NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Tuesday, January 26, 2016

MASWALI 9 ‘MSUKULE’ KUKUTWA NYUMBA YA TAJIRI CHINI YA SHIMO LA CHOO

Hofu imeendelea kutanda maeneo ya Kibamba jijini Dar na kuacha maswali tisa kwa wananchi kuhusiana na mwanamke aliyekutwa kwenye shimo la urefu wa futi kumi, nyumbani kwa mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina moja la Mtei.

HALI YA MWANAMKE HUYO
Mwanamke huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 27, aliwashangaza wakazi wa eneo hilo kwani ndani ya  shimo alilokutwa alionekana mchafu, aliyenyongea, akiwa hoi kwa njaa na mtupu kiasi cha kudhaniwa ni msukule (mtu aliyechukuliwa ndondocha).

SIKU YA TUKIO
Ilikuwa Jumanne ya Januari 19, mwaka huu katika shimo hilo lililojengwa na Mtei, inasemekana kuwa, shimo hilo  ni kwa ajili ya chemba ya choo lakini haijaanza kutumika kwa vile nyumba hiyo nayo haijaanza kukaliwa rasmi na familia zaidi ya kuwepo kwa mlinzi.

 Akiwa uchi shimoni.
UWAZI ENEO LA TUKIO
Kufuatia kusambaa kwa taarifa za mwanamke kukutwa shimoni kwenye nyumba ya mfanyabiashara huyo, Uwazi kama ilivyo ada yake, lilitinga eneo la tukio kwa lengo la kuchimba mawili, matatu kuhusu hali halisi.

MAJIRANI WASHANGAZWA
Baadhi ya majirani wa eneo hilo walionesha kushangazwa na tukio hilo huku wakiwa na maswali hayo tisa kuhusu mwanamke huyo ambaye walisema si mkazi wa maeneo hayo na wala hawajawahi kumuona.

 Mwanamke huyo baada ya kutolewa shimoni.

MASWALI YA MAJIRANI
Ni nani aliyemuingiza shimoni mwanamke huyo na kwa madhumuni gani? Kwani kwa jinsi shimo lilivyo, lazima aliingizwa au aliingia kwa kutumia ngazi.

Alikuwa akiishi kwa kula chakula gani kwani wakati anatolewa, muda mwingi alikuwa akilalamikia njaa.

Swali la tatu ambalo majirani walikuwa nalo, mwanamke huyo aliishi ndani ya shimo hilo kwa siku ngapi? Kwani nywele na kucha zake ziliashiria si zaidi ya mwezi mmoja. Swali kuu, aliingia/ aliingizwa lini na muda gani kati ya mchana na usiku?

Je, aliingizwa kwenye shimo hilo akiwa na nguo zake halafu aliyemwingiza/ waliyomwingiza walizipeleka wapi?

Swali la tano ambalo majirani hao walikuwa wakilijadili sana ni, je! Mwanamke huyo ni mgonjwa wa akili au ni msukule? Kama si chochote kati ya hayo mawili, kwa nini alikuwa hapigi kelele?
Sita, majirani hao waliulizana kama siku za karibuni wamewahi kusikia kwenye vyombo vya habari kuna mwanamke mwenye umri huo anatafutwa? Wote walisema hawajasikia.

Wengi walisema huenda mwanamke huyo aliingizwa kwenye shimo hilo na ‘maadui’ wa biashara wa Mtei. Lakini kama ni kweli, walikuwa na lengo gani na walimpata wapi mwanamke huyo na akiwa katika hali gani?

Katika mahojiano na majirani wakati bado akiwa ndani ya shimo amekaa, mwanamke huyo aliweza kujibu maswali karibu yote, lakini swali la anaitwa nani na ameolewa au la, yalimshinda kujibu. Ni kwa nini?

Polisi Mbezi wanasema wamekuwa wakimpigia simu Mtei, lakini hapokei. Ni kwa nini?

MFANYAKAZI WA MTEI SASA
Naye mfanyakazi anayeitunza nyumba hiyo, Richard Pascal alipozungumza na Uwazi kuhusu tukio hilo alikuwa na haya:

 “Ninachokumbuka mimi, Jumanne, wiki iliyopita, saa 3:00 asubuhi, bosi wangu Mtei alikuja. Ni kawaida yake kuja na kukagua mji wake.

 “Nikiwa naendelea na shughuli zangu, aliniita hapa nje. Nilipofika  aliniambia nichungulie ndani ya shimo. Nilifanya hivyo, nikashtuka sana kumwona mwanamke akiwa mtupu huku akinikodolea macho.
“Niliogopa kwa sababu sikutarajia kama kuna mtu anaishi shimoni bila mimi kujua wakati ndiyo nalinda hapa siku zote.”

Hali aliyokuwa nayo.

AWAITA MAJIRANI
“Niliamua kuwaita majirani. Baada ya muda mfupi watu wakawa wamejazana hapa kila mmoja akishangaa na bosi wangu akatoa taarifa Kituo Kidogo cha Polisi Kibamba ambapo askari walifika.
“Lakini na wao walipatwa na mshangao huku wakijiuliza ni vipi mwanamke huyo aliingia shimoni bila kuumia wala kuvunjika?”

POLISI WAMUHOJI
“Mwanamke huyo alipohojiwa na polisi alisema ameishi humo miaka mingi na mara nyingi alipokuwa akihojiwa alikuwa akililia chakula. Polisi waliniomba ngazi, wakaitumbukiza shimoni kisha yeye mwenyewe akapanda haraka mpaka nje.”

APELEKWA TUMBI
“Polisi walimchukua na kumpeleka Hospitali ya Tumbi (Kibaha mkoani Pwani) ambako nadhani anapatiwa matibabu.”

MLINZI APATA WASIWASI
“Mpaka sasa hivi mimi napatwa na wasiwasi. Nitamuomba bosi wangu aniongezee mtu mwingine ili tuwe wawili, kwani mimi hapa ni mgeni. Nimekuja hapa, Desemba 9, mwaka jana.”

SIKILIZA MAHOJIANO
Uwazi lilifanikiwa kunasa mahojiani kati ya mwanamke huyo akiwa ndani ya shimo amekaa na polisi huku wananchi wakiwa nje wakitaka kumuokoa.
Polisi: “We, unaitwa nani?”
Mwanamke: (kimya).
Polisi: “Unakaa wapi?”
Mwanamke: “Mbezi Makabe.”
Polisi: “Umeolewa?”
Mwanamke: (kimya).
Polisi: “Umekuja lini hapo?”
Mwanamke: “Hapa kwangu.”
Polisi: Umekuja lini?”
Mwanamke: “Mi njaa inaniuma bwana.”

UWAZI NYUMBANI ANAKOISHI MTEI
Uwazi lilifika nyumbani kwa Mtei, Kibamba ya Luguruni jijini Dar, hatua chache tu kutoka kwenye Kituo cha Mabasi Kibamba lakini hakupatikana, Uwazi liliacha namba ya simu lakini hakupiga na ilipopigwa, imekuwa ikiita bila kupokelewa.

UWAZI KITUO CHA POLISI
Siku hiyohiyo, Uwazi lilifika Kituo cha Polisi Mbezi ambapo askari mmoja ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa vile si msemaji wa jeshi hilo, alisema mpaka sasa wanamtafuta Mtei ili kumsikia kwa kina kuhusu tukio hilo kwa vile yeye ndiye aliyepiga simu polisi kutoa taarifa.
“Huyo Mtei, tunamtaka hapa. Yeye ndiye aliyetoa taarifa ya mwanamke kukutwa kwenye shimo nyumbani kwake. Lakini tulipofika hatukumkuta. Na kila tukipiga simu yake, inaita tu bila kupokelewa,” alisema afande huyo.

UWAZI HOSPITALINI TUMBI
Baada ya hapo, Uwazi lilifunga safari hadi Hospitali ya Rufaa ya Tumbi, Kibaha, Pwani ambapo halikufanikiwa kumpata msemaji, lakini muuguzi mmoja wa hospitali hiyo alikiri kupokelewa kwa mwanamke huyo.

UWAZI LAMBANA MTEI
Juzi, Uwazi lilimpigia simu Mtei na mambo yakawa hivi;
Uwazi: “Wewe ni Mtei?”
Mtei: “Eee, unasemaje?”
Uwazi: “Tunaomba ufafanuzi kuhusu yule mwanamke aliyekutwa kwenye shimo nyumbani kwako…”
Mtei: “Ooh! Siyo mimi, yule ni Mchaga mimi ni Muhaya, nipo Kagera.”
Uwazi likamrudia aliyetoa namba…
“Kwani si ulikuwa unaongea naye sasa hivi na akakwambia yeye si Mtei! Nimesikia maongezi yenu, lakini alisogea mbali. Kwa hiyo sijui zaidi.”

KAMANDA WA POLISI KINONDONI
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Christopher Fuime alipoulizwa kuhusu tukio hilo,  alikiri kulitambua na kwamba, bado wanalifanyia uchunguzi.
Yeyote anayemjua mwanamke huyo (pichani ukurasa wa mbele) apige simu namba 0715454656 au 0784 339616, chumba cha habari.
#Global Publishers

NYUMBA YA MCHUNGAJI LAKATWARE YASABABISHA JANUARY MAKAMBA KUCHUKUA HATUA KALI KWA MAAFISA HAWA

SAKATA la maofisa watatu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), waliosimamishwa kazi kwa tuhuma ya kukiuka miiko yao ya kazi, limechukua sura mpya, baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, kuagiza wafikishwe mbele ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Pamoja na hayo, Waziri huyo amemsimamisha kazi aliyekuwa mwanasheria wa baraza hilo, John Mnyele kwa matumizi mabaya ya ofisi.

Akizungumza  jana, alisema tayari amemwagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, kuwasilisha mashtaka yanayowakabili maofisa hao watatu Takukuru kwa ajili ya uchunguzi na hatua zaidi, ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Maofisa waliosimamishwa kazi kutokana na udhaifu huo ni pamoja na Ofisa Mazingira Mwandamizi Dk Eladius Makene, Mwanasheria Daraja la II Wakili Heche Suguta Manchare ; na Ofisa Mazingira Boniface Benedict Kyaruzi. Wanatuhumiwa kukiuka miiko ya kazi yao katika kusimamia kiwanda cha kusindika minofu ya punda kilichopo mkoani Dodoma.

Pamoja na maofisa hao, pia Mwanasheria Mnyele, anayetuhumiwa kuingia mkataba na Mchungaji Getrude Rwakatare wa kuondoa kesi mahakamani kwa niaba ya NEMC bila kuijulisha ofisi, naye anachunguzwa na taasisi hiyo ya rushwa.

Mama Rwakatare kwa sasa ana kesi mahakamani dhidi ya baraza hilo ya kupinga kubomolewa kwa nyumba yake, inayodaiwa kujengwa mahali pasiporuhusiwa.

Kiwanda hicho cha minofu ya Punda cha China, kilianza kazi hiyo rasmi mwaka 2012 huko Dodoma ambapo pamoja na kuchinja, pia huuza nyama hiyo nje ya nchi, hususan China.

Kiwanda hicho kilipatiwa vibali vyote, ikiwemo cha Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) na cha Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi cha kuchinjia.

Pia, kilikuwa na vibali vingine vya Manispaa. Hata hivyo, hakikuwa na kibali cha masuala ya mazingira kutoka NEMC.

Katika ukaguzi uliofanywa siku za nyuma na Baraza hilo, ilibainika kuwa kiwanda hicho hakina kibali hicho cha mazingira, lakini pia kilikuwa kikilalamikiwa na wananchi wanaokizunguka kutokana na kutofuata taratibu za utunzaji wa mazingira.

NEMC ilibaini kuwa kiwanda hicho, hakikuwa na mfumo wa majitaka, lakini pia kilikuwa kikichoma mabaki yanayotumika kuchinjia ndani ya kiwanda hicho na moshi wake kusambaa maeneo yanayokizunguka.

Kutokana na makosa hayo, baraza hilo lilikifungia kiwanda hicho kama adhabu na kukilipisha faini ya Sh milioni 240.

Juzi Waziri January pamoja na kuwasimamisha maofisa hao watatu kwa kukiuka miiko yao ya kazi, pia aliagiza Mkurugenzi Mkuu wa baraza hilo, Mhandisi Bonaventura Baya, apewe barua ya onyo kali na la mwisho kwa tuhuma za udhaifu katika usimamizi wa watumishi wa baraza hilo, hivyo kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa baraza hilo.

WEMA SEPETU KUJIFUNGUA MWEZI AUGUST

Malkia wa filamu, Wema Sepetu anatarajia kujifungua mwezi August 2016, kwa mujibu wa mpenzi wake Idris Sultan.
Akizungumza katika kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM Jumanne hii, Idris alisema mpenzi wake huyo anatarajia kupata mtoto baada ya miezi 6 au 7 hali ambayo imetafsiriwa na wadau wa mambo kuwa huenda mwanadada huyo akawa na mimba ya miezi 3 au 2.
“Yes very soon natarajia kupata mtoto kama miezi 6 au 7 ijayo,” alisema Idris. Pia Idris alisema bado hajatambua jinsia ya mtoto anayetarajia kujifungua mpenzi wake.
“No hatujui mwenzangu anataka surprise. Mimi nataka kujua kabla kwahiyo bado hatujafikia muafaka, naogopa nisije nikawa nanunua vigauni akaja Wa kiume bure,” alisema.
Aliongeza, “Huwezi kuwazuia watu kuongea, waache waongee maana sometimes watu ni wagumu kupokea changes lakini siku zinavyoenda naamini wataelewa tu.”
Pia Idris alisema wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.

JAJI ADAIWA KUPOKEA RUSHWA YA $2M KENYA

Dkt Mutunga ameitisha kikao cha tume ya mahakama Jumatano
Jaji mmoja wa mahakama ya juu nchini Kenya anachunguzwa kwa madai ya kupokea rushwa ya jumla ya $2 milioni kutoka kwa mwanasiasa.
Jaji huyo anadaiwa kupokea pesa hizo ili kumpendelea mwanasiasa huyo kwenye kesi ya kupinga kuchaguliwa kwake kwenye uchaguzi mkuu wa 2013.
Kiongozi wa idara ya mahakama nchini Kenya, Jaji Mkuu Willy Mutunga amekiri kupokea nyaraka kuhusu malalamiko dhidi ya jaji huyo Novemba mwaka jana.
Amesema uchunguzi wa kina umefanywa na ripoti ya uchunguzi itakabidhiwa Tume ya Huduma za Mahakama (JSC), Tume ya Kupambana na Rushwa na afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.
Dkt Mutunga, ambaye majuzi alinukuliwa na gazeti moja la Uholanzi akisema Kenya imeshikwa mateka na “magenge ya wanyang’anyi” na kwamba ufisadi umekita mizizi, ameitisha kikao cha dharura cha JSC.
“Kwa mtazamo wa idara ya mahakama, ukizingatia cheo cha jaji huyu, na uzito wa madai dhidi yake, pamoja na vile kisa hiki kimevutia umma, nitawasilisha suala hili kwa kikao maalum cha JSC Jumatano,” amesema Dkt Mutunga, kupitia taarifa.
Magazeti mengi Kenya yanaongoza na habari hizo

“Tume ya JSC itaendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria na kufuata utaratibu unaofaa," amesema Dkt Mutunga.
#BBC Swahili

ESTER BULAYA AMGARAGAZA TENA WASIRA...ASHINDA KESI YA UCHAGUZI ILIYOFUNGULIWA KUPINGA USHINDI WAKE

Ester Bulaya Ameandika Maneno haya Baada ya Ushindi wa Mahakamani;
"Nilimshinda Wasira kwa wananchi, na leo nimemshinda kisheria, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imetupilia mbali kesi ya Uchaguzi dhidi yangu, iliyofunguliwa na wapambe wa wasira. Mungu husimama na watu waliowema. Nakutumaini mungu wangu na wewe ndiye mlinzi wangu.Asante sana Wananchi wangu wa Bunda Mjini mliokwenda Mwanza kusikiliza Hukumu. Mbunge wenu nipo dodoma tayari kwa kuanza vikao vya Bunge Kesho." Ester Bulaya

WATU WAWILI WAFARIKI KIGOMA BAADA YA KUSOMBWA NA MAJI YA MVUA

Kigoma
Na Emmanuel Senny, Kigoma
Watu wawili wakazi wa Kata ya Kagunga kitongoji cha Zashe Mwambao wa Ziwa Tanganyika Mkoa wa Kigoma wamefariki dunia baada ya  kusombwa na maji kutokana na kunyesha mvua kubwa huku kaya tisa zikikosa makazi ya kuishi ikiwemo nyumba mbili kuangukiwa na kifusi cha mlima.
Akizungumza na Modewji Blog, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma, Joshua Elisha alisema kuwa, tukio hilo lilisababishwa na mvua kubwa iliyonyesha Januari 22 ambapo sehemu mbalimbali mkoani hapa ziliathiriwa na mvua  ikiwemo kuharibika kwa miundombinu ya madaraja pamoja na makazi ya watu.
Alisema kuwa, waliokufa katika tukio hilo ni watu wawili ambao  walijulikana kwa jina moja moja akiwemo Kizigo (45) na Malisela (70) ila awali majina, umri na jinsia zao hazikufahamika.
“Nyumba zilizoanguka ni zaidi ya sita ikiwemo nyumba waliyokuwemo marehemu ambayo ilisombwa na maji na kusababisha vifo vyao,” alisema Elisha.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Kagunga akiwemo Nassoro Mussa ambaye ni mgambo alisema kuwa, mnamo Januari 22, mwaka huu majira ya saa 6:00 usiku mvua kubwa ilianza kunyesha hadi kuamkia Januari 23, ambapo maji yalikuwa mengi na kusababisha mafuriko na kupelekea nyumba tisa kuanguka huku nyumba mbili zilizojengwa karibu na mlima zikiangukiwa na mlima huo.
“Hadi leo tunavyozungumza zaidi ya nyumba tisa zimebomoka na wahanga wanaishi kwa majirani huku mali za wakazi wa kijiji hiki zikipotea baada ya kusombwa na maji zikiwemo  mashine sita za kuchakata  mafuta ya mawese,” alisema Mussa.
Kamanda-wa-Polisi-mkoani-Kigoma-SACP-Ferdinand-Mtui-akizungumzia-tukio-la-mtoto-kubakwa.2
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, SACP Ferdinand Mtui (pichani) alithibitisha kutokea kwa vifo vya watu hao wawili baada ya nyumba waliyokuwemo kusombwa na maji ya mvua.
Aidha kunyesha kwa mvua hiyo kulisababisha miundombinu mkoani hapa kuharibika ikiwemo mradi wa chanzo cha maji kilichokasimiwa na Shirika la UN kwa lengo la kukabiliana na changamoto ya ugonjwa wa kipindupindu katika kata ya Kagunga.
Miundombinu mingine iliyoharibika ni pamoja na madaraja yaliyoko katika mfereji unaopitisha maji kuelekea ziwa Tanganyika katika Manispaa ya Kigoma-Ujiji ambapo serikali ya mkoa ililazimika kufunga barabara ya  Kaya Road ambayo daraja la kwa Jaffer liliathiliwa na mvua hiyo.

CHADEMA WAMKARIBISHA BENARD MEMBE KUJIUNGA NA CHAMA CHAO!!!


Waziri wa zamani wa Mamboya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amekaribishwa kujiunga na Chama Cga Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiwa ni siku chache tangu atoe maoni yake akiikosoa serikali ya Rais John Magufuli.

Mwanasiasa huyo mkongwe amekaribishwa na Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob ambaye alimshawishi kwa kutumia mifano ya wanasiasa wakongwe waliokuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliohamia Chadema na Ukawa kwa ujumla akiwemo Edward Lowassa, Frederick Sumaye na Kingunge Ngombale Mwiru.

Wiki iliyopita Membe alinukuliwa akimkosoa Dk Magufuli katika maeneo kadhaa, likiwamo la kubana matumizi, kudhibiti safari za nje na uteuzi wa Baraza la Mawaziri.

Jana, meya huyo kutoka Chadema alisema watu wanamshangaa Membe na kumshambulia siyo kwa sababu amesema mambo ya ajabu, ila yeye si mtu sahihi wa kutoa kauli hiyo.

“Watu hawashangai alichosema (Membe) kwa sababu siyo hoja ngeni, zimesemwa sana na wapinzani. Wanachoshangaa ni yeye (Membe) kusema hayo. Hafanani na hoja anazoziongea,” alisema.

Jacob ambaye alikuwa diwani katika manispaa hiyo katika Serikali ya Awamu ya Nne alisema, hoja zilizotolewa na Membe ni nzuri na kama zingetolewa na mpinzani zingeonekana zina mashiko zaidi.

"Asiwe vuguvugu, hicho ndicho kinachompa shida. Kama anataka kuja huku asiwe na wasiwasi chama changu kitampokea na hata hayo anayoyaongea yatakuwa na mantiki na watu watamsikiliza kwa sababu ni upinzani,” alisema na kuongeza;
“Avuke moja kwa moja kama walivyofanya akina Kingunge (Ngombale Mwiru), (Edward) Lowassa, na (Frederick) Sumaye kuhamia upinzani.”

Jacob alisema Sumaye na Lowassa ambao waliwahi kuwa mawaziri wakuu na Kingunge aliyekuwa kada mkongwe wa CCM, walikuwa viongozi wa ngazi za juu, lakini walihamia upande wa pili (upinzani) na sasa wanaisimamia na kuikosa Serikali kwa uhuru.

“Asiwe mwoga kwamba ataishi maisha gani, Sumaye na Lowassa wamekuwa mawaziri wakuu wakaondoka na maisha yanaendelea.”

Hata hivyo, Jacob alisema Membe hakupaswa kukosoa sera ya Rais Magufuli ya matumizi na Rais kudhibiti safari za nje, kwa sababu yeye amenufaika nayo.

“Nadhani hakuwa mtu sahihi kusema hayo, alipaswa kwanza kumtafuta mtu mwingine aseme halafu yeye afuate baadaye, lakini kuanza kusema yeye moja kwa moja wakati alikuwa ananufaika na anachopinga Rais, anaonekana anamwonea wivu na mgongano wa masilahi.
“Sasa anapoanza yeye kujibu inashangaza. Kwa sababu yeye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje, iliyokuwa inafanya matumizi makubwa halafu unakosoa unaonekana kabisa unaonyesha kuna mgongano wa masilahi,” alisema na kuongeza:

Jacob alisema kwa mpinzani kusema hivyo angeonekana anataka kumuwajibisha Rais ili hayo mambo yaangaliwe kwa kina zaidi.

Alitoa mfano wa waziri wa zamani, Dk Makongoro Mahanga na kusema alipoikosa Serikali hakushambuliwa kwa sababu alishahama kutoka CCM na sasa yupo upinzani.

“Alipozungumzia suala la matumizi ya ardhi, Serikali haikujibu ilikaa kimya kwa sababu aliyeongea ni mtu sahihi,” alisema na kuongeza.
" Kwanza alikuwa kwenye Baraza la Mawaziri na pili hivi sasa yupo kwenye upande wa kuishambulia na kuikosoa Serikali na kuiwajibisha.”

WIMBO WA ADELE WAVUNJA REKODI YOUTUBE

Wimbo wa Hello ulivuma sana 2015
Wimbo wa mwanamuziki Mwingereza Adele umevunja rekodi nyingine kwa kutazamwa mara bilioni moja haraka zaidi katika YouTube.
Video ya wimbo huo, Hello, imetazamwa mara bilioni moja katika YouTube siku 87 pekee baada ya kupakiwa kwenye mtandao huo.
Wimbo huo umeupita wimbo wa Psy kwa jina Gangnam Style ambao ulitazamwa mara bilioni moja siku 158 baada ya kupakiwa. Wimbo huo ulichomolewa studioni Julai 2012.
Albamu ya tatu ya Adele, kwa jina 25, ndiyo iliyokuwa maarufu zaidi mwaka 2015 licha ya hali kwamba ilichomolewa studioni Novemba.
YouTube wanasema ni video 17 pekee ambazo zimetazamwa mara bilioni moja kwa sasa.
Video hizo ni pamoja na Sugar wa Maroon 5, Lean On wa Major Lazer, Love The Way You Lie wa Eminem, Party Rock wa LMFAO, Counting Stars wa OneRepublic, na Chandelier wa Sia.
Albamu ya 25, yenye wimbo Hello, ilitolewa mwezi Novemba
Wimbo Baby wa Justin Bieber ulichukua miaka minne kutazamwa mara bilioni moja kwenye YouTube.
Kwa nyimbo zilizotolewa mwaka 2013, wimbo uliofikia rekodi ya kutazamwa mara bilioni moja upesi ulikuwa Roar wa Katy Perry uliochukua siku 487.

Mwaka 2014, wimbo wa Taylor Swift kwa jina Blank Space ulitumia siku 238.
#BBC Swahili

DIAMOND PLATINUMZ AFUNGUKA KUHUSU WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO MHE. NAPE NNAUYE..!

Diamond Platnumz amesema akiachana na muziki anataka kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuweka vitu sawa na kutoa fursa zaidi kwa vijana. Akizungumza katika kipindi cha Papaso cha TBC FM, Diamond alisema kama akiingia kwenye siasa basi nia yake ni kuwa Waziri wa Michezo.
“Kwa sasa hivi siasa bado ila nikiingia kwenye siasa baadaye akimaliza mheshimiwa Nape nachukua mimi kile cheo cha Waziri wa Michezo,”alisema na kuongeza
“Kile nakiweza kabisa kwa sababu mimi ukinimbia sijui kuhusu mpira, movie mimi naweza kabisa nikiwa Waziri, nikavifanya na vikawa na maendeleo. 

"Ni kitu ambacho naweza siyo nasema nataka kuwa mbunge ila mimi nataka ile siku nimeacha kufanya muziki naingia kwenye siasa basi nakuwa Waziri  wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuboresha vitu”

Diamond ambaye hakuweka wazi kwamba ataingia kwenye siasa kupitia chama gani, mwaka jana katika kampeni za uchaguzi mkuu uliomuingiza rais Magufuli madarakani, alishiriki kikamilifu kwenye kampeni za CCM na kutengeneza wimbo pamoja na video.

WAZAZI MKOANI MWANZA WASIKITIKA NA ELIMU BURE KUWABAGUA WANAFUNZI WA ELIMU YA WATU WAZIMA.

Wazazi na Walezi wa Wanafunzi wanaosoma kitengo cha elimu ya Watu Wazima katika Shule ya Sekondari Pasiansi iliyopo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, wameiomba Serikali kuondoa ada kwa wanafunzi hao ili nao waweze kunufaika na mpango wa elimu bure nchini.

Wazazi hao wametoa ombi hilo hii leo baada ya kumalizika 

kwa kikao baina yao na uongozi wa Shule hiyo pamoja na 

Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza, 

sanjari na viongozi wengine akiwemo diwani wa Kata ya Pasiansi pamoja na Afisa elimu Sekondani katika Manispaa ya Ilemela.

Malalamiko yao yanafafanua kwamba, hawakuambiwa tangu  awali kuwa watoto wao wanasoma elimu ya Watu Wazima, malalamiko ambayo hata hiyo yamekanushwa na Mkuu wa  Shule hiyo Mwalimu Joseph Bangirana.

Awali wazazi hao walisema kuwa hawako tayari kulipa ada kwa ajili ya watoto wao wanaosoma katika shule hiyo, jambo  lililomlazimu Malimi Joram ambae ni Mkufunzi Msaidizi 

kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza 

kueleza bayana kwamba, wanafunzi wa Elimu ya Watu 

Wazima hawanufaiki na mpango wa elimu bure nchini kwa 

kuwa Serikali haitoi ruzuku kwa ajili yao.

Ufafanuzi huo ukaungwa mkono na Mwalimu Juma 

Kasandiko ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Manispaa 

ya Ilemela.

Wakati ufafanuzi huo ukitolewa, mmoja wa wanafunzi 
wanaosoma katika shule hiyo ya Pasiansi akasisitiza suala la wao kuondolewa ada ili nao wanufaike na mpango wa elimu bure.

Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima katika shule ya 

Sekondari Pasiansi, kilianzishwa Mwaka 2014 na kuanza kupokea wanafunzi waliomaliza darasa la Saba waliokuwa na ufaulu wa chini ya Wastani wa pinti 100 kwa lengo la kuwapa fursa ya kupata elimu ya Sekondari ambapo mbali na michango mingine, wanafunzi hao wanalipa ada ya Shilingi Laki Moja na Elimu Hamsini kwa mwaka.
Kikao Kikiendelea
Mwalimu Juma Kasandiko ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Manispaa ya Ilemela akitoa ufafanuzi kwa Wazazi juu ya suala la Elimu Bure nchini.
Malimi Joram ambae ni Mkufunzi Msaidizi kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza
Andrea Swai kutoka Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi katika kikao hicho
Mwalimu Joseph Bangirana ambae ni Mkuu wa Shule Pasiansi Sekondari akitoa ufafanuzi katika kikao hicho
Diwani wa Kata ya Pasiansi Mhe.Japhesi Joel Rwehumbiza akitoa ufafanuzi wake. Amewapongeza wazazi kwa kufuatilia masuala ya elimu yanayowahusu
Mdau wa Elimu Mkoani Mwanza, Peter Matonyi akitoa mchango wake juu ya suala la elimu bure kwa wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Mwenyekiti wa Mtaa wa Pasiansi Mkoani Mwanza, Emmanuel Masuka akifafanua jambo
Mmoja wa Wazazi akiwasilisha malalamiko yake juu ya suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Mmoja wa Wazazi akiwasilisha malalamiko yake juu ya suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Wanalalamikia suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Elimu bure inawabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Elimu bure inawabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Kutoka Pasiansi Sekondari Jijini Mwanza, Mimi ni Mzee wa Karanga fotoooooooo, GB Pazzo wa Binagi Media Group

IDRIS SULTAN AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA KUHUSU MIMBA YA WEMA SEPETU..ATAJA MIMBA INA MIEZI MINGAPI!!! *AUDIO*

Wema na Idriss
Kumekuwa na headline nyingi zikiandikwa kuhusu mastaa wa bongo Idris Sultan na Wema Sepetu na hii ni kuhusu mapenzi yao, hapa nakukutanisha na Idris akifunguka yote makubwa usiyoyajua kuhusu mapenzi yao.

Sunday, January 17, 2016

ALSHABAAB: ''TUNAWAZUILIA MATEKA WA KENYA''

wapiganaji wa Alshabaab
Kundi la wapiganji wa Alshabaab limesema kuwa linazuia kile linachokitaja ni wafungwa wa vita kutoka Kenya kufuatia shambulio lao katika kambi ya kijeshi kusini mwa Somalia.
Alshabaab ambao waliivamia kambi hiyo wamesema kuwa wanajeshi 100 wanaohudumu katika muungano wa Afrika waliuawa.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema siku ya ijumaa kwamba baadhi ya wanajeshi wa Kenya waliuawa lakini hakutoa idadi yao.
Al Shabaab wamesema kuwa ni mara ya kwanza kwa kikosi chake cha Saleh Ali Saleh Nabhan kutekeleza shambulio ndani ya Somalia.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Mashambulizi yake mengine yamekuwa nchini Uganda na Kenya.

Saleh Ali Saleh Nabhan alikuwa kiongozi wa kundi la al Qaeda katika eneo la Afrika mashariki ambaye aliuawa katika shambulio la Marekani nchini Somalia mwaka 2009.
#BBC Swahili

ZILIZOSOMWA ZAIDI