NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Wednesday, September 30, 2015

CCM WAITUHUMU UKAWA KUMWAGIA MIKOJO OFISI ZAO TANGA!!!

Chama cha Mapinduzi kinasikitishwa na kitendo cha wafuasi wa vyama vinavyounda UKAWA kupiga mawe na kutupa chupa, baadhi zikiwa na mikojo, kwenye Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga jana, tarehe 28 Septemba 2015, kabla na baada ya mkutano wao wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tangamano, Tanga Mjini.
Kama ilivyo kawaida yetu miaka yote, CCM iliazimia kufanya kampeni za amani, zinazoheshimu sheria za nchi na utu wa wapinzani wetu. Hadi sasa, tumeweza kuwadhibiti wapenzi, washabiki na wanachama wa CCM wasifanye vitendo vya ufunjifu wa amani.
Tukio la Tanga sio la kwanza. Tarehe 27 Septemba 2015 viongozi wa UKAWA waliwapanga vijana, katika eneo la stendi ya Uyole, mkoani Mbeya ili wasimamishe msafara wa Mgombea wa Urais wa CCM na kumfanyia vurugu na kumpigia kelele ili wananchi wasimsikie vizuri.
  
Ingawa Mgombea wetu alifanikiwa kukabiliana na hali hiyo, tunaamini kwamba huu sio ustaarabu. Washabiki wa CCM pia wana uwezo wa kupanga na kufanya mambo haya, tena kwa ufanisi mkubwa zaidi. 

Lakini viongozi wa CCM wa ngazi zote wamekuwa wanawahimiza wasifanye mambo haya kwasababu CCM hatuamini kwamba hiyo ni njia sahihi ya kuomba ridhaa ya Watanzania kuliongoza taifa letu na pia, kwa kuwa sisi ndio tuliokabidhiwa na Watanzania nchi hii kuiongoza, tunafahamu dhamana yetu kubwa ya uongozi wa taifa na ulinzi wa amani ya Taifa letu.

Tunawasihi wenzetu wa UKAWA kwamba, katika kipindi hiki cha kampeni kilichobaki, tufanye kampeni kwa amani ili tumalize uchaguzi kwa amani na taifa liendelee kuwa na amani baada ya uchaguzi.
Wenzetu wa UKAWA wasitufikishe mahala ambapo washabiki wa CCM watashindwa kuvumilia kuona Chama chao na viongozi wao wanadhalilishwa.
Tukio la Tanga la Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga kupigwa mawe limewaudhi na kuwakera wana-CCM na wapenda amani wote wa Tanga.
Hata hivyo, tumewasihi wana-CCM wasilipize kisasi. Chama chetu kina dhamana ya uongozi wa nchi na ulinzi wa amani ya nchi yetu. Wenzetu dhamana hiyo hawana. 
  
Chama chetu kina uhakika wa kushinda na kushika dola, wenzetu wana uhakika wa kushindwa na wamekwishakata tamaa.

Tunawapongeza wana-CCM kote nchini kwa utulivu waliouonyesha katika kipindi chote cha kampeni.
Tunawashukuru kwa kubaini na kutoyumbishwa na propaganda za wenzetu ikiwemo ya Tanga, kwamba mkutano wa Tanga uliahirishwa kwasababu watu walikuwa wengi. 

Itakuwa ni mara ya kwanza katika historia kwamba mkutano wa kampeni unaahirishwa kwasababu ya wingi wa watu. Katika mikutano ya kampeni, ikiwemo ya CCM, na hata katika sherehe za kitaifa, baadhi ya watu huzidiwa nguvu na huhudumiwa na wahudumu wa huduma ya kwanza huku mikutano ikiendelea.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa wenzetu kutafuta kisingizio cha kutofanya mikutano ya kampeni. Mkutano wa kampeni ya UKAWA wa Geita pia waliuahirisha kwa kisingizio tofauti, kwamba jukwaa na vipaza sauti havikuandaliwa ingawa aliyetangaza kuahirisha alisimama jukwaani na akasikika na watu wote. 

Mabadiliko wanayoyahubiri wenzetu yanaanza na kusema ukweli. Imefika mahali sasa wenzetu wa UKAWA wawaeleze ukweli Watanzania kuhusu mgombea wao kushindwa kuhutubia baadhi ya mikutano au kuhutubia kwa dakika 3 kuliko kuwahadaa kwa kutengeneza matukio na vioja ili kuficha mapungufu ya mgombea wao.

Tunarudia kuwataka viongozi wa UKAWA kuacha kupanga vurugu, kuharibu mali za CCM, na kutukana wana-CCM. Tunarudia kuwataka waache kauli zao za kuibiwa kura. 
  
Kauli hizo ni za kukata tamaa na kuwandaa watu kufanya fujo. Tunadi sera zetu na wagombea wetu kwa amani ili tuwape Watanzania fursa ya kuchagua kwa amani ili taifa liendelee kuwa la amani, umoja, utulivu na mshikamano mara baada ya uchaguzi.

Imetolewa na:
January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
29.09.2015

RAY C AREJESHA KIUNO CHAKE KISICHO NA MFUPA? *PICHAZ*


Huenda jitihada za Ray C kukirejesha kiuno chake kisichokuwa na mfupa zimeanza kuzaa matunda!

Kwa muda mrefu muimbaji huyo amekuwa akijaribu kuupunguza unene wake uliompoteza muonekano wake wa zamani uliompa sifa jukwaani na sasa picha zake mpya zinaonesha mafanikio.

Muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Rehema Chalamila, ameshare picha zake mpya kuonesha hatua aliyofikia.

Haka ni kanani???yaani sitaki kuamini haka katoto ni mimi uwiii !jamani nina furaha sana moyoni kumuona ray c.wa miaka ile yaani acha tu!je nipungue zaid au?sasa ndio muda wa kurudi rasmi kwenye muziki Babutale, Mkubwafela dada yenu niko tayari sasa,” ameandika.

Unamuonaje Ray C huyu mpya?

HIZI NDIO SAFARI NDEFU ZAIDI ZA NDEGE DUNIANI, UNAKAA MPAKA SAA 17 ANGANI..! *PICHAZ*

Unaweza ukaona safari ya kutoka Mwanza mpaka Dar es Salaam ni ndefu kwa sababu unatumia kati ya saa 12 mpaka 16 ndani ya basi, lakini kwa Usafiri wa Ndege ni kama saa moja tu hivi unakuwa umemaliza safari !!
Sasa hizo saa za kukaa kwenye basi safari ya Mwanza-Dar kuna watu wanazitumia wakiwa angani kwenye Ndege… Nimezipata Rekodi Mitandaoni, zinaonesha safari kumi za Ndege ambazo wasafiri wanatumia muda mwingi zaidi hewani kwenye safari moja.
1.Dubai Mpaka Panama– Hii ni Safari ambayo inachukua saa 17 na dakika 35 angani… yani Ndege ikiruka Dubai hakuna sehemu inatua mpaka ifike Panama. Hii ndio safari ndefu zaidi kwa sasa ambayo inafanywa na Ndege za Emirates… umbali toka Dubai mpaka Panama ni Kilometa 13, 820.
emirates (1)
2. Dallas mpaka Sydney- Unaambiwa umbali toka Dallas Marekani mpaka Sydney Australia ni Kilometa 13,804. Hiyo ni safari ambayo inachukua saa 17 kwa Ndege za Qantas.
3. Atlanta mpaka Johannesburg– Hapo kuna umbali wa Kilometa 13,580.. safari hii inakamilika kwa Ndege za Shirika la Delta kukaa angani kwa saa 16 na Dakika 55 ambazo ni kama saa 17 hivi mwanzo mpaka mwisho wa safari.
60966325
4. Los Angeles mpaka Dubai– Kama kuna wakati unawaza kufanya safari kati ya hayo Majiji mawili, basi utambue kabisa kwamba umbali wake ni Kilometa 13,420.. na Ndege inatumia saa 16 na Dakika 30. Hii sio safari fupi hata kidogo mtu wangu !!
5. Los Angeles mpaka Jeddah– Shirika la Ndege la Saudi Arabia ndio ambao wamekamata hii njia, unaambiwa umbali toka Los Angeles Marekani mpaka Jeddah Saudi Arabia inakuchukua saa 17 pia kuimaliza hiyo safari yenye umbali wa Kilometa 13,409.
Picha ya muonekano wa juu wa Jeddah Airport mpya, Saudi Arabia.
Picha ya muonekano wa juu wa Jeddah
Airport mpya, Saudi Arabia.
6. Los Angeles mpaka Abu Dhabi– Umbali kati ya hiyo Miji miwili ni Kilometa 13,500.. sio safari ndogo aisee, Ndege za Etihad zinakamilisha hiyo safari kwa saa 16 na Dakika 50 mwanzo mwisho.
7. Houston mpaka Dubai– Kilometa 13,145 zimetajwa kwamba ndio umbali kati ya Miji hiyo miwili, safari yake mwanzo mpaka mwisho kwa Ndege inachukua muda wa saa 16 na Dakika 10… Ndege za Emirateszinahusika pia kusafirisha watu kati ya Miji hii miwili.
8. San Francisco mpaka Abu Dhabi– Umbali kati ya hiyo Miji ni Kilometa 13,130.. na safari yake inachukua saa 16 kukamilika.
9. Dallas mpaka Hong Kong– Hapo unazungumzia Marekani na China, umbali wake ni Kilometa 13,700 na umbali huo kwa safari ya Ndege inachukua saa 16 na Dakika 15… Ndege za American Airlineszimeunganisha hii Miji miwili kwa Ndege za moja kwa moja.
American_Airlines_Boeing_777-200ER_N775AN_PVG_2013-5-21
10. San Francisco mpaka Dubai– Hii nayo imo kwenye list ya safari ndefu za Ndege, umbali wake ni Kilometa 13,040… Ndege za Emirates zimeunganisha hii Miji pia kwa safari ya Ndege ya moja kwa moja. Safari yote inakamilika ndani ya saa 16 na Dakika 40.

Sunday, September 27, 2015

BULAYA: ''SASA NIMEMDHIBITI WASSIRA''

MGOMBEA ubunge anayewakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) jimbo la Bunda mjini, mkoani Mara, Esther Bulaya anajivuna kuwa amefanikiwa kumdhibiti mpinzani wake mkubwa katika uchaguzi mkuu, Stephen Wassira.

Akizungumza na MwanahalisiOnline, Bulaya ambaye alikuwa mbunge wa Viti Maalum akitokea Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), amesema kwamba amedhoofisha ngome ya Wassira, ambaye amekuwa kiongozi serikalini tangu awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere.

“Kulikuwa na matukio ya mikutano yetu kuvamiwa, wafuasi wetu kuvamiwa na kubambikiziwa kesi, hata hivyo tulijipanga na kudhibiti huku tukishirikiana na Jeshi la Polisi,” anasema akizungumzia mikakati iliyopangwa kumkwamisha kukubalika kwa wananchi.

“Ninavyoongea na wewe gari yangu ipo Polisi kwa madai kuwa imehusika na uhalifu wa kutumia silaha, dereva wangu pia anashikiliwa lakini wananchi kwa hasira wamenipatia gari sita za kampeni,” anasema Bulaya aliyejiunga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kuhama CCM mara tu bunge lilipovunjwa.

Bulaya ambaye pia kitaaluma ni mwandishi wa habari, amesema mpaka jana ameshafanya kampeni katika Kata 14 za jimbo hilo huku akipita kila kijiji na kila kitongoji na sasa anatarajia kuanza awamu ya pili ya kampeni akiwa ameimarika zaidi.

Kuhusu upinzani anaokumbana nao kutoka kwa Wassira, Bulaya anasema “pamoja na mbinu chafu dhidi yangu nipo imara sana, ninamkabili kisawasawa na anakosa watu kwenye mikutano mingi.”


Jimbo la Bunda mjini ni moja ya majimbo yenye upinzani mkali likishikiliwa na Wassira ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano), aliyewahi kuwa NCCR-Mageuzi na kushinda ubunge kabla ya kuvuliwa na Mahakama Kuu kwa kosa la kununua kura. Alikuwa ameshindana na Joseph Warioba wa CCM.
#MwanahalisiOnline

MAGUFULI AZOMEWA JIJINI MBEYA.....WANANCHI WASEMA WANAMTAKA LOWASSA. *VIDEOZ*

Katika  hali  isiyo  ya  kawaida,Mgombea  Urais  kwa  tiketi  ya  CCM, Dr. John Magufuli  leo  alijikuta  katika  wakati  mgumu  baada  ya  kukutana  na zomea zomea  ya  kundi  la  vijana  waliovamia  msafara  wake  akiwa  njianI  kuelekea  Mbarali  na kuanza  kuimba wakidai  Lowassa  ndo  Rais  wao....Tazama  Video hii

Pamoja  na  kadhia  hiyo,Magufuli  alifanikiwa kufika  Mbarali  na  kuhutubia  maelfu  ya  wananchi  ambao  amewaahidi  kushughulikia  migogoro  yao  ya  muda  mrefu  ambayo  imekuwa  kete  ya  kuombea  kura  kwa  baadhi  ya  wanasiasa  wenye  uchu  wa  madaraka. Tazama Na Hii

Dr. Magufuli  leo  pia  amefanya  mikutano  kadhaa  ya  kampeni  mkoani  Iringa  ambako  alilazimika  kumalizia  viporo  hivyo vilivyokuwa  vimebaki  mkoani  humo. 
Wananchi kwa maelfu wakimsikiliza Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia huko Makambako mkoani Iringa ambako alipita leo kumalizia viporo vya mkoa huo kwenye kampeni zake.

Wagombea wa nafasi mbalimbali wa Mafinga wali-Magufulika mbele ya Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli katika jimbo la Mafinga mkoani Iringa ambako alipita leo kumalizia viporo vya mkoa huo kwenye kampeni zake.
Mgombe ubunge jimbo la Mafinga Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Cosato Chumi, aki-Magufuli-ka
Mgombea Ubunge Jimbo la Mufindi Kaskazini, Mahamudu Mgimwa akidhihirisha kuwa yupo fiti.

MKUTANO WA KAMPENI ZA CCM MKOKOTONI LEO



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akizungumza na WanaCCM na Wananchi na Wapenda amani katika Wilaya ya Kaskazini A Jimbo la Tumbatu katika Uwanja wa Sunrize Mkokotoni Mkoa wa kaskazini Unguja leo jioni,
#Picha na Ikulu.

MAALIM SEIF ASIKITISHWA NA AJIRA ZA WATOTO WILAYA YA MICHEWENI *PICHAZ*

 Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia watoto wanaovyojihusisha na kazi ya uvunjaji wa kokoto katika Wilaya ya Micheweni, alipotembelea kikundi kinachojihusisha na kazi hiyo.
 Baadhi ya watoto wakijihusisha na kazi ya uvunjaji wa kokoto katika Wilaya ya Micheweni.
 Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia kazi ya useremala inayofanywa na wananchi wa kijiji cha Wingwi na maeneo mengine ya Wilaya ya Micheweni.

 Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akipandisha bendera ya chama hicho katika tawi jipya la CUF katika kijiji cha Kwale Micheweni, kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi hilo.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akipandisha bendera ya chama hicho katika tawi jipya la CUF katika kijiji cha Kwale Micheweni, kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi hilo. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Na: Hassan Hamad, OMKR
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameelezea kusikitishwa na ajira za watoto zinazoendelea katika Wilaya ya Micheweni.

Amesema ajira hizo hazifai na zinapaswa kupigwa vita kwa kulinda afya na ustawi wa watoto nchini.

Maalim Seif  ameeleza hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea vikundi vya ujasiriamali katika Wilaya ya Micheweni ambapo amejionea shughuli mbali mbali zinazofanywa na wananchi wa Wilaya hiyo zikiwemo useremala, uvuvi, uchuuzi na uvunjaji wa kokoto.

Amesema watoto wengi katika wilaya hiyo wamekuwa wakijihusisha na uvunjaji wa kokoto pamoja na uvuvi na uparaji wa samaki, mambo ambayo yanakwenda kinyume na mikataba ya kimataifa.

Maalim Seif ambaye pia ni mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi CUF, amesema watoto wengi wanalazimika kujiingiza katika ajira hizo kutokana na uwezo mdogo wa wazazi wao, na kwamba iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar atabadilisha maisha ya wananchi hao kwa kuweka mazingira ya kupata ajira zinazokubalika na zenye heshima.

Amesema serikali atakayoiongoza itaanzisha benki ya wajasiriamali, ili kutoa mikopo kwa wananchi kuweza kuongeza mitaji yao na kuendeleza vipaji vya wajasiriamali.

Amewashauri wajasiriamali wanaojihusisha na kazi ya useremala kuungana na kuunganisha nguvu zao ili waweze kuzifuata au kuagizia malighafi katika mikoa ya Tanzania bara, ili kuepusha ukataji miti ovyo katika visiwa vya Zanzibar, ambavyo vinakabiliwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayotokana na uchaguzi wa mazingira.

Katika risala ya wavunja kokoto iliyosomwa na ndugu Abdalla Omar Ali, wameomba kupatiwa mitaji na vitendea kazi vya kisasa ili kuondokana na usumbufu unaowakabili.

Nao wajasiriamali wa useremala wamesema wanakabiliwa na upungufu wa utaalamu, zana duni za kufanyia kazi, uchache wa malighafi pamoja na soko la kuuzia bidhaa zao, na kuomba kutafutiwa ufumbuzi wa matatizo hayo.

Hata hivo wamesema wamenufaika na kazi wanazozifanya ambazo zimeweza kuajiri zaidi ya watu mia tatu na kufanya zaidi ya watu elfu tatu kunufaika na ajira hizo.

Wakati huo Maalim Seif ambaye pia Katibu Mkuu wa CUF na mgombea urais wa Zanzibar, amefungua tawi la CUF katika kijiji cha Kwale Micheweni, na kuwataka wananchi kuacha kulumbana na tofauti za kisiasa.

Amesema Wazanzibari wanapaswa kuungana kutokana na Uzanzibari wao, na kuachana kulumbana kwa mambo ambayo hayatowaletea tija isipokuwa kuvuruga umoja na maridhiano ambayo yaliasisiwa kwa nia njema.

ITAZAME NA UIPAKUE VIDEO MPYA YA DAVIDO - DODO


MBASHA NA SIMULIZI YA KUTAKA KUJINYONGA

Brighton Masalu
KUMBUKUMBU ya kusikitisha! Siku chache baada ya kushinda kesi ya ubakaji wa shemejiye, Emmanuel Mbasha ameibuka na kusimulia jinsi alivyonusurika kujitoa uhai wakati kesi hiyo ilipokuwa ikiunguruma, Risasi Jumamosi linaandika.
Emmanuel Mbasha. 
‘Akimnong’oneza’ mwandishi wetu kwa njia ya simu Jumatano ya wiki iliyopita katika mahojiano maalum, Mbasha alisema kesi hiyo ilikuwa ikimuumiza moyo na kujiona hana thamani ya kuendelea kuishi hivyo njia bora ya kuepukana na kadhia hiyo ni kujitoa uhai.
Mbasha, ambaye alikuwa mume wa mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha alisema kitendo cha jamii kuaminishwa kuwa alitenda unyama huo, akiangalia heshima aliyonayo ikiwemo kueneza Injili kwa njia ya uimbaji, ilikuwa ni aibu mbaya ambayo kwa ujasiri wa kibinadamu haikuwa rahisi kukabiliana nayo.
Katika mazungumzo na mwandishi wetu, alisema mara nyingi watu wa karibu naye wakiwemo wazee wenye busara walishtukia njama zake za kutaka kujiua na kuamua kuwa naye karibu huku wakimpa nasaha za kumfariji na kwamba Mungu alikuwa akimpitisha kwenye jaribu hilo kwa makusudi maalum.
“Yaani wewe acha tu kaka, hakika nilitaka kujiua kabisa, ni bora ningesingiziwa mambo mengine na si kubaka, nikiangalia heshima yangu kwenye jamii, nikifikiria maisha ya jela tena kwa kosa la kusingiziwa, kwa kweli sikuona kabisa thamani yangu duniani,” alisema Mbasha.
TUJIKUMBUSHE
Mbasha alikuwa akikabiliwa na mashtaka mawili ya kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17, kinyume cha sheria.Katika shitaka la kwanza, Mbasha alidaiwa kuwa Mei 23, 2014 alimbaka shemeji yake katika eneo la Tabata Kimanga huku katika kosa la pili la kesi hiyo, akidaiwa kufanya kosa hilohilo kwa mtu huyohuyo ndani ya gari.

Hukumu iliyomuacha huru ilitolewa Jumatatu ya wiki hii katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ilala, ambapo hakimu Flora Mujaya alisema kwa mujibu wa sheria juu ya madai hayo, Mbasha hakuwa na hatia.

CRISTIANO RONALDO ANAISUBIRI REKODI HII KWA TABASAMU, KAMA AKIFANIKIWA KUFANYA HIVI

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldoambaye ni baba wa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Cristiano Ronaldo Junior, September 25 amepiga picha nakuiweka katika account yake ya Instagram huku akiwa na tabasamu la furaha linalotafsiriwa kuwa ni furaha yake ya kukaribia kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa Real Madrid wa muda wote.2CBEFBE300000578-0-image-a-39_1443175044026
moja kati ya picha zake alizopost Ijumaa katika account yake ya Instagram
Cristiano Ronaldo anatajwa kuwa, huenda akaingia katika rekodi ya ufungaji bora wa muda wote wa klabu ya Real Madrid endapo atafanikiwa kufunga hat trick katika mchezo wa September 26 dhidi ya Malaga katika uwanja wao wa nyumbani Santiago Bernabeu. Rekodi ya ufungaji wa muda wote kwa sasa inashikiliwa na Raul  ambaye ana magoli 323.
2CB10F9A00000578-3248839-Ronaldo_did_not_score_as_Real_Madrid_secured_a_hard_fought_2_1_a-a-55_1443177400612
Uwezekano wa Cristiano Ronaldo kuvunja rekodi hiyo Jumamosi ya September 26 upo licha ya kuwa hadi sasa amefunga goli nane katika mashindano yote kwa msimu huu ila bado hajafunga goli lolote katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu msimu huu. Ronaldo alifunga goli tano katika mechi ya Laliga dhidi ya Espanyol na alifunga hat trick katika mechi ya UEFA dhidi ya Shakhtar Donetsk.

MO AMPIKU DANGOTE MFANYABISHARA BORA AFRIKA

MO dewji
Vinara wa biashara Afrika walipewa tuzo mbalimbali za African Business katika picha ya pamoja. Kuanzia kushoto ni Daphne Mashile Nkosi, Strive Masiyiwa, Helen Hai na Mohammed Dewji . hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika hoteli ya Four Seasons Hotel mjini New York.(Picha na African Business).
Na Mwandishi wetu, New York
MTANZANIA Bilionea Mohamed Dewji amepata tuzo ya Mfanyabiashara Bora wa Afrika wa mwaka 2015, katika kinyang’anyiro cha tuzo za wafanyabiashara bora wa Afrika (African Business Awards 2015).
Dewji maarufu kama Mo alikabidhiwa tuzo hizo usiku wa kuamkia jana mjini New York.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Four Season mkabala na jengo la Umoja wa Mataifa (Baraza Kuu) watu wengine waliopata tuzo ni Aliko Dangote, Daphne Mashile Nkosi, Strive Masiyiwa na Helen Hai.
MO alimshinda Aliko Dangote ambao walikuwa kwenye Kategori moja wakiwania tuzo hiyo ya mfanyabiashara bora wa Afrika, huku wengine walioshindanishwa kwenye kategori hiyo ni CEO wa Paramount Group, Ivor Ichikowitz, CEO wa Groupe Loukil, Groupe UADH, Bassem Loukil, na Oscar Onyema DG wa Nigerian Stock Exchange.
Tuzo hizo zimeandaliwa na jarida la African Business .
Pia katika tuzo hizo taasisi kadhaa zinazofanya vyema bara la Afrika zilitambulika. Taasisi hizo ni pamoja na kiwanda cha sementi cha Dangote , Guaranty Trust Bank, Abellon Clean Energy, Nigerian Stock Exchange na taasisi ya bima kwa masoko yanayochipukia ya BIMA.
Akielezwa wasifu wake katika hafla hiyo, Mo ameelezwa kama mfanyabiashara aliyefanikiwa kutokana na kuongeza kipato na ukubwa wa kampuni ya Mohammed Enterprise toka aitwae kutoka kwa baba yake.
Akiwa mtendaji wa kampuni hiyo, akiwa katika miaka ya 40 amefanya mabadiliko makubwa katika makampuni mbalimbali ya umma yaliyoshindwa kujiendesha katika sekta ya kilimo, viwanda na maeneo ya makazi na viwanda.
Uongozi wake uliwezesha kampuni hiyo ya MeTL kufanya makubwa kiasi cha kumfanya aingie katika jarida la Forbes la matajiri wa Afrika.
Majaji waliompa tuzo kwa mwaka huu walisema kwamba uongozi wake umewezesha biashara katika kampuni hiyo kuchupa kutoka dola za Marekani milioni 30 hadi bilioni 3.
Akipokea tuzo hizo Dewji alisema kwamba tuzo hiyo ni ishara muhimu kwa waafrika wote na uwakilishi wa uhakika wa vijana katika masuala ya ujasirimali.
DSC_0310
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji.
Tuzo ya Biashara ya Mwaka ilienda kwa kiwanda cha saruji cha Dangote kinachoongozwa na bilionea wa Afrika, Aliko Dangote.
Kiwanda hiki kilichopo Nigeria kimejipanga kusambaza uzalishaji katika nchi nyingine za Afrika, hatua ambayo imeifanya tuzo hiyo kuwa ya kwao.
Akipokea tuzo hiyo Aliko alisema amefurahishwa sana na tuzo hiyo ya thamani kubwa na kwamba imetolewa wakati ambapo kiwanda hicho kinatanua shughuli zake kuhakikisha ukombozi wa uchumi kwa nchi za Afrika unafanyika kwa dhati.
“Tunaamini katika Afrika. Tunaamini kwamba katika kuhakikisha kuna uwekezaji mkubwa wa miundombinu Afrika itaweza kusonga mbele katika uchumi wake”.
Daphne Mashile Nkosi, Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya manganisi ya Kalagadi ya Afrika Kusini alipokea tuzo mwanamke bora katika biashara. Majaji walimpa tuzo hiyo kwa kuwa ameonesha mafanikio makubwa katika sekta ambayo kwa kawaida huendeshwa na wanaume.
Mdada huyo anatambulika kwa kuwezesha kupatikana kwa ajira 30,000 huko Northern Cape, na ni muasisi wa mgodi wa aina yake katika kipindi cha miaka 30.
Mfanyabiashara wa Zimbabwe, mjasiriamali, anayependa kusaidia watu wenye mahitaji Strive Masiyiwa alipata tuzo ya mafanikio katika maisha.
CPoF_XCWcAAyCO6
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akipokea tuzo yake.
Strive ambaye ni mmoja wa waanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji kwa kampuni ya kimataifa ya mawasiliano ya simu Econet Wireless amepewa tuzo hiyo kwa mafanikio yake na pia kwa misaada mingi aliyotoa kwa vijana.
Masiyiwa ametumia utajiri wake kusomesha vijana zaidi ya laki moja wa Afrika katika kipindi cha miaka 20.
“Ni heshima kuu kupata nafasi ya kuthaminiwa na jarida lako, Ni heshima kuwa miongoni mwa marafiki… tafadhali endelezeni kazi hii njema,” alisema akizungumza kwa njia ya video.
Tuzo ya mfanyabiashara wa Mfano imeenda kwa Helen Hai, Mtendaji mkuu wa Made in Africa Initiative.
Tuzo hii kwa kawaida hutolewa kwa mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kuboresha hali ya ufanyaji biashara barani Afrika.
Helen ambaye ana asili ya China amewezesha mabadiliko makubwa katika biashara ya viatu ya Ethiopia baada ya kuanzisha kiwanda cha viatu cha Huajian Oktoba 2011 baada ya kuwa na mkutano na rais wa nchi hiyo Meles Zenawi mwaka huo huo.
Imeelezwa kuwa kiwanda hicho mara baada ya kuanzisha katika kipindi cha miezi sita tu waliweza kuongeza pato la mauzo ya nje ya nchi hiyo kwa mara mbili na katika kipindi cha miaka miwili kiliajiri waethiopia 4000.
Sasa hivi mdada huyo amefungua kiwanda cha nguo nchini Rwanda.
“Sekta binafsi haikuja Afrika kutoa msaada, tumekuja afrika kufanyabiashara. KLakini katika biashara tunatekeleza maelengo ya maendeleo. Nina imani kubwa na Afrika, naamini kupitia simulizi za mafanikio tunashawishi wengine kujiamini kutwaa uongozi na kuliwezesha bara hili kutambua fursa zake,” alisema Helen.
Guaranty Trust Bank, iliwashinda wengine kadhaa waliotajwa na kushinda tuzo ya utawala bora wakati Abellon Clean Energy ilipata tuzio ya ubinifu wakati Nigerian Stock Exchange ilipata tuzo ya urejeshaji kwa jamii faida ikiwa ni huduma bora za jamii. 
Akizungumzia tuzo hizo ambazo ni za sab, Omar Ben Yedder alisema hafla hiyo imwezeshwa na Zenith Bank, GTBank, Agility na Cofina .
Washindi wa 2015
AFRICAN BUSINESS OF THE YEAR 
-Dangote, Nigeria
BUSINESS LEADER OF THE YEAR
-Mohammed Dewji, CEO, Mohammed Enterprise, Tanzania
MOST OUTSTANDING WOMAN IN BUSINESS
-Daphne Mashile Nkosi, Executive Chairperson, Kalagadi Manganese, South Africa
AWARD FOR GOOD CORPORATE GOVERNANCE
-Guaranty Trust Bank, Nigeria
AWARD FOR BEST CORPORATE SOCIAL RESPONSIBILITY
-The Nigerian Stock Exchange, Nigeria
AWARD FOR INNOVATION
-Abellon Clean Energy, Ghana
INSURANCE COMPANY & INITIATIVE OF THE YEAR
-BIMA ( bimamobile.com )
LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD
-Strive Masiyiwa
AFRICAN BUSINESS ICON
-Helen Hai

SOMA RATIBA YA MAZISHI YA MHE. CELINE KOMBANI


MAGUFULI AWATAJA WANACCM WANAOMSALITI HUKU WAKIMSANIFU KUWA WANAMUUNGA MKONO

MGOMBEA Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, jana aligeuka mbogo baada ya kuamua kuwataja hadharani watu wanaohujumu kampeni zake kwa kujifanya mchana wako pamoja na usiku wakigeukia upande wa upinzani.

Akiwahutubia wananchi wa mkoani Shinyanga jana katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kambarage, Dk. Magufuli, alisema kuna mamluki wanaokihujumu chama hicho katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Dk. Magufuli aliwataja hadharani baadhi ya makada hao ambao wamekuwa wakiipigia kampeni CCM mchana na usiku wakiwapigia wapinzani.

 “Kuna baadhi ya wana-CCM wanatujuhumu sana, wengine nawajua hata majina yao bahati nzuri huwa sisemi uongo bali ukweli, kuna huyu Gasper mchana tunakuwa naye CCM lakini usiku anaungana na wapinzani,” alisema.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Dk. Magufuli ilipokelewa kwa mshangao na  baadhi ya wananchi na wanachama waliokusanyika uwanjani hapo, kwa kuwa baadhi ya makada hao walikuwa wameketi jukwaa kuu wakifuatila hotuba yake.

Mwandishi wa habari hizi alimshuhudia meneja kampeni wa mgombea huyo, Abdallah Bulembo, akimfuata Magufuli na kumnong’oneza ghafla Magufuli alibadilisha na kudai msaliti ni Gasper Anthony wala si Gasper Kileo aliyetajwa awali.

Hata hivyo, Magufuli  baada ya kumaliza hotuba yake alimfuata kada huyo na kumkumbatia huku akimtuliza na kuendelea na msafara wake.

Kada huyo aliyetajwa kuwa msaliti anadaiwa awali kuwa mpambe wa mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, anayeungwa mkono na vyama vinavyunda Umoja wa Katiba (Ukawa).

Akizungumza katika mkutano huo wa kampeni, Kileo alisema alimuunga mkono Lowassa akiwa CCM, lakini kwa sasa anamuunga mkono mgombea urais wa chama hicho, Dk. Magufuli na wala kwa kilichotokea hatarajii kukihama chama.

Akiwahutubia mkoani Shinyanga, Magufuli amesema hashangai wananchi kuanza kumwita rais kwasababu hata yeye anajua kuwa ndiye atakayeibuka na ushindi mnono kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.


Alisema wagombea wengine wa nafasi ya urais ni wasindikizaji tu kama walivyo wapambe wa kwenye harusi.

LOWASSA AMNADI MBATIA JIMBONI VUNJO *PICHAZ*

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Vunjo na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mh. James Mbatia, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Himo, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Polisi Himo, Jimbo la Vunjo, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 27, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Himo, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Polisi Himo, Jimbo la Vunjo, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 27, 2015
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Himo, katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye uwanja wa Polisi Himo, Jimbo la Vunjo, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 27, 2015.
Wananchi wa Jimbo la Vunjo, wakishangilia wakati Mgombea Ubunge wao, Mh. James Mbatia, akiwahutubia, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Polisi Himo, Jimbo la Vunjo, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 27, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wakuu wa UKAWA, wakati wakiondoka eneo la Uwanja wa Polisi Himo, kulimofanyika  Mkutano wa Kampeni, leo Septemba 27, 2015.

Saturday, September 26, 2015

YANGA, SIMBA, AZAM ZASHINDA VPL, MATOKEO YOTE HAPA

Vigogo vya ligi kuu ya Tanzania bara Simba,Yanga na Azam vimeibuka na ushindi katika michezo yao ya mzunguko wa pili.

Yanga wakicheza katika uwanja wa Taifa waliwachapa Tanzania Prisons kwa mabao 3-0, huku Simba Sport wakicheza ugenini dhidi ya Mgambo Jkt walichomoza na ushindi wa mabao 2-0.
Azam Fc walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stand United mchezo uliochezwa kwenye dimba la Kambarage Shinyanga.


Matokeo Mengine ya ligi hiyo ni:
Ndanda FC 1-0 Coastal Union (Nangwanda Sijaona, Mtwara)
Mbeya City 3-0 JKT Ruvu (Sokoine, Mbeya)
Majimaji FC 1-0 Kagera Sugar (Majimaji, Songea)
Mwadui FC 2-0 African Sports (Mwadui Complex, Shinyanga)
Toto Africans 1-2 Mtibwa Sugar (CCM Kirumba, Mwanza)

ZILIZOSOMWA ZAIDI