Leo Jan 9 chama cha ACT- Wazalendo kilifanya mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na kumpongeza Mbwana Samatta pamoja na ishu ya Bomoabomoa inayoendelea Dar es Salaam.
Akizungumza Naibu katibu mkuu Msafiri Mtemelwa alisema..’ACT Wazalendo katika misingi yetu tunatanguliwa na kauli mbiu ya utu, uzalendo na uadilifu ambayo kila mmoja akiitekeleza ipasavyo itakuwa chachu ya kuondoa mikwamo kama inayoendelea sasa katika kadhia hii ya bomoabomoa’– Msafiri Mtemelwa
‘Tunaamini mpaka kufikia hatua ya wanawanchi kubomolewa nyumba zao kuna watu walikosa uzalendo kwa Taifa lao kwa kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo na hawa ni watendaji kuanzia ngazi ya mtaa mpaka ngazi ya Taifa’ – Msafiri Mtemelwa
‘Mwisho wa zoezi la bomoa bomoa utakapokamilika ndiyo uwe mwanzo wa kuwawajibisha wale wote waliozembea kutekeleza majukumu yao hata kufukia wananchi kujenga katika maeneo yasiyoruhusiwa.
Tunaungana na Watanzania wengine kumpongeza shujaa wetu Mbwana Samata kwa kufanikiwa kuwa mchezaji bora wa Africa kwa wachezaji wanaocheza soka la ndani (CHAN)’ – Msafiri Mtemelwa
‘Serikali inapaswa kujikita katika kuhakikisha mifumo ya michezo mbalimbali inaboreshwa kwa kuanza na kurudiasha maeneo ya wazi iliyokuwa ikitumiwa na vijana wetu kwa ajili ya michezo mbalimbali.
ACT Wazalendo tumepokea wanachama wapya 10 kutoka vyama mbalimbali wakiwemo Museven Kusaga (TLP), Neema Musukwa (NCCR) Getruda Pwilla( katibu mkuu wanawake NCCR) Frida Bohella (NCCR) Esta Kapama( katibu mwenezi TLP) Jeremea Shelukindo( Katibu mkuu TLP)’ – Msafiri Mtemelwa
0 comments:
Post a Comment