Saturday, May 17, 2014

DIAMOND PLATNUMZ NDANI YA BET AWARDS

Msanii toka Tanzania Diamond Platnumz ameipa tena heshima kubwa bendera ya Tanzania kwa kuwa kwenye kipengele cha msanii bora wa Kimataifa [Best International Act ], Hii ni hatua kubwa kwa Diamond baada ya siku chache tu nyuma alitangazwa kwenye tuzo za MTV Base (Mama Awards).
Diamond Platnumz kwenye kipengele hichi cha tuzo kubwa za Television kubwa ya burudani Marekani ya BET yupo kama Best International Act Africa na anawania tuzo hii na wasanii Davido kutoka Nigeria, Mafikizolo kutoka South Africa, Tiwa Savage kutoka Nigeria, Toofan na Sarkodie kutoka Ghana.
BET imetumia twitter kutoa hii taarifa kama kuthibitisha uchaguzi wa Diamond na kuumpa hongera kama msanii pekee Africa Mashariki.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI