Friday, June 6, 2014

MAPENZI YA DHATI YAONESHWA KWA WHITNEY HOUSTON, BAADA YA SHABIKI MMOJA KUNUNUA NYUMBA ALIYOKUWA AKIISHI

fan
Mapenzi yaliyopitiliza ya shabiki wa muziki wa Marehemu Whitney Houston yamemfanya kununua nyumba ya mwanamuziki huyo na kuahidi kuitunza kwa ajili yake.
Nyumba hiyo ya Whitney iliyopo katika mji wa Mendham huko New Jersey imeuzwa kwa takribani dola milioni 1.5 kwa Matthew Krauthamer, ambaye ni shabiki wake na amedai kuwa hataki kuibadilisha nyumba hiyo yenye ukubwa wa hekari tano.
Whitney-Houston
Nyumba hiyo ambayo Whitney hakuishi kwa muda wa miaka mitano kabla ya kifo chake kilichohusishwa na dawa za kulevya kilichotokea February mwaka 2012 ina jumla ya vyumba vitano, garage sita za magari.
Wakati mwanamuziki huyo ananunua nyumba hiyo aliiongezea studio ya kurekodi muziki, chumba cha michezo, chumba cha burudani, uwanja wa mchezo wa Tennis na nyumba ya bwawa la kuogelea na mmiliki huyo mpya amesema anataka kuifanya nyumba hiyo ya kiburudani zaidi.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI