Friday, June 6, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA KIWANDA CHA COCACOLA MWANZA KATIKA MAADHIMISHO YA KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Mwanza na wa Kiwada cha Cocacola, wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana Juni 5, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa ubora wa Mazingira na Usalama Kazini, Peter Simon, kuhusu jinsi wanavyo tunza mazingira kwa kutotupa maji machafu ambayo hutengenezwa na kuwa masafi na kutumika upya kwa baadhi ya shughuli za kiwandani hapo kama kumwagia bustani, kuoshea magari na n.k, wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana Juni 5, 2014.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Cocacola Mwanza, Christopher Gachuma, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kuzungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho, wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana Juni 5, 2014.
Picha ya Pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni hiyo.
Makamu akiagana na wafanyakazi wa kiwanda hicho baada ya ziara yake.
Picha na OMR

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI