NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Wednesday, December 23, 2015

OMMY DIMPOZ: NIKO TAYARI KUOA HATA SASA,KAMA NIKIPATA…!


STAA wa Bongo Fleva,Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ amesema kuwa yuko tayari kuoa hata sasa hivi kama nikipata mtu sahihi katika maisha yake.
Ommy ameyazungumza hayo wakati akiitambulisha video ya ngoma yake mpya iitwayo ‘Achia Bodi’ kwenye kipindi cha Clouds360  cha Clouds Tv wakati alipoulizwa na mtangazaji kipindi hicho Hudson Kamoga kuwa anatarajia kuoa lini.
Niko tayari kuoa hata sasa hivi kama nikipata mtu sahihi katika maisha yangu” Ommy Dimpoz.
Miezi ya hivi karibuni msanii huyo alitupia picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na msichana ambapo picha hizo zilizua maswali kwa mashabiki wake na kuuuliza huenda alikuwa ndiye shemeji yao,lakini hawakupata jibu.

WATU 7 WAFARIKI KWA KUUNGUA MOTO BAADA YA GARI KUPINDUKA NA KUWAKA MOTO

WATU saba wamefariki duniani na wengine kumi wamejeruhiwa katika ajali ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka na kulipuka na kuwaka moto.

Akiongea na mtandao huu ofisini kwake Mganga Mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Kigoma Maweni Dkt. Leonard Subi amesema kuwa jana majira ya saa 12 jioni walipokea miili ya marehemu 6 na majeruhi 11 ilipofika saa 6 usiku majeruhi mmoja alifariki duniana na kupelekea idadi ya vifo kuwa saba.

Aliwataja waliofariki katika ajali hiyo ni Ashura Mussa, Kadogo Yusuph, Kabwe Iddy, Mwamvua Juma na Peter Sungura,maremu wawili miili yao bado haijatambulika sababu ya kuungua vibaya.

Dkt. Subi aliwataja pia majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Andrew Peter, Amos Thomas, Mutta Hamis, Shabaan Fadhil, Hassan Kasa, Esau Elias, Asha Kassim na Riziki Jaah.

"Majeruhi wote wamelazwa wodi namba saba na hali zao siyo nzuri wanaendelea na matibabu, mtoto aitwaye Riziki Jaah mwenye umri wa miezi nane ndiye aliyenusurika katika ajali hiyo hajaumia popote mama yake alimtupa dirishani baada ya moto kuwaka ila mama yake alifariki kwa kuungua kwenye ajali hiyo"alisema Dkt. Subi.

Naye Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma, Ferdnand Mtui amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya gari aina ya Toyota Hiace lenye  namba T.700 ADK lililokuwa likitoka Kigoma mjini kwenda katika kijiji cha Subankala kata ya Ilagala Wilayani Uvinza kilichopo mwambao mwa ziwa Tanganyika.


Kamanda Mtui alisema kuwa ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Mwakizega na chanzo cha ajali hiyo ni dereva kuwakwepa watembea kwa miguu kisha kugonga gema iliyopelekea gari kupinduka na kuwaka moto.

ZITTO KABWE ACHEKELEA UTABIRI WAKE KUTIMIA ZANZIBAR....MAJESHI YAANZA KUONDOLEWA

KIONGOZI wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ameelezwa kufurahishwa na jitihada za kumaliza mzozo wa kisiasa visiwani Zanzibar,huku akitaja baadhi ya mbinu ambazo chama chake waliishauri Serikali ambazo zimeanza kuchukuliwa hatua.

Hii hapa chini ni post yake katika mtandao wa facebook juu ya suala hilo

Zanzibar tartiibu….

Disemba 20 mwaka huu 2015 Kamati ya Uongozi ya Chama cha ACT Wazalendo ilitoa tamko lake baada ya kufuatilia hali ya Zanzibar.

Moja ya mambo yaliyoelezwa katika tamko hilo ni uwepo wa askari wengi katika kisiwa hicho hali iliyokuwa inatishia amani kwa wananchi

Taarifa hiyo ya ACT mbali na masuala mengine, ikaeleza kuwa ni wakati muafaka kwa serikali kuhakikisha inawarudisha askari hao wa vikosi mbali mbali kuanzia jeshi la Polisi,JKU,KMKM JWTZ na Mafunzo katika makambi yao.

Lengo likiwa ni kuwaacha wananchi wakiwa katika uhuru wa kufanya shughuli zao wakati suala la mtanziko wa kisiasa kisiwani humo ukiwa unafanyiwa kazi

Kuanzia jana Disemba 22 na leo Disemba 23 majeshi hayo yameshaanza kuondoka katika maeneo mbali mbali ya mji wa Znz hali inayoashiria mwanzo wa mwisho mwema katika kadhia ya uchaguzi wa Zanzibar.

Ninaomba mamlaka husika ziendelee kufanyia kazi mapendekezo yetu mengine ili kulimaliza kabisa suala hili.

Wednesday, December 9, 2015

RAIS MAGUFULI AKIFANYA USAFI DAR ES SALAAM DEC 9 2015

Rais John Magufuli na Watanzania wengine walivyoshiriki katika siku ya usafi Tanzania Dec 9, 2015
Unayapata yote kwa kubonyeza Play hapa chini.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI NA WANANCHI WA ENEO LAKE KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA, MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kufagia na baadhi ya wananchi wakazi wa eneo lake la Oysterbay Karume Raod, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo Dec 9, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuzoa taka na baadhi ya wananchi wakazi wa eneo lake la Oysterbay- Karume Raod, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili eneo la Kituo cha Daladala cha Morocco, kwa ajili ya kuendelea kushiriki na wananchi wa eneo hilo kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiingia kukagua eneo la kuhifadhia Taka lililopo eneo la Kituo cha Daladala cha Morocco, wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kuendelea kushiriki na wananchi kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuzoa taka na baadhi ya wananchi wa eneo Morocco, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi na wasanii mbalimbali waliojitokeza kushiriki naye katika zoezi hilo baada ya kuhitimisha zoezi la usafi eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoka eneo la Morocco, baada ya kushiriki zoezi hilo na wananchi wa eneo hilo la kufanya usafi wa mazingira leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo ameshiriki katika zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya Mtaa wa Oysterbay na Morocco stand katika wilaya ya Kinondoni katika kuadhmisha miaka 54 ya uhuru wa Tanzania Bara.
Akizungumza na wananchi waliojumika katika maeneo ya Morroco stand Makamu wa Rais amewaagiza viongozi wa wilaya za mkoa wa Dar es salaam kutoa taarifa za wazabuni wa kufanya usafi ili ziweze kufuatiliwa.
“Haya makampuni yanapewa fedha kwa ajili ya kazi ya kufanya usafi; lakini inaonyesha hayafanyi kazi ipasavyo kwa sababu mji bado ni mchafu,” Alisema Mhe. Samia.
Alielezea kufurahishwa kwake kwa jinsi wananchi walivyojitokeza katika zoezi hilo ambalo alisema ni endelevu na kuwataka Wakuu wa wilaya na wenyeviti wa serikali za mitaa kupanga siku maalum kwa ajili ya kufanya usafi katika maeneo yao.
Makamu wa Rais alisema Watanzania hawawezi kujivunia miaka 54 ya uhuru ikiwa miji ni michafu na kuwataka wananchi kushirikiana kutekeleza kauli mbiu ya uhuru na kazi kwa kila mmoja kufanya kazi bidii mahali alipo aweze kuongeza  tija ambayo italiwezesha Taifa kupata madawa na elimu bora.
Pamoja na wananchi waliojumuika na Makamu wa Rais kufanya usafi katika Mtaa wa Oysterbay, kwa upande wa Morocco stand walikuwepo pia wafanyakazi wa benki ya DTB, Radio ya EFM na wasanii mbalimbali
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
 Dar es salaam

RONALDO AVUNJA REKODI YAKE NA KUWEKA MPYA

IGxwi
Mchezaji bora wa dunia mwaka 2014 na mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo (pichani)ameweka rekodi mpya katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA baada ya hapo jana kufunga goli 4 katika mchezo kati ya Real na Malmo.
Magoli ya Ronaldo yalifungwa katika dakika ya 39, 47, 50 na 58 na kufanikiwa kufikisha magoli 11 katika michezo ya makundi rekodi ambayo ilikuwa haijawahi kufikiwa na mchezaji yoyote.
Kabla ya kuweka rekodi hiyo mpya, Ronaldo alikuwa na rekodi ya kufunga goli 9 katika hatua ya makundi kwa msimu wa 2013/2014 rekodi ambayo pia ilikuwa imefikiwa na mchezaji wa Shakhtar Donetsk, Luiz Adriano aliyoiweka mwaka jana.
Baada ya kufikisha magoli hayo Ronaldo anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga 11 katika michezo ya hatua ya makundi akifuatiwa na Luiz Adriano goli 9 na Ruud Van Nistelrooy, Hernan Crespo na Filippo Inzaghi ambao walifunga goli 8 kila mmoja.
Magoli mengine ya Real Madrid katika mchezo huo wa Malmo yalifungwa na Karim Benzema dakika ya 12, 24, 74 na Mateo Kovacic dakika ya 70.

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ASHIRIKI ZOEZI LA USAFI SOKO KUU LA CHALINZE

jk1

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Welle Ndikilo wakielekea soko kuu la Chalinze kushirikiana na wananchi kufanya usafi wa mazingira leo Desemba 9, 2015 ikiwa ni kuadhimisha miaka 54 ya UHURU kama ilivyoagizwa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli.
jk2
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakifanya usafi katika soko kuu la Chalinze leo Desemba 9, 2015 ikiwa ni kuadhimisha miaka 54 ya UHURU kama ilivyoagizwa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli.
jk4
jk5
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na wananchi wa Chalinze baada ya kushirikiana nao kufanya usafi wa mazingira ya soko kuu la Chalinze leo Desemba 9, 2015 ikiwa ni kuadhimisha miaka 54 ya UHURU kama ilivyoagizwa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli.

WAZIRI MKUU ATAKA ZOEZI LA USAFI LIWE ENDELEVU

IMGS4237
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafisha mtaro wa maji machafu kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadiki.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
IMGS4254
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekea eneo la shimoni kwenye soko kuu la Kariakoo kufanya usafi Desemba 9, 2015.
IMGS4277
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitoka eneo la shimoni kwenye soko kuu la  Kariakoo kufanya usafi Desemba 9, 2015. Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
IMGS4287
IMGS4343
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na umati ulioshiriki katika kufanya usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015.  Kulia kwake ni  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadiki na Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
IMGS4392
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na umati ulioshiriki katika kufanya usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015.  Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
IMGS4402
Waziri Mkuu,Kassim Majliwa akiwa amezongwa  na wananchi wakati alipokwenda kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam kufanya usafi Desemba 9, 2015.
IMGS4351
Baadhi ya washiriki wa zoezi la usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam wakipiga picha kwa kutumia simu wakati Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa alipozunguza nao baada ya kufanya usafi  sokoni hapo  Desemba 9, 2015.
IMGS4433
 Gari alilopanda Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa likitoka kwenye eneo la soko kuu la Kariakoo alikokwenda kushiriki katika kufanya usafi Desemba 9, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
IMGS4437
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema zoezi la usafi lililofanyika leo nchini kote lisiishie hapo bali liwe endelevu ili Tanzania iwe na taswira nzuri kwa wageni wanaoingia nchini.
Ametoa wito huo leo kwenye soko la Kariakoo wakati akishiriki zoezi la kufanya usafiikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli la kutaka maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru yasiwepo na badala yake watu wote washiriki kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.
Waziri Mkuu Majaliwa pia amewataka viongozi wa soko la Kariakoo wafike ofisini kwake Jumatatu ijayo (Desemba 14, 2015) saa 4 asubuhi ili wamueleze wana mikakati gani ya kuboresha utoaji huduma kwenye soko hilo.
“Natambua kuwa siyo sahihi kupanga chini biashara tulizonazo. Nataka hawa viongozi waje wanieleze wana mpango gani endelevu wa kuboresha soko hili,” alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.
Waziri Mkuu ambaye alienda kufanya usafi kwenye soko hilo,  alilazimika kuzungumza na mamia ya wananchi waliofika kushiriki zoezi hilo. Pia alikagua maeneo mbalimbali ya soko hilo hadi shimoni na kusema aneridhika na usafi uliofanyika bali amesisitiza usafi huo uendelezwe.
“Kaulimbiu ya Mheshimiwa Rais Magufuli ya HAPA KAZI TU inatupa ari ya kufanya kazi. Fanyeni kazi. Watanzania mko huru kufanya kazi yoyote lakini cha msingi fuateni taratibu na kanuni. Serikali hii tumamua kuwajali watu wa chini. Tutahakikisha wajasiriamali wadogo, akinamama lishe na wamachinga mnafanya kazi kwa amani na utulivu, ” alisema.
Rais Magufuli aliamua kuitangaza siku ya leo (Desemba 9, 2015) ambayo ni maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru iwe ni siku ya kufanya usafi nchi nzima ili kuepukana na magonjwa mbalimbali na hasa kipindupindu.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
DAR ES SALAAM.

RAIS WA ZANZIBAR DK.ALI SHEIN AJUMUIKA WATANZANIA KATIKA WAZANZIBARI KUADHIMISHA DISEMBA 9 KWA KUFANYA USAFI LEO


 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akifuatana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Zanzibar Khatib Abrahman Khatib wakati alipowasilikati eneo la Malindi Mjini Zanzibar katika zoezi ka Usafi wa mazingira katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililoshirikisha Viongozi na Wananchi mbali mbali nchini.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizoa taka katika  zoezi ka Usafi wa mazingira katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania eneo la Malindi Mjini Unguja leo zoezi ambalo liliwashirikisha Viongozi na Wananchi mbali mbali nchini (kushoto) Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban,
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizoa taka katika  zoezi ka Usafi wa mazingira katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania eneo la Malindi Mjini Unguja leo zoezi ambalo liliwashirikisha Viongozi na Wananchi mbali mbali nchini (kushoto) Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)  akimimina taka katika kontena  baada ya kufanya usafi wa madhingira leo wakati wa  zoezi hilo lililofanyika nchi nzima  katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo eneo la Malindi Mjini Unguja,ambapo viongozi mbali mbali walijumuika katika kufanikisha kazi hiyo,
 Baadhi ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ walishiriki katika zoezi ka Usafi wa mazingira katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania eneo la Malindi Mjini Unguja leo zoezi ambalo liliwashirikisha Viongozi na Wananchi mbali mbali nchin
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)  akitoa nasaha zake baada ya kumalizika kwa zoezi la kufanya usafi  wa madhingira leo wakati wa  zoezi hilo lililofanyika nchi nzima  katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo eneo la Malindi Mjini Unguja,ambapo viongozi mbali mbali walijumuika katika kufanikisha kazi hiyo,(kushoto)Mstahiki Meya wa Manispaa ya Zanzibar Khatib Abrahman Khatib,
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ walishiriki katika zoezi ka Usafi wa mazingira katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania eneo la Malindi Mjini Unguja leo zoezi ambalo liliwashirikisha Viongozi na Wananchi mbali mbali nchini.
#Picha na IKULU-Zanzibar

Tuesday, December 1, 2015

SAKATA LA MAKONTENA: POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA TRA WAKAMATA MAKONTENA 9

Maofisa wa Jeshi la Polisi  Dar es Salaam kwa kushirikiana na TRA, wanayashikilia makontena 9   Mbezi Tanki Bovu baada  ya  kuyatilia shaka kuwa yalikuwa yanasafirishwa kinyememela usiku wa kumakia leo

ZILIZOSOMWA ZAIDI