi msikitini kufuturu na 
waumini wenzake wa dini ya Kiislamu na kufanya ibada ya
 sadaka. Anatakiwa dua njema tu na watoto hadi wazee, wake 
kwa waume na hakuna ajabu akiendelea kuwa mwanaoska
 nyota Tanzania.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI