NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Tuesday, September 30, 2014

SENTENSI 'KUNTU' ALIZOZIONGEA MUME WA LADY JAY DEE, GADNER G. HABASH KWENYE MKASI!

MTANGAZAJI Gardner G. Habash ni miongoni mwa Watangazaji hodari ambao Tanzania imewahi kuwa nao ambapo alianza kwa kusikika kupitia CloudsFM kwenye shows mbalimbali ikiwemo Jahazi kabla ya kuanza kazi.Wakati huu ambapo kumekua na stori zilizoenea mtaani kuhusu yeye na ndoa yake pia kazi, show ya TV ya Mkasi inayoongozwa na mtangazaji Salama Jabir imepata nafasi Exclusive ya kuongea nae. Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya sentensi alizoziongea Captain G kwenye Mkasi on EATV.
Kwanza alianza kwa kuongelea jinsi alivyoingia kufanya kazi Redioni hukuakimkumbuka Othman Njaidi aliemchukua na kumpeleka CloudsFM sio kama mtangazaji bali akajiunge na timu ya Marketing, akakutanishwa na Ruge Mutahaba aliekua General Manager wakati huo ambae alipoisikia tu lafudhi ya Gardner akasema huyu anafaa kuwa mtangazaji.
Staa aliefurahi baada ya kukutana nae ni D’Banj wa Nigeria, alifurahia uchangamfu wake…

Salama alipomuuliza kuhusu uhodari wake wa kutangaza habari za mastaa wa dunia… Captain G. akasema ‘nilikua nanunua majarida kwenye maduka yanayouza majarida kutoka nje, wakati Internet hamna kulikua na majarida mengi kidogo’

‘Mimi ni mchaga kabisa wa Baba na Mama lakini Wazazi wangu walihamia Tanga zamani alafu mimi nimezaliwa Ngamiani pale Hospitali na tukaishi Chumbageni muda mrefu kwa hiyo nilipata lafudhi ya Tanga pale, na hiyohiyo lafudhi ya Tanga ndio iliyonipa kazi kwenye Radio’

Salama akamuuliza ‘Unajisikiaje ukisikia mtu anatangaza kama wewe‘ >> Gardner akajibu ‘kuna baadhi ya watu kusema ukweli wanachukizwa sana na hicho kitu na wananilalamikia sana kwamba kuna Watangazaji wengi wamekua wanakuiga kwenye kutangaza Redioni na kwenye kutengeneza jingle kama za kwako lakini mimi nimeiona ni baraka kwangu, kama watu wamekupenda kiasi kwamba wanakuiga ni jambo la kufurahisha kwangu mimi linanifurahisha sana’

Kuhusu kitu kilichomfanya akaondoka kwenye Radio, Captain amesema ‘Nilifanya kazi miaka 9 akili ikawa imechoka nikafikiria lazima pia nifanye biashara watu wanakusifia kwamba una uhodari flani kwa hiyo unajipa challenge kwanini nisitengeneze kitu changu, ndio tukafungua biashara za chakula lakini zaidi nilikua nataka kupumzika’

Swali jingine kutoka kwa Salama likawa ‘nasikia kuna stori kwamba hivi karibuni pia unaweza kurudi kule ama ukaenda sehemu nyingine‘ Captain G. akajibu >>> ‘ni mmoja kati ya hao wawili, stori ni ya ukweli ndio maana naondoka, nimemaliza mkataba nimepata ofa nyingine kubwa naichukua’

Swali jingine lililokua linasubiriwa ni hili alilouliza Salama >> ‘kuna stori mtaani kwamba wewe na Lady Jaydee mmeachana’ Gardner akajibu ‘mimi sijawahi kupata interview muda mrefu sana… nadhani hii inaweza kuwa interview yangu ya kwanza, kwahiyo nilikua nataka nikuombe tuongee kuhusu mimi kwanza manake tukizungumzia kuhusu JayDee nitafunikwa hapa’

MAGAZETI YA LEO JUMATANO 01/10/2014

1_0cc44.jpg
32_12885.jpg2_844cf.jpg33_fe5d8.jpg
7_c94b9.jpg25_f06a0.jpg
3_c9cbe.jpg26_ce2f3.jpg
4_c8bf4.jpg30_70cf9.jpg
5_06a5b.jpg
27_2cd1d.jpg6_0a1c2.jpg31_cb691.jpg
8_f1f90.jpg29_dcc76.jpg
9_1cb9f.jpg28_72b03.jpg
11_b1c7f.jpg39_d824a.jpg

VANESSA MDEE ALIA NA WATANZANIA

VANESSA MDEE ambaye yeye pamoja na Diamond Platnumz na Peter Msechu wamechaguliwa kuwania tuzo za ‘All Africa Music Awards, AFRIMA 2O14, amesema kama Watanzania watawaunga mkono wana nafasi ya kuiletea nchi sifa kubwa.
 
Vanessa amesema kuwa muziki wake unaonesha mwanzo mzuri wa kuanza kutambulika zaidi kimataifa.
“Inaonyesha ile kazi tunayofanya kila siku tunavyoamka tunaenda studio, tunavyofanya show tunaonekana tunakubalika,” amesema Vanessa. “Kusema kweli nilivyokuwa naanza muziki nilikuwa naona nitafanya vitu vikubwa na Mungu ndo anazidi kunifungulia milango, yaani sasa hivi kila kitu kinaenda sawa. Pesa tuliyoweka kwenye muziki inaanza kurudi kama unavyoona nominations, watanzania wengi tumepata nomination Peter Msechu, Diamond and myself ndio tumepata nomination. Kusema ukweli hiki ni kitu kikubwa sana kwetu. Kwa sasa tunaendelea kuonekana watanzania kimuziki.”
“Mimi ningependelea kuendelea kupata support kutoka kwa watanzania. Ukiangalia Wanigeria wanashikana sana, Wasouth wanashikana sana, na naona Wakenya wanashikana sana kwenye mambo ya muziki wao. Kushikana lazima tushikane, kweli ninafikiria watanzania wataona umuhimu wa ku-support kazi za nyumbani, kusaidia wasanii wa nyumbani Diamond, Peter na mimi kwenye Afrima,” alisema Vee.
  
Diamond Platnumz ambaye pia anawania tuzo hizo.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI

SHIRIKA la ndege la Australia linalofahamika kama Qantas limeanza kurusha ndege yake ambayo inatajwa kuwa kubwa zaidi ya abiria duniani na inayofanya safari zake kwa umbali mrefu zaidi.
Ndege hiyo iliyotwa kama Airbus A380 ilitua katika uwanja wa kimataifa wa Dallas-Fort Worth saa 15 tangu ilipoondoka Sydney, Australia safari ya Kilometer 13,805 ikiwa na abiria 480.
Uwanja wa kimataifa wa Dallas- Fort Worth ni uwanja mkubwa wa ndege unaounganisha ndege zote za Marekani na Latin America. Uwanja huo umeonekana kufaa zaidi kwa ndege hiyo. 
Angalia picha za ndani:

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

.
.
.
20_9305d.jpg

21_70ca3.jpg

BONGO MOVIE MAJANGA:: ANGALIA WALICHOFANYA IRINE UWOYA NA RICHIE, KINAKUBALIKA? *VIDEO*

Tasnia ya filamu nchini huenda ikawa na mengi yanayofanyika nyuma ya pazia wakati wa majaribio ya kutafuta shots nzuri zenye uhalisia hasa kwenye scene za mapenzi!
Lakini napata kigugumizi kikali kwa kile kilichoonekana kwenye video hii inayoaminika kuwa ni kipande cha filamu mpya inayotarajia kutoka iliyowakutanisha Rich na Irene Uwoya ambao wanaonekana wakibadilishana mate kwa kiss za uweli.
Je, uhalisia huu kwenye filamu za Bongo unakubalika kimaadili? Bila shaka haukubaliki hapa kwetu Tanzania.

CHAMA KIPYA CHA ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY ‘ACT’ CHAPOKEA WANACHAMA WAPYA

 
Mwanachama wa zamani wa CHADEMA, Batuli Abdallah  akijieleza mbele ya wanahabari (hawako pichani)
 
 Yassin Bahama aliyekuwa mwanachama wa zamani wa Chadema akizungumza.
 
Mohamed Ngulangwa aliyekuwa mwanachama wa zamani wa CCM akivaa fulana ya chama hicho.
 
Wajumbe waliohudhuria mkutano.
 
Mwenyekiti  wa ACT,  Hamis Chambuso akiwa ameshika kadi za Chadema zilizorudishwa na wanachama hao wapya.
 
Wajumbe na wanahabari wakiwa mkutanoni.

CHAMA cha siasa hapa nchini cha Alliance for Change and Transparency ‘ACT, leo kimewapokea wanachama wapya ambao wamehama toka vyama mbalimbali vya siasa nchini.

Waliopokelewa ni  Yassin Bahama aliyekuwa mjumbe wa serikali ya mtaa wa matofalini,  Ujiji Kigoma, Batuli Abdallah aliyekuwa Katibu  Mwenezi Bavicha katika Jimbo la Kawe, Ofisa na mwasisi  wa chama cha Chauwa,  Sylvester Kasonga pamoja na Engineer Mohammed Ngulangwa toka Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza  mbele ya GPL, eneo la Msasani Club, jijini Dar, Mwenyekiti  wa Mkoa wa ACT, Hamis Chambuso amewakaribisha na kuwapongeza  wanachama hao wapya kwa hatua waliyoichukua.
(Habari/Picha na: Gabriel Ng’osha/GPL)

RAILA ODINGA ACHAPWA VIBOKO UKUMBINI WAKATI AKICHEZA NGOMA

HALI ya taharuki iliibuka katika mkutano wa hadhara katika jimbo la Kwale nchini Kenya, baada ya mwanamume mmoja kwenda ukumbini na kuanza kutandika bakora kiongozi wa upinzani Raila Odinga pamoja na wanasiasa wengine.

Raila alikuwa amejiunga na kikundi cha wanawake waliokuwa wanacheza densi ya kitamaduni kuwatumbuiza wageni, pamoja na gavana wa jimbo la Kwale Pwani ya Kenya Salim Mvuruya katika mkutanmo wa kisiasa.

Walikuwa wameambatana na viongozi wengine, wakiwemo, Seneta Juma Boy, Hassan Omar, Agnes Zani, James Orengo, Johnstone Muthama na wengineo.

Mwanamume huyo alimshambulia Odinga ambaye ni waziri mkuu wa zamani na kumchapa mara mbili kabla ya kumgeukia gavana wa jimbo hilo na pia kumchapa mara mbili. Hata hivyo mwanamume huyo alishindwa nguvu na walinzi wa Raila Odinga.

Polisi walithibitisha kuwa walimkamata mwanamume huyo na kumwachilia baada ya kugundua kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili.

Haijulikani kwa nini mwanammume huyo alimshambulia Raila ila baadhi wabnasema ni kwa sababu alighadhabishwa pale waziri mkuu alipocheza densi na mwanamke aliyesemekana kuwa mke wake ambaye alikuwa katika kikundi cha wanawake waliokuwa wanawatumbuiza wageni waheshimiwa.

Viongozi waliofika walilazimika kusitisha densi hiyo kabla ya mwanamume huyo kushindwa nguvu.

Chanzo: BBC Swahili

BAADA YA KUPATA TUZO MBILI HIKI NDICHO ALICHOKISEMA MSANII RAY

NI POST ya mwigizaji staa wa Tanzania Ray ‘Vicent Kigosi’ instagram ambayo ni baada ya kupata tuzo mbili juzi ambazo ni Life achievement Award na Best Director.
Ray 2
Ameandika >>> ‘Kila kwenye nia kuna njia, tulivyoanza tulionekana kama wauza sura tu lakini sasa hivi naweza sema kuwa tunayafaidi matunda tuliyoyavumilia kwa muda mrefu sana, naweza kuthubutu kusema kuwa sekta ya bongo movie ndio sekta ya bongo iliyotoa ajira kwa vijana wengi sana kuliko sekta yoyote‘

Ray amemalizia kwa kusema ‘Mungu ibariki bongo movie, Mungu ibariki kazi ya mikono yote’

BREAKING NEWS: EBOLA YATUA NCHINI MAREKANI KWA OBAMA

Ugonjwa wa Ebola bado unapasua vichwa vya wanasayansi walio wengi katika kuutafutia chanjo ama tiba ili kukabiliana nao, ingawa mpaka sasa walau kuna matumaini ya dawa ya Zimapp.

Mgonjwa wa kwanza ametambuliwa nchini Marekani eneo la Dallas, Texas mahali amabako utafiti wa kilimo unafanyika .

Mgonjwa huyo aliyegunduliwa bado hajatambuliwa na ametengwa kwa uchunguzi ili kumfuatilia na kuepusha kuambukiza watu wengine.Mtu huyo ametambuliwa jinsi yake kuwa ni mwanamume na alipata uambukizo nchini Liberia na hii ni baada ya kuonesha dalili zote za ugonjwa huo.

Mwanamume huyo anaripotiwa kuondoka nchini Liberia mapema mwezi September na kufika mjini Texas siku iliyofuatia bila ya kuonesha dalili za uambukizo wa virusi hatari vya ugonjwa wa Ebola.Mkurugenzi wa ufuatiliaji magonjwa na udhibiti nchini Marekani Thomas Frieden aliwaambia waandishi habari mapema wiki hii kwamba wote waliotembelea nchini Liberia waligundulika na virusi vya ugonjwa huo nchini Marekani

Mpaka sasa watu zaidi ya 3,000 wamefariki dunia huko Africa Magharibi, na baadhi ya wafanyakazi wa kujitolea kutoka nchini Marekani wamepata ahueni baada ya kurejeshwa nchini Mwao pindi walipogundulika kuwa na dalili za awali za ugonjwa huo.

Chanzo: BBC

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

20_bc575.jpg
21_44536.jpg
22_20eef.jpg
23_d8e05.jpg

ZILIZOSOMWA ZAIDI