Monday, November 3, 2014

WATU 14 WAMERIPOTIWA KUUAWA NCHINI CONGO

Machafuko yameendelea kushuhudiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo takriban watu 14 wanaripotiwa kuuawa na waaasi wa ADF-NALU wa Uganda.
KWA mujibu wa Gazeti la Le Figaro la Ufaransa linaripoti kwamba,  mji wa Beni ulioko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo jana ulishuhudiwa vitendo vya utumiaji mabavu vilivyofanywa na waasi wa ADF-NALU wa Uganda.
Maelfu ya raia wamelazimika kuyakimbia makazi yao wakihofia usalama wa maisha yao kutokana na kuibuka wimbi jipya na mashambulio ya waasi hao katika mji wa Beni.
Wakati huo huo, ripoti zinasema kuwa maandamano makubwa yamefanywa katika mji wa Beni, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, baada ya mauaji ya karibuni yaliyofanywa na makundi ya wanamgambo.
Mashambulio ya watu wenye silaha katika maeneo ya mashariki mwa Congo yameua watu wasiopungua 110 tangu mwezi uliopita hadi sasa.
Maafisa wa serikali ya Congo hadi sasa hawaja toa taarifa yoyote kuhusu kuuliwa watu hao.
Waasi wa Uganda  wa ADF-NALU wanatuhumiwa kuhusika na mashambulizi ya mara kwa mara huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI