Mti wa mpera ni miongoni mwa miti ya matunda ambayo
inafahamika vizuri katika jamii ya watu wengi hapa nchini. Mti huu hutoa matunda yanayofahamika kama
mapera na asili ya mti huu ni Amerika ya
Kati na Kusini licha ya kuwa kwa siku hizi mti huu unapatikana sehemu mbalimbali hapa
duniani.
Mmea huu kama ilivyo kwa mimea mingine ya matunda, unastawi zaidi katika hali ya hewa ya kitropiki. Hapa nchini Tanzania mmea huu unasadikika uliletwa na wakoloni waliotoka mashariki ya mbali waliokuja Afrika kwa madhumuni mbalimbali ikiwemo suala la kueneza dini ya Kiislamu na Kikrosto.
Wataalam wa tiba asili wanauzungumzia mti huu kama
tiba nzuri inayoweza kutibu magonjwa mbalimbali yakiwemo yale ambayo ni tishio kwa kizazi cha sasa kama figo.
Tabibu wa tiba asili hapa nchini Dk Abdallah Mandai
kutoka Mandai Herbalist Clinic anasema majani ya mti huo yanasaidia sana
kuondoa kichefuchefu, lakini pia yanapopondwa na yakitumiwa vizuri yanazuia
ugonjwa wa kiharusi.
“Majani
ya mpera yanaponya vidonda vya tumbo na pia yanavirutubisho vingi ambavyo
husaidia kuimarisha fizi na kuongeza vitamin B na A mwilini”
anaeleza Dk Mandai.
Aidha, anaendelea kusema kwamba majani ya mpera yenye
uzito wa kilo moja yanapopondwa na kisha mgonjwa akanywa lita moja yana saidia
sana kukinga seli za mwili dhidi ya magonjwa.
Dawa hiyo pia hutibu ugonjwa wa malaria , aidha
anasema mgonjwa atumie tiba hiyo kati ya siku 14 hadi mwezi mmoja
kulingana na ukubwa wa tatizo la mgonjwa
husika.
Hali kadhalika anasema kwamba juisi ya mapera
husaidia sana kutibu mgolo au bawasila, figo na hata kuondoa mafuta katika
moyo.
Anabainisha kuwa,
mizizi ya mpera ikichemshwa inasaidia sana kwa akinamama wenye matatizo
ya hedhi au wanaotoa maji yenye harufu mbaya kutoka sehemu zao za siri.
Matunda yanayotokana na mti wa mpera yaani mapera ambayo pia watu wengi wanapenda kula |
Sambamba na hayo, Dk Mandai anaeleza kuwa, majani mateke
yanapofungwa shingoni kwa mwenye tezi yanauwezo wa kuponyesha tatizo hilo pia
na mwenye jipu akifunga sehemu husika hulifanya jipu kuiva haraka mno.
Watoto wadogo wenye matatizo ya kutopata choo zaidi
ya siku mbili, Dk Mandai anasema wakinyweshwa maji ya majani hayo baada ya
kuchemshwa wanapona kabisa tatizo hilo, lakini pia maua ya mpera yanasaidia
katika kutibu tatizo la manjano na hata homa kali.
Mizizi na matunda hali kadhlika husaidia kuongeza vitamin B na C, ambapo mtumiaji
atapaswa kuchemsha majani yenye ujazo wa gramu moja kisha anywe kikombe kimoja
mara tatu kwa siku.
Hata hivyo, Dk Mandai anaonya kuwa endapo
unasumbuliwa na maradhi hayo ambayo yameelezwa kutibika kwa mti huo wa mpera ni
vizuri ukafanya utaratibu wa kuonana naye kwanza kabla ya kuanza tiba hiyo kwa
ajili ya maelekezo na ushauri wa kitabibu zaidi. Dk Mandai anpatikana Ukonga,
Mongolandege kwenye kituo chake kiitwacho Mandai Herbalist Clinic.
0 comments:
Post a Comment