WANARIADHA toka nchini Kenya Wilson Kipsang pamoja na Mary keitany wameibuka kidedea katika mashindano ya mbio za New York Marathoni zilizo fanyika katika jiji la New York huku kukiwa na hali ya baridi pamoja na mawingu.
Washiriki kutoka kenya Wilson Kipsang pamoja na Mary Keitany waliweza kumaliza mbio hizo katika nafasi za kwanza na kuweza kuwashinda wapinzani wao kwa ushindi mwembamba kuelekea mwisho wa mbio hizo.
Kipsang aliweza kuwatangulia washiriki wenzake kama Lelisa Desisa ambaye alimtangulia mshiriki kutoka Ethiopia kwa sekunde 11, pamoja na mshiriki mwingine Gebre Gebremariam alie maliza katika nafasi ya tatu.
Kipsang amesema kua alihifadhi pumzi za mwisho ili kuibuka kidedea kwa kujipatia kitita cha EURO 80000 na kuwa mshindi wa mbio za New York marathon kwa mwaka 2013-2014.
Kwa upande wa wanawake Mary Keitany aliibuka mshindi kwa mara ya kwanza tangu amalize katika nafasi ya nne kwenye mashindano ya Olympiki ya london akiwa ni mjamzito.
Katika hali ya baridi na mawingu kwa wingi washiriki wote waliweza kimbia kuulekea kilele cha mbio izo kwa umbali wa mita 26.2 kutokea mji mkubwa wa marekani wa new york.
0 comments:
Post a Comment