Ugonjwa wa Ebola bado unapasua
vichwa vya wanasayansi walio wengi katika kuutafutia chanjo ama tiba ili
kukabiliana nao, ingawa mpaka sasa walau kuna matumaini ya dawa ya
Zimapp.
Mgonjwa wa kwanza ametambuliwa nchini Marekani eneo la Dallas, Texas mahali amabako utafiti wa kilimo unafanyika .
Mgonjwa
huyo aliyegunduliwa bado hajatambuliwa na ametengwa kwa uchunguzi ili
kumfuatilia na kuepusha kuambukiza watu wengine.Mtu huyo ametambuliwa
jinsi yake kuwa ni mwanamume na alipata uambukizo nchini Liberia na hii
ni baada ya kuonesha dalili zote za ugonjwa huo.
Mwanamume huyo
anaripotiwa kuondoka nchini Liberia mapema mwezi September na kufika
mjini Texas siku iliyofuatia bila ya kuonesha dalili za uambukizo wa
virusi hatari vya ugonjwa wa Ebola.Mkurugenzi wa ufuatiliaji magonjwa na
udhibiti nchini Marekani Thomas Frieden aliwaambia waandishi habari
mapema wiki hii kwamba wote waliotembelea nchini Liberia waligundulika
na virusi vya ugonjwa huo nchini Marekani
Mpaka sasa watu zaidi ya
3,000 wamefariki dunia huko Africa Magharibi, na baadhi ya wafanyakazi
wa kujitolea kutoka nchini Marekani wamepata ahueni baada ya kurejeshwa
nchini Mwao pindi walipogundulika kuwa na dalili za awali za ugonjwa
huo.
Chanzo: BBC
0 comments:
Post a Comment