Pengine umewai kujiuliza kwanini ukiifadhi viazi ulaya au viazi vitamu nyumbani havikai muda mrefu vikiwa vizima ,naamini mara nyingi umehifadhi viazi vikaaribika kwa kutoa maji,kutengeneza rangi yakijani, kuanza kuota vikiwa stoo na wakati mwingine kutengeneza rangi nyeusi na kijani unapovipika
Viazi na vitunguu maji vimehifadhiwa pamoja
Viazi na vitunguu maji huendana vizuri sana katika mapishi ,Lakini ni maadui wakubwa inapofika katika suala zima la uhifadhi wake.Havifai kuhifadhiwa pamoja kwani vitunguu huozesha viazi kwa haraka sana
Kwanini Vitunguu huozesha viazi
Vitunguu vina gesi asilia aina ya Ethylene,gesi hii ndio huaribu viazi.Ethylene husababisha viazi vichuje maji yake ya asili, tendo hili hufanya viazi viharibike au vioze kwa haraka.
kiazi kilichoharibika kwa kuchuja maji baada yakuhifadhiwa pamoja na vitunguu.
Gesi ya Ehylene hupatikana kwa wingi kwenye aina mbalimbali ya matunda na mboga ,baadhi ya matunda hayo ni pamoja na Ndizi mbivu,apples ,maembe na nyanya.
Unapohifadhi viazi na vitunguu katika eneo moja au stoo moja hakikisha unavitenganisha na unaviweke mbalimbali.
Namna sahihi ya kuhifadhi viazi
Viazi ni chakula chenye asili ya mizizi.Ni moja kati ya vyakula visivyohifadhiwa frijini.Unaweza kuhifadhi viazi vibichi adi wiki nane vikiwa vizima endapo utazingatia kanuni za uhifadhi sahihi.
Hifadhi viazi mahali pakavu ,penye hewa yakutosha na pasipokua na mwanga.Tandika karatasi juu ya chombo au mahali unapohifadhia viazi.
Unyevu: huozesha viazi kwa haraka sana kwani hutoa hali nzuri ya bacteria waharibifu kuzaliana kwa haraka
Joto:Huozesha viazi,viazi huitaji sehemu yenye hewa yakutosha
Mwanga:Mwanga huaribu viazi nakufanya vibadilike rangi yake yaasili na kutengeneza rangi yakijani.Tunza viazi sehem ya giza au isiyokua na mwanga.
Karatasi:Husaidia kutunza ukavu hivyo kutotengeneza mazingira ya bacteria waharibifu kuzaliana
Usioshe viazi adi pale unapotaka kuvitumia,kuosha viazi kisha ukavitunza hufanya viazi viharibike haraka.Endapo kiazi kimoja kitaonyesha dalili yakuharibika kitoe haraka kwani kitaharibu na viazi vingine.
Uhifadhi nwa viazi frijini
Unaweza kuhifadhi viazi frijini endapo vimekwisha menywa ,uhifadhi huu niwamuda mfupi wa siku mbili au tatu.Unaweza kuhifadhi viazi kwakugandisha na vikakaa muda mrefu.Uhifadhi huu wa friji na kugandisha hubadili ladha ya viazi na viazi huwa rojo unapovipika.Ni vyema kujua kwamba uhifadhi huu pia unambinu zake
Kuna njia yakienyeji yakuhifadhi vyakula vyenye asili ya mizizi,watu wa makabila ambayo ni wakulima wazuri wa viazi na mihogo hutumia sana njia hii.
Katika makala zijazo Tutaangazia zaidi juu ya gesi ya Ethyleme kwani inanafasi kubwa sana katika uhifadhi wa mboga na matunda .