NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Saturday, January 31, 2015

NAZIZI AFANYA MAAJABU: AJIKONDESHA NA KUWA MREMBO WA HAJA UKIMUONA HUTOAMINI..MCHEKI HAPA!!!

MWANAMUZIKI Nazizi Kutoka Kenya Ameshangazi Wengi Baada ya Kufanikiwa kupunguza mwili wake kwa kiasi cha wengi kuto amini kama ni yeye, Mwanamuziki huyo kabla ya hapo alivyo sasa alikuwa ni Bonge nyanya yaani mnene kupindukia, lakini siku za karibuni mwanamuziki huyo ameingia Gym na Kufanikiwa kupunguza mwili wake kwa kiasi kikubwa sana,
Artist and music sensation Nazizi has made all our jaws drop to the floor, as we get busy picking our jaws from the floor and getting reanimated from our shock, lets share the shock with you too, lets see if you handle the jaw-drop. Damn this is like an RKO from nowhere! She has literally stunned us.
 Now look at That!

AGNESS MASOGANGE AKANA KUTOKA NA KING LAWRENC, SAA YA MKONONI YALETA UTATA *PICHA*

 
BAADA ya Mrembo Agness Masogange Aishie Njia South Afrika kupost kwenye instagram Picha ya Mkono wa Mwanaume wenye saa nyeusi, watu na page mbali mbali walianza kumshambulia na kusema mkono huo ni wa King Lawrenc na wengine kuandika kuwa ni project mpya, Agness Masogane Amejitokeza na kuandika haya instagram:
"Mkono huo ni wa Boyfriend wangu na sio wa huyo mnaemsema na wala simjui hata sijawahi kumuona..muwe mnachunguza vitu kwanza sio kukurupuka tu na kuongea ongea ovyo"

ISHUHUDIE SAFARI YA MWISHO YA BABA YAO P SQUARE ALIYEFARIKI 2014 NA KUZIKWA 2015 *PICHAZ*

Psq VII
Mzee Moses Okoye, baba mzazi wa mastaa wa muziki kutoka Nigeria, Peter na Paul Okoye wa kundia la ‘P Square’ alifariki November 25 2014 baada ya kuanguka kwenye ngazi ndani ya nyumba.

Taarifa za wanafamilia zilisema mzee huyo alifanyiwa upasuaji wa goti siku za nyuma na hali yake ilianza kuwa sawa kabla ya kufariki ambapo leo January 30, 2015 ndio mzee huyu amezikwa, ikiwa ni miaka miwili imepita toka kufariki kwa mama yao.
Hizi ni picha za safari ya mwisho ya Mzee Moses Okoye, baba wa mastaa mzazi wa P Square na Jude ‘Engees’ Okoye.
Ps
Psq II
PSq Iv
Psq IX
.
Peter na Paul Okoye.
Psq VI
PSQ vkas
.
Peter na kaka yake, Jude Okoye.
pSQ
P S 1
PS 2
PS 3
Kulikua na ulinzi pia
Kulikua na ulinzi pia
ps 5
ps 6

ICHEKI BRAND NEW VIDEO YA DAVIDO FT. UHURU & DJ BUCKZ - ‘THE SOUND’

.
STAA wa Nigeria David Adedeji Adeleke aka Davido ana hit nyingi tunazozijua SkelewuAye na ile Tchelete aliyofanya na wakali wa Mafikizolo, zote ni kali!
Davido, amekuletea video ya single mpya inayoitwa ‘The Sound’ akiwa amewashirikisha Dj Buckz pamoja na kundi la Uhuru kutoka Afrika Kusini. Hebu Bonyeza play kuenjoy#TheSound

BABA MZAZI AJITOA UHAI BAADA YA KUONA PICHA CHAFU ZA MWANAE…ZITAZAME HAPA!!!


Loredana Chivu ni mwanamitindo nchini Romania.

Baba mmoja amejiua baada ya kuona picha za uchi zamwanawe wa kike katika jarida la Playboy nchini Romania.
Loredana Chivu alirarua ukurasa uliokuwa na picha yake akiwa 'amepos' katika jarida hilo la Playboy na punde babake alipogundua kuhusu picha hizo, alizongwa na mawazo na hata kumkana mwanawe.
Kwa mujibu wa mtandao wa Mirror, msichana huyo mwenye umbo la kuvutia alisema,
'' babangu aliacha kuongea na mimi na kuonekana mwenye hasira sana''.
"alipogundua kuwa picha hizo zilikua zangu, alijitenga sana na kujaribu kunitenga na mimi''.
Nilidhani labda angesahau na sikudhani hata siku moja angejitoa uhai.
 Loredana Chivu anasema anajuta sana kwani babake hakuwahi kuongea naye baada ya kupata picha zake.
Mwanamitindo huyo Loredana Chivu mwenye mamia ya picha akiwa nusu uchi kwenye akaunti yake ya Instagram, alikuwa na uhusiano wa karibu sana na babake lakini alisema yote hayo yalibadilika baada ya babake kuona picha zake akiwa nusu uchi.
Alipokwenda kumtembelea babake miezi michache baadaye, baada ya kuamua kwamba kimya kilikuwa kimeendelea kwa muda mrefu sana, alishtuka sana kumpata babake akiwa amejitoa uhai
"nilipata akiwa na kamba shingoni akiwa ananing'inia chumbani''.
Loredana,anayeishi nchini Romania, anasema kuwa tangu kifo cha babake, amekuwa akiwaza na kuwazua kwamba aliamua kujiua kwa sababu ya mgogoro kati yetu na hasa kuhusu picha zangu zilizoziona kwenye jarida la Playboy.
''Najuta sana kwamba hakuwahi kupata muda wa kuzungumza na babangu kuhusu yaliyotokea''.
''Hakuwacha ujumbe wowote kabla ya kujitoa uhai, siku zote tulikuwa na uhusiano mzuri lakini yote yalibadilika baada ya baba kuona picha zangu nikiwa uchi. Bado inaniuma sana na singemtakia mtu yeyote kupatwa na kama yaliyonikuta''.

MEYA WA MORO, DEREVA NA MWANDISHI WAKIMBIZWA MUHIMBILI KWA MATIBABU

MSTAHIKI Meya wa halmashauri ya manispaa  ya Morogoro, Amir Nondo (45), Dereva  Mwambala Ally (55),  na Mwandishi wa habari ambaye ni mpiga picha wa Televisheni, Hussein Nuha (28) ,wamehamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  kwa uchunguzi wa kina na kupatiwa matibabu zaidi.
Hayo yamesemwa leo na Mganga mkuu wa mkoawa Morogoro , Godfrey Mtei , akielezea hali ya majeruhi hao ambao waliokuwa wamelezwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya  kujeruhiwa wakati gari lao lilipogongwa na basi la abiria lenye namba za usajili T 831 CEH, aina ya Scania mali ya kampuni ya Happy Africa likitokea mkoani Njombe.
Tukio hilo lilitokea Januari 30, mwaka huu majira ya saa 9: 30 alasiri , eneo la Msamvu Mzambarauni darajani katika barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaam, ambapo basi hilo lilikuwa likotokea mkoani Njombe.
Hata hivyo alisema, mwandishi mmoja, Anitha Chali (30)  ambaye amelezwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro anaendelea vizuri na wakati wowote anaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani.

UWANJA WA WAPENDANAO: MFANYIE MAMBO HAYA MPENZI WAKO WA KIKE AKUZIDISHIE RAHA DUNIANI! (+18 YRS)


MAMBO vipi ndugu zangu? Ni furaha yangu kwa mara nyingine tena kukutana nanyi wapendwa wasomaji wa blog hii. Tumshukuru Muumba wetu kwa kutujaalia uhai na afya njema, lakini zaidi ya hapo tumshukuru pia kwa kutuumbia kitu mapenzi au siyo jamani?
Siku zote hatutaacha kuzungumza juu ya mapenzi kwani ni ukweli usiopingika kwamba mapenzi ndiyo maisha yetu. 
Tunafanya kazi usiku na mchana, tunahangaika huku na huko, lakini mwisho wa siku tunafikiria jinsi gani tutapata kuboresha na kufurahia maisha na wapenzi wetu. 
Tunafikiria pia ni jinsi gani tunaweza tukapata utulivu na amani katika maisha ya kimapenzi na wapenzi wetu, waume zetu au wake zetu katika siku zote za maisha yetu.
Ndugu zangu, Mungu ametuwekea mapenzi ili tupate raha na amani katika maisha yetu.
Kwa maana hiyo, wale wanaoyachezea na kuyavuruga mapenzi kwa makusudi kwa kuumiza hisia za wenzao kisha kuwasababishia vilio si watu wa kupendeza mbele ya macho ya wale wanaojua hasa nini maana ya mapenzi. 
Wanawake ni watu wa kuheshimika na kupewa furaha wanayohitaji.
Unapompata mwanamke anayekupenda na kukuheshimu, huna sababu ya kumfanya ajute kuwa na wewe.
MPENDE NA MTHAMINI!
Yawapasa wanaume mfahamu kuwa, wanawake ni zawadi kwenu, pumziko na tulizo la mioyo yenu. Wanawake ndiyo raha na amani kubwa ya maisha yenu.
Kosa kubwa mnalofanya wanaume ni kuutumia vibaya mfumo dume hasa katika suala nyeti kama mapenzi.  Mapenzi si ubabe, mapenzi ni upole na ukarimu. 
 Pamoja na kwamba mmebarikiwa kwa kupewa nafasi ya kuwa kichwa katika nyumba lakini linapokuja suala la kurekebisha tofauti zinazojitokeza katika uhusiano wenu, si vyema kutumia njia za kibabe.
Niwaambie kitu, wanawake ni wa hisia zaidi na waliobarikiwa kuwa na upendo wa hali ya juu na ndiyo maana wakapewa dhamana ya kubeba mtoto tumboni kwa miezi tisa na pia kumnyonyesha na kumlea kwa miaka kadhaa, wewe mwanaume ungeweza?
Nasema ni watu wa hisia kwa sababu, hivi uliwahi kufikiri ni kwa nini wanawake huridhika na kujisikia poa kweli wanapopewa zawadi kama ya maua na kadi zenye ujumbe wa mapenzi ukilinganisha na wanaume? 
Unafikiri ni kwa nini wana machozi ya haraka wanapotendwa? Au unafikiri ni kwa nini wanapenda kutumiwa ‘love sms’ zaidi kuliko kupigiwa simu? Jiulize.
Mimi nawaona wanawake kama watu wa kuheshimiwa na kupendwa kwa dhati.  Mkumbuke wanawake ndiyo mama zetu, walezi wetu na ndiyo nyumba zetu. Jaribuni pia kujicontroo na huo mnaouita ukijogoo kwamba eti ninyi ni watu msioridhika na mpenzi mmoja. 
Jaribuni kufanya kila mnaloweza kuifuta ile dhana ya kwamba wanaume hawaaminiki hata kidogo. Ridhika na mpenzi uliyenaye, heshimu hisia zake na thamini mapenzi yake kwako na mpe ile kitu roho inapenda!

MMMH…JOJO KIDOTI + MILLARD AYO KUNAKO KEKI YAKAIBUKA MAMBO MAZITO! FUATILIA HAPA!

‘Mtu wa Nguvu’ Millard Ayo na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ wakifurahia jambo kwenye ‘bethidei’ yake. Stori: Hamida Hassan na Musa Mateja/Ijumaa 
Keki iliyoandaliwa na Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kwa ajili ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ‘bethidei’ ya Millard Ayo ‘Mtu wa Nguvu’ imeibua mambo kwa mashabiki wao. 
Ishu hiyo ilijiri Januari 26, mwaka huu ambapo Jokate alidaiwa kuangusha pati nyumbani kwa jamaa huyo maeneo ya Ubungo-Msewe jijini Dar. 
Kwenye pati hiyo, Millard ambaye ni mtangazaji mkali wa Vipindi vya Amplifaya na Top 20 vya Clouds FM, alidaiwa kumwalika Jokate ambaye mashabiki wao walimpa jina la Special Girl (msichana maalum). 
Pia katika pati hiyo, ‘ubuyu’ ulienea kwamba Jokate ndiye aliyekaangariza madikodiko na kupakua nyumbani kwa jamaa huyo kisha akamwandalia bonge la keki

CHEKI TOTO LA BECKHAM NDANI YA CLUB YA ARSENAL *PICHAZ*

brooklyn
PAMOJA na kua mtoto wa nyota wa zamani wa Manchester United, David Beckham kijana Brooklyn Beckham yuko njiani kuanza maisha kama mchezaji wa kikosi cha kwanza cha wapinzani wakubwa wa baba yake Arsenal ‘The Gunners’.
Kijana huyu mwenye umri wa miaka 15 anafahamika kama shabiki wa Arsenal kwa muda mrefu na alisaini kuichezea timu hiyo mwaka jana akianzia kwenye kikosi cha wachezaji wenye umri chini ya miaka 16.
Hivi karibuni Brooklyn alipakia picha kwenye mtandao wa Instagram akiwa na wachezaji wenzie akiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vya uwanja wa mazoezi wa Arsenal.
Akiwa amekaa kwenye chumba hicho na wachezaji wenzie Beckham alionekana akiwa mwenye furaha kuwa na wachezaji wenzie na dalili zote zinaonyesha kuwa huenda atafuata nyayo za baba yake ambaye ni moja kati ya wachezaji waliopata mafanikio makubwa kwenye mchezo wa soka.
Brooklyn Beckham akiwa na wachezaji wenzie wa kikosi cha wachezaji wenye umri chini ya miaka 16 wa Arsenal.
Brooklyn Beckham akiwa na wachezaji wenzie wa kikosi cha wachezaji wenye umri chini ya miaka 16 wa Arsenal.
Brooklyn huko nyuma amewahi kufanya majaribio na timu za ChelseaManchester United, Fulham na Queens Park Rangers na alifanya majaribio na Arsenal ambao wamemsainisha mkataba tangu mwezi mwezi novemba mwaka jana.
Cha kushangaza kuhusu familia ya Beckham ni kwamba watto wake wote wa kiume ni mashabiki wa Arsenal na hakuna yoyote aliyechagua kufuata nyayo za baba yao ambaye ni shabiki na gwiji wa Manchester United.
Beckham akiwa na Brooklyn wakitoka kuangalia mechi uwanjani huko England .
Beckham akiwa na Brooklyn wakitoka kuangalia mechi uwanjani huko England.
Sio kushabikia tu bali watoto hawa wamekwenda mpaka hatua ya kujiunga na timu hiyo ambapo Cruz mwenye umri wa miaka 9 anachezea kikosi cha vijana wa Arsenal chini ya miaka 10 na Romeo mwenye umri wa miaka 12 anachezea kikosi cha The Gunners kwa watoto chini ya miaka 13 na kaka yao Brooklyn anachezea kikosi cha vijana chini ya miaka 16.

YANGA YATUMIA NDEGE KUSAJILI WINGA WA AZAM

Wachezaji wa Yanga katika moja ya mazoezi.
Picha|Maktaba  na Khatimu Naheka.
YANGA na Azam zilikuwa zikiwania saini ya mchezaji wa Kimondo FC, Geofrey Mwasuya kwa ajili ya msimu ujao, lakini vijana hao wa Jangwani wamecheza akili sana na kuiacha Azam na utajiri wake kwenye mataa.
Azam ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufanya mazungumzo na mchezaji huyo, lakini Yanga ilipostukia ikamtumia tiketi ya Ndege kutoka Mbeya kuja Dar es Salaam.
Mchezaji aliposikia anapanda ndege kwa mara ya kwanza akapagawa na kuja Dar es Salaam haraka bila kujiuliza akamwaga wino Yanga huku Azam wakibaki wanashangaa.
Winga huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu na habari zinasema kuwa Yanga walimsajili Mwasuya wakimtuma nahodha wao wa zamani Shadrack Nsajigwa ambaye pia ni kocha wa kikosi cha timu ya vijana ya timu hiyo alipewa kazi maalum ya kukamilisha usajili huo huku Azam wakimpa kazi hiyo meneja wao Jemedari Said.
Kiongozi huyo alisema kufanikiwa kwa Yanga katika usajili huo kulitokana na kutumia ujanja mdogo uliomchanganya winga huyo ambapo walimtumia tiketi ya ndege kutua jijini Dar es Salaam kukamilisha usajili huo jambo lililomchanganya mchezaji huyo.
“Hakuwahi kupanda ndege sasa alipoambiwa kwamba Yanga wamemtumia tiketi akachanganyikiwa kabisa, huku akatudanganya kwamba anauguliwa kumbe amekuja Dar es Salaam kusaini mkataba wa miaka mitatu hapo ndipo Azam walipopigwa bao,”alisema mmoja wa viongozi wa Kimondo.
Msemaji wa Kimondo Chris Kashilika alipoulizwa alikiri Mwasuya kusajiliwa na Yanga ingawa alisema klabu hiyo bado haijakamilisha taratibu zake.
“Taarifa hizo tunazo kwamba Mwasuya amesajiliwa Yanga ingawa mwenyewe alikuwa ametuficha lakini tunachoweza kusema ni kwamba bado Yanga hawana uhalali wa usajili huo kutokana na kuwa mchezaji huyo bado ana mkataba na Kimondo utakaomalizika mwakani na hawajakamilisha taratibu.”
Habari zinasema kwamba Yanga walikuwa hawana mpango sana na mchezaji huyo lakini baada ya kuona Azam wanamfuatilia kwa karibu na wao wakaamua kuingia kwenye kinyang’anyiro na kubaini kwamba mchezaji huyo ni mdogo na anaweza kuibeba Yanga miaka mingi.
#Mwananspoti.

'WASHABIKI MSIPENDE KUDANDIA TRENI KWA MBELE MTAGONGWA' - SHILOLE AFUNGUKA

KUPITIA Kipindi cha TV cha Friday Night Jana usiku Kituo cha EAT Shilole Amefungukia mashabiki wake kuwa Wasipende kudandia Treni kwa mbele Mtagongwa, kawaambieni hivyo mashabiki wake kwakuwa mmeishupalia ishu ya kumpiga vibao 'mmewe' wakati hamjui kilichotokea.

TANZANIA KUANZISHA DUKA LA KUDUMU LA BIDHAA ZENYE ASILI YA KITANZANIA NCHINI OMAN *PICHAZ*

Balozi wa Tanzania Nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh kulia akipata Maelezo kutoka kwa Maafisa wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) Sabra Shehe na Mussa Abdullah  wakati Balozi huyo alipofanya ziara ya kuwatembelea Watanzania hao wanaoshiriki, Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea katika Mji wa Mascut nchini humo.
Wasanii wa Fani ya Uchoraji Tanzania Fred Halla na Salum Ameir Muchi wakimkabidhi Ua kama zawadi Balozi wa Tanzania Nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh kulia wakati Balozi huyo alipofanya ziara ya kuwatembelea Watanzania hao wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea katika Mji wa Mascut.
Balozi wa Tanzania Nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akisalimiana na Mbunifu wa Mavazi (Designer) Farida Amiri wakati Balozi huyo alipofanya ziara ya kuwatembelea Watanzania hao wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea katika Mji wa Mascut nchini humo.
Balozi wa Tanzania Nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh kulia akitoa nasaha zake kwa Wasanii wa Fani ya Uchongaji Tanzania.Kutoka kushoto Iddi Amana, Mwandale Mwanyikwa(Big Mama)na Abdulrahman Abdulla mara baada ya Balozi huyo kuwatembelea Watanzania hao wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea katika Mji wa Mascut nchini humo.
Msanii wa Sanaa ya Ufumaji Bi Mtumwa Omar Bakar akifurahia jambo na Balozi waTanzania Nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh kulia mara baada ya Balozi huyo kuwatembelea Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea katika Mji wa Mascut.
Msanii wa Sanaa ya Mapambo mbalimbali kutoka Tanzania Rahma Juma (Kushoto) akifurahia jambo  na Balozi wa Tanzania Nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh (kulia) mara baada ya Balozi huyo kuwatembelea Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea katika Mji wa Mascut nchini humo katikati ni Mshiriki mwingine Masika Mohamed.
Balozi wa Tanzania Nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh kulia akipata Maelezo kutoka kwa Wajasiriamali wa Bidhaa za Viungo mbalimbali ikiwemo Karafuu kutoka kushoto ni Kulthum Mohamed na Saumu Abdalla na Mke wa Balozi huyo.Balozi Saleh alifanya ziara ya
kuwatembelea Watanzania hao wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea katika Mji wa Mascut.
Msanii wa Kuchora Katuni nchini Tanzania Maarufu kama Tingatinga kushoto Mussa Suleiman Augosi akipokea nasaha kutoka kwa Balozi wa Tanzania Nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh kulia..Balozi Saleh alifanya ziara ya 
kuwatembelea Watanzania hao wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea katika Mji wa Mascut.
Mjasiriamali wa Mavazi mbalimbali ikiwemo ya Kimasai Bi Anna Matinde akitoa ufafanuzi wa bidhaa zake kwa Balozi wa Tanzania Nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh kulia. Balozi Saleh alifanya ziara ya kuwatembelea Watanzania hao wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea katika Mji wa Mascut.
Mjasiriamali wa Mapambo mbalimbali ya ndani Khadija Faraji akitoa ufafanuzi wa bidhaa zake kwa Balozi wa Tanzania Nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh kulia. Katikati ni Mke wa Balozi huyo.Balozi Saleh alifanya ziara ya kuwatembelea Watanzania hao wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea katika Mji wa Mascut
Balozi wa Tanzania Nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akibadilishana Mawazo na baadhi ya Watanzania Mavazi wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea katika Mji wa Mascut nchini humo kutoka kulia ni Mkuu Msaidizi wa Msafara Masha Hussein, Bi Anna Matinde na Mkuu wa mambo ya kiufundi wa Msafara Bi Moza Habib. Balozi Salehe alifanya ziara ya kuwatembelea katika Maonesho hayo.
Balozi wa Tanzania Nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh mwenye Koti Jeusi akifurahia jambo  na Wapishi wa Mashi ya Kitanzania mara baada ya Balozi huyo kuwatembelea Watanzania hao wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea katika Mji wa Mascut nchini humo katikati ni Mshiriki mwingine Masika Mohamed.
Picha na Faki Mjaka-Mascut Oman.

HATIMAYE PROF. SOSPETER MUHONGO AKABIDHI OFISI KWA SIMBACHAWENE JIJINI DAR LEO *PICHAZ*

Waziri  mpya wa Nishati na Madini,George Simbachawene (kulia)
akikabidhiwa rasmi nyaraka za ofisi na Aliyekuwa Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo, leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Waziri  mpya wa Nishati na Madini,George Simbachawene (kulia)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati makabidhiano
ya ofisi na Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo, leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

ALIYEKUWA Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo amesema uadilifu unahitajika katika sekta ya Nishati na Madini pasiwepo na rushwa kwani hiyo ni kuweza kusaidia watanzania masikini wanaongalia sekta hiyo kwa maendeleo ya uchumi wao.

Muhongo ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akikakabidhi ofisi kwa Waziri  mpya wa Nishati na Madini,George Simbachawene,amesema lazima kuwepo na uzinagatiaji wa mikataba ili watanzania waweze kunufaika na rasilimali zao.

Muhongo amesema Simbachawene sio mtu wa tamaa siku zote alipokuwa Naibu wa Waziri wa Nishati na Madini walikuwa wakiambiana juu ya kuwatumikia watanzania wengi na sio mtu binafsi.

Amesema lazima tujenge uchumi imara kutokana na sekta hii ili watanzania waweze kukua kiuchumi kutokana na sekta ya madini inavyokua kwa kasi.

Muhongo amewataka waandishi kuelimisha watanzania kwa ajili ya ustawi wa taifa na sio mtu mmoja au ubinafis wa mtu.

Kwa upande wa Simbachawene amesema ataendeleza mazuri yaliyoachwa na mtangulizi wake kwa  kuweka uwazi kwa kila kitu kinachofanyika,kwani ofisi ya umma sio mali ya mtu.

Saturday, January 24, 2015

ICHEKI VIDEO MPYA YA BEBE COOL - ‘EVERYWHERE I GO’

BEBE Cool ni miongoni mwa wasanii wakubwa Uganda mwenye hit nyingi kwenye tv na radio.
Hii video yake mpya Every were i go, wimbo unatoka kwenye album yake mpya ya Go Mama ya mwaka 2015. Video imetayarishwa na God Father Productions.
Bonyeza play kuitazama, kisha tuachie comment yako hapo chini!

'I HATE MY WIFE' FILAMU ILIYOMKOROGA SHAMSA FORD

MARA nyingi humtokea mtu yoyote ambaye anafanya kazi fulani hata kama kaizoea kiasi gani lakini kuna kipindi inafika anakutana na ugumu wa kazi hiyo anayoifanya.
Shamsa Ford kutoka kiwanda cha filamu Tanzania amekubali kutuambia kwake filamu ipi ilimpa ugumu wakati anaigiza>>’Filamu ya I hate my wife kwangu ilikua ngumu kidogo kwenye kucheza ambayo nilicheza na Rado na Jb’
Kwenye sentensi nyingine amesema>’Ugumu ulikuwepo pale nilipotakiwa kuigiza kama mchawi,kuna watu wengine walikua wananiogopa mtaani  wakawa wananiita mtaani Shakabula Shakabula’.

ICHEKI VIDEO MPYA KUTOKA YAMOTO BAND #NITAKUPWELEPWETA

ymt2
STYLE ya muziki wanaoufanya imewafanya kupanda mashabiki wa umri tofauti,Yamoto Band wametuletea video yao mpya hii inaitwa Nitakupwelepweta,imeongozwa na Adam Juma.

Bonyeza play kuitazama mwanaULIMWENGU WA HABARI

ZILIZOSOMWA ZAIDI