NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Friday, October 30, 2015

LEMBELI AELEZA HATMA YAKE BAADA YA KUSHINDWA, AJIBU TETESI JUU YAKE

Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kahama, James Lembeli ameelezea kinachoendelea katika maisha yake ya kisiasa hasa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka huu akiwa ndani ya chama chake kipya cha Chadema.

Akiongea katika taarifa rasmi kwa wananchi wa jimbo hilo, Lembeli amesema kuwa hivi sasa atajikita zaidi katika shughuli za chama chake pamoja na shughuli alizokuwa akizifanya kabla ya kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Alisema kuwa ataendelea kufanya kazi zake na mashirika ya kimataifa kama mjumbe wa Bodi mbalimbali. Pia, ataendelea kufanya kazi ya kusimamia radio yake (Kahama FM) ambayo amedai kuwa taarifa zilizosambazwa kuwa ameiuza kulipa deni la mkopo aliopewa kuendesha kampeni sio za kweli.

Pia, Lembeli amewashukuru wananchi waliojitokeza kumuunga mkono na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika masuala ya maendeleo na ataendeelea kushirikiana nao kukamilisha miradi mbalimbali aliyokuwa ameanza kuitekeleza kwa juhudi zake binafsi.

Kadhalika, Lembeli amekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa kuwa alikamatwa na jeshi la polisi mara tu baada ya Jumanne Kishimba wa CCM kutangazwa kuwa mshindi.

Kuhusu afya yake, alisema kuwa yeye ni mzima tofauti na habari zinazoendelea kuenea kuwa ni mgonjwa hasa baada ya kupata ajali ya gari na matokeo kutangazwa.

ZARI THE BOSS LADY AFANYA UAMUZI MGUMU KWA MWANAYE TIFFAH

Tiffah akiwa kwenye pozi.
*******
NA HAMIDA HASSAN
Zarinah Hassan a.k.a Mama Tiffah amechukua uamuzi mgumu wa kumvua mwanaye Tiffah ile dawa aliyokuwa amefungwa mkononi ‘hirizi’, hali iliyowafanya watu wengi wabakina vingi viulizo.
Awali, Tiffah alivishwa hirizi hiyosiku chache baada ya kuzaliwa na Diamond akaizungumzia kuwa, ni utamaduni wa kawaida ambao kwa mila za Kibongo siyo tatizo..
KUONA ALIVYOMTOLEA 
Hata hivyo, wakati Diamond akitoa ufafanuzi huo baada ya watu kuibua maneno kuwa ‘hirizi’ hiyo inahusiana na mambo ya kishirikina, 

Zari alidaiwa kutokubaliana na uamuzi huo na ikadaiwa kuwa, alishindwa kugoma ili kutomkwaza mama Diamond ambaye ndiye aliyefanya zoezi hilo.

Baada ya Tiffah kudumu na ‘dawa’ hiyo kwa miezi michache (kitu ambacho si cha kawaida), Zari alipokwenda Sauzi alifanya maamuzi magumu ya kwenda kinyume na utamaduni na mzazi mwenzake na kuamua kuivua ‘hirizi’ hiyo.

Ushahidi wa Zari kufanya hivyo unaonekana kwenye picha za hivi karibuni alizoposti kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo moja inamuonesha Tiffah akiwa kavaa ‘hirizi’ hiyo na nyingine hana.

Kufuatia uamuzi huo, baadhi ya Wabongo walionesha kumshangaa Zari huku wakimponda kuwa alichokifanya siyo sawa.

“Unajua ule ni utamaduni wa bwana wake, alitakiwa auheshimu hata kama kwao mambohayo hayapo.

 Kitendo cha yeye kwenda Sauzina kumvua Tiffah ile dawa ni kuonesha dharau, amemdharau Diamond na mama yake pia, siyo sawa,” alisema shabiki wa Diamond aliyejitambulisha kwa jina la Mariam.

Diamond hakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia uamuzi wa mzazi mwenzake huyo.

MWANAFAMILIA ACHOMA MOTO NYUMBA YAO PEMBA

Nyumba ya familia, inayokaliwa na bibi Siajabu Adam Ali wa kijiji cha Minazini shehia ya Tibirinzi wilaya ya Chake chake Pemba, ambayo ilidaiwa kuchomwa na mdogo wake, Zahara Hamza Adam kutokana na ugomvi wao wa muda mrefu, nyumba hiyo iliteketea kila kitu, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
Sehemu ya ndani ya nyumba ya familia, inayokaliwa na bibi Siajabu Adam Ali na watoto wake wawili, kijiji cha Minazini shehia ya Tibirinzi wilaya ya Chake chake Pemba, ambayo ilidaiwa kuchomwa na mdogo wake Zahara Hamza Adam, kutokana na ugomvi wao wa muda mrefu, nyumba hiyo iliteketea kila kitu.
Baadhi ya vitu vilivokuwemo ndani ya nyumba anayoishi Siajabu Adam Ali, ikiwa ni pamoja na magodoro, mabegi mawili ya nguo, vitanda, baiskeli na vyombo vya matumizi ya ndani, vikiwa vimeteketea, baada ya nyumba hiyo kudaiwa kuchomwa na mmoja wa familia wa nyumba hiyo, Zahara Hamza Adam kwa ugomvi wa kiamilia na sasa anashilikiwa Polisi.
Siajabu Adam Ali akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkasa wa nyumba ya familia anayoishi, baada ya kuchomwa na mdogo wake Zahara Hamaza Adam, usiku wa kuamkia juzi, kutokana na hitilafu zao za kifamilia, na kuiteketeza yote na hakukuwa na mtu aliejieruhiwa.

WASANII BUNGENI WATIMIZE WALIYOAHIDI - STEREO


Msanii Stereo amewataka wasanii waliofanikiwa kuchaguliwa kuingia Bungeni, wakatimize wajibu wao kwa kuyatekeleza yale waliyoyaahidi kipindi cha kampeni, na si kuyapuuzia baada ya ushindi.
Stereo ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, na kueleza kwamba iwapo hawatattekeleza wananchi hawatasita kuacha kuwachagua kipindi kingine.
"Kikubwa ni kwamba wakatimize yale ambayo waliyaahidi, kwa sababu watu wamewapa ridhaa ya kuwaongoza katika majimbo husika, kwa hiyo wito wangu mkubwa sana kwa muheshimiwa mtarajiwa Joseph Haule na Joseph Mbilinyi, wakafanye yale mambo ambayo wameyaahidi watu, kwa sababu vinginevyo utakuwa ni uongo, kama watashindwa kutekeleza kwa makusudi yale ambayo waliwaahidi watu katika majimbo yao, basi nadhani watastahili kabisa kunyimwa kura kwa awamu inayokuja", alisema Stereo.
Pia Stereo amewataka viongozi hapo kutumia juhudi binafsi kutosubiri uamuzi wa serikali kutekeleza baadhi ya mambo ambayo wanahitaji katika majimbo yao, na kutokuwa wabinafsi kwa kutanguliza matakwa yao wenyewe.
"Kimsingi focus, maendeleo ya watu mbele, ustawi wa watu mbele kwanza ndipo wajiangalie wao, ikiwezekana mara nyingine hakuna haja ya kusubiri sana kwamba kuna mfuko wa kitu fulani hapa kutoka serikalini, unaona serikali inachelewa kufanya kitu fulani sehemu fulani na wewe ni mbunge sehemu hiyo na una kinafasi fulani na unaona kuna pesa ipo kwenye akaunti yako toa fanya, usisubiri mpaka serikali ifanye", alimaliza Rapa Stereo.

HISTORIA YA SAMIA SULUHU HASSAN

Image captHistoria ya Samia Suluhu Hassan wa CCM
Lakini Bi Samia ni nani?
Ushindi wa John Pombe Magufuli wa CCM umetoa fursa kwa Bi Samia Suluhu Hassani kuhudumia taifa hilo la Afrika Mashariki kama mwanamke wa kwanza kuwa makamu wa rais wa Tanzania
Tangu kongamano la Chama tawala nchini Tanzania CCM kumteua Daktari John Pombe Magufuli Joseph kuwa mshika bendera wa CCM, Chama hicho kiliweka historia kwa kumteua Bi Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza.
Tangu Dodoma, Bi Samia aliwekwa kwenye ramani ya wanasiasa wanawake waliobobea barani Afrika.
Lakini Bi Samia Suluhu Hassanni Nani ?
Bi Samia Suluhu ana umri wa miaka 54.
Kwa wale wanaomjua Bi Samia wanasema kuwa ni mchache wa maneno.
Asili yake ni Kisiwani Zanzibar.
Bi Samia Suluhu Hassan amewahi kushikilia nyadhifa za uwaziri katika serikali ya Muungano wa Tanzania na kadhalika amewahi kutumikia serikali ya visiwani Zanzibar kama waziri katika afisi ya makamu wa rais.
Ni mwanamke wa Kwanza kuwa Mgombea Mwenza
Image captionBi Samia atakuwa naibu wa John Pombe Magufuli rais wa Jamhuri ya Tanzania
Tangazo la kumtaja kama mgombea mwenza wa rais mteule wa tano wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania sasa limezaa matunda na kumuweka Bi Samia katika mstari wa mbele barani Afrika kama naibu rais wa Jamhuri ya Tanzania.
Chama CCM pia kimeingia katika daftari la vyama vilivyowapa wanawake sauti katika serikali yake katika karne hii ya 21.
Bi Samia alikamilisha masomo ya shule ya upili mwaka wa 1976 .
Masomo
Aliajiriwa kama mchapishaji katika wizara ya mipango na maendeleo ya nchi, kazi ambayo aliifanya huku akiendelea na masomo yake hadi alipohitimu katika chuo kikuu cha Manchester, Uingereza.
Bi Samia anasema kuwa njia yake ya ufanisi haijakuwa rahisi kama inavyodhaniwa.
''Safari yangu katika siasa imekuwa njia ndefu na yenye tija.''
Kimsingi ufanisi wangu katika siasa za Tanzania umetokana na uweledi na umakini katika kila jambo ninalolifanya.''
''Sio rahisi kuwajibikia familia yako wakati huohuo ukiendelea na maisha ya siasa elimu na majukumu mengine ya kikazi," anasema Bi Samia.
Familia
Aliolewa mwaka wa 1978, kwa Bw Hafidh Ameir, ambaye wakati huo alikuwa afisa wa Kilimo .
Walijaliwa watoto wanne.
Mmoja kati ya wanawe Wanu Hafidh Ameir (1982), ni mwakilishi maalum katika bunge la Zanzibar
Image captionBi Samia Suluhu Hassan na rais Mteule John Magufuli
Siasa
Alijiunga na siasa mwaka wa 2000.
Wakati huo alijiunga na bunge la wawakilishi la Zanzibar kama mjumbe maalum.
Haikuchukua muda nyota yake ikaanza kung'aa na akateuliwa kuwa waziri na rais Amani Karume.
Alitumikia taifa hadi mwaka wa 2005 alipochaguliwa tena na kuteuliwa upya kama waziri.
Mwaka wa 2010 alichaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo la Makunduchi.
Punde tu akateuliwa na rais Jakaya Kikwete kuwa waziri wa maswala ya muungano.
#BBC Swahili

DIAMOND PLATINUMZ APOST HIVI BAADA MHE. JOHN POMBE MAGUFULI ALIPOTANGAZWA MSHINDI WA URAIS

Hiki hapa chini ndicho alichopost mtandaoni msanii wa kimataifa Diamond Platinumz

POLISI YAVAMIA KITUO CHA UKUSANYAJI TAARIFA CHA TACCEO NA KUKAMATA MAAFISA 36 PAMOJA NA VIFAA

Mtandao wa Asasi za Kiraia za Kuangalia chaguzi nchini jana ulipata pigo katika mwendelezo wake wa kukusanya taarifa juu ya mchakato wa uchaguzi mkuu wa 2015 kama unavyoendelea nchi nzima baada ya Jeshi la Polisi kuvamia kituo cha kukusanya taarifa kilichopo katika ofisi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ofisi ya Mbezi Beach. Tukio hilo lisilo la kawaida lilitokea Majira ya saa nane mchana baada ya polisi kufika kituoni hapo na kuwaweka wahusika wa kituo hicho wapatao 36 chini ya ulinzi na kuwashinikiza kusimamisha kazi na Kufungua mitambo bila kutoa sababu ya kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC ambao ndio waratibu wa TACCEO Wakili Imelda – Lulu Urio amelaani vikali kitendo cha jeshi la polisi kuvamia na kusimamisha shughuli ambazo zinafanyika kwa mujibu wa sheria na pia zinafanyika kwa kibali kutoka Tume ya Uchaguzi ya Tanzania.”Kitendo hiki ni cha kidhalilishaji ukizingatia sisi( TACCEO)  tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria na pia tuna vibali vya kufuatilia uchaguzi kwa mujibu wa sheria” Kituo chetu kinaaminika kwa kufanya kazi kwa maslahi ya umma wa Tanzania na hii sio mara ya kwanza kwa sisi kufuatilia uchaguzi za nchi hii hivyo tumeshangazwa na kusikitishwa na kitendo hiki cha polisi kuvamia bila taarifa” – Aliongeza.

Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC Wakili Harold Sungusia akizungumza kwa masikitiko katika eneo la tukio alisema “mpaka sasa hatujui kosa kwani tumekuwa tukifuatilia chaguzi mbali mbali toka kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini na tumekuwa tukifuata sheria na taratibu zote zinazopaswa kama waangalizi na hata Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetupa vitambulisho vya uangalizi kwa kutambua mchango na nafasi yetu”.

Hata hivyo sakata hilo bado linaendelea kwani wafanyakazi pamoja na vifaa vyao vya kazi ikiwemo kompyuta 27 pamoja na simu zao za mkononi ambavyo vimeshikiliwa na Jeshi la polisi likiongozwa na afisa mpelelezi wa Kituo cha Polisi cha Kawe aliyefahamika kwa jina la Mgonja. Wafanyakaizi wamefikishwa Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi.

KANYE WEST AGEUKA KITUKO KWA GEORGE BUSH

Siku chache zimepita tangu tangu mwanamuziki na mwanamitindo nchini Marekani, kutangaza nia ya kugombea nafasi ya urais nchini humo, imeonekana kuwa kichekesho kwa baadhi ya watu.
Inadaiwa kuwa Rais wa zamani wa Marekani, George W. Bush, ameangua kicheko kutokana na wazo la rapa Kanye West, kuwania urais wa Marekani mwaka 2020.
Inadaiwa kuwa Bush, alikuwa akitoka kwenye mlo wa usiku Jijini Washington DC, ambapo alisimama kusaini picha kadhaa walizokuwa nazo watu na ndipo mpiga picha mmoja alipomuuliza juu hatma ya kisiasa ya Kanye.
Taarifa zinadai kuwa Rais huyo wa zamani wa Marekani, alionekana kukwepa kujibu swali la mpigapicha huyo na badala yake aliangua kicheko kwa mara mbili.
Sambamba na hilo rais Obama, alimtaka Kanye, kutumia muda mwingi kufanya maamuzi kwa sababu kuna watu wengi ambao wana tabia za ajabu hivyo anapaswa kukabaliana nao ili aweze kumudu nafasi yake.Hata hivyo siku za nyuma rais Obama, alishangazwa na uamuzi wa Kanye West kuwania nafasi hiyo na pia hakuwa na kikubwa cha kumshauri kuhusu uamuzi wake huo.
Pia alimuuliza kama anafikiri tena Wamarekani watampa Mmarekani mweusi nafasi ya kuwaongoza kama ilivyokuwa kwake.

LOUIS VAN GAAL AJIBU MASHAMBULIZI YA PAUL SCHOLES

Louis van Gaal amjibu Paul Scholes
Louis van Gaal amjibu Paul Scholes
Louis van Gaal amejibu mashambulizi kutoka kwa Paul Scholes kwamba Manchester United ni butu, kwa kusema: “Fimbo na mawe zitaumiza mifupa yangu lakini majina hayataniumiza!”
Gwiji wa Old Trafford Scholes amelalamika kuhusu “ukosefu wa kujituma na ubunifu” akidai kwamba asingependa kuchezea kikosi cha United cha sasa ambacho mechi zake mbili za mwisho zilimalizika bila magoli.
Van Gaal amesema atafanya kila awezalo kuipa mafanikio Manchester United
Van Gaal amesema atafanya kila awezalo kuipa mafanikio Manchester United
Van Gaal alisistiza kwamba timu yake huwa inajituma na kuburudisha, na kumshutumu Scholes kwa kutoa maoni kwa sababu analipwa na chombo cha habari.
Man U itavaana Crystal Palace siku ya Jumamosi
Man U itavaana Crystal Palace siku ya Jumamosi
Mholanzi alisema: “Scholes hana majukumu, hivyo anaweza kusema lolote. Kwanini anajisemea lolote? Hii ni kwa ajili ya klabu au kwa manufaa yake mwenyewe?
Paul Scholes amekikosoa kikosi cha Louis van Gaal
Paul Scholes amekikosoa kikosi cha Louis van Gaal
“Siwezi kujitetea mwenyewe kwa sababu siwezi kijitetea, kwa sababu ni gwiji na kwa sababu ana sauti kubwa, naisikia. Nafikiri unapokuwa gwiji, unapaswa kuzungumza na kocha au rafiki yake, Ryan Giggs, au Ed Woodward, lakini sio namna hi, kwa sababu atalipwa na BBC au Sky.
Louis van Gaal akiwa na msaidizi wake Ryan Giggs
Louis van Gaal akiwa na msaidizi wake Ryan Giggs
“Una muonekano wako. Daima natumia muonekano wa Uholanzi, lakini una muonekano mzuri ila fimbo na mawe zinaweza kunivunja mifupa yangu, lakini sio majina ya watu. Muonekano mzuri. Unaelewa maana yake?.
Louis van Gaal amesema hawezi kujitetea kwa maoni aliyotoa Paul Scholes
Louis van Gaal amesema hawezi kujitetea kwa maoni aliyotoa Paul Scholes
“Scholes akitaka niondoke, naondoka. Lakini sio jukumu lake, yeye sio Glazers au Ed Woodward.
“Najua lini tutapoteza kupoteza na kupoteza, nitakwisha, lakini nitafanya kila niwezalo kwenye hii klabu, kama nilivyosema, hii klabu sio ya kawaida.”

CHINA YAFUTA SHERIA YA WANANDOA KUZAA MTOTO MMOJA, *SASA RUKSA WATOTO WAWILI*

CHINA yafuta sheria ya wanandoa kuzaa mtoto mmoja.
Hatimaye China kupitia shirika la habari nchini humo la Xinhua imeamua kufuta sheria iliyodumu kwa miongo mingi iliyokuwa ikizitaka familia za nchi hiyo kutokuzaa mtoto zaidi ya mmoja ‘one-child policy’.
Ambapo kwasasa wanandoa wameruhusiwa kuzaa watoto wawili ili kupunguza athari zinazoletwa na sheria ya mwaka 1979 ikiwa ni pamoja na kuzuia ongezeko la watoto milioni 400 na ongezeko kubwa la idadi ya watu wenye umri mkubwa wanaozidi idadi ya vijana nchini humo.
Hapo awali wanandoa waliokiuka sheria hiyo walipewa adhabu mbalimbali kama kulazimishwa kutoa mimba, kutozwa faini, na kufukuzwa kazi.

MUIGIZAJI MOHAMED MWIKONGI 'FRANK' AFUNGUKA KUKOSA KITI CHA UBUNGE SEGEREA

Msanii wa filamu za kibongo Mohamed Mwikongi ‘Frank’
Baada ya wasanii mbalimbali kujitokea katika kingang’anyiro cha kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu na baadhi yao kufanikiwa kutwaa nafasi hizo na wengine kukosa, Frank afunguka kukosa kwake.
Msanii huyo wa filamu nchini Tanzania, Mohamed Mwikongi ‘Frank’, alijitokeza kugombea Ubunge jimbo la Tabata Segerea, kupitia tiketi ya ACT-Wazalendo lakini kutokana na kura zake kuwa chache hakufanikiwa kuwa mshindi wa jimbo hilo.
Amesema kuwa alikuwa mgombe ubunge jimbo la Segerea kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, ingawaje hakuwa mshindi lakini ana imani wananchi wa Segerea, wamempokea vizuri mshindi Bonnah Kaluwa na kudai kuwa hata yeye amekubali matokeo hayo.
Amedai kuwa bado anaona kuwa ana deni kwa wananchi waliompigia kura kama wawakilishi wa wana Segerea, hivyo kuna baadhi ya mambo yaliyo ndani ya  uwezo wake atayafanya kwa wananchi wake.
Ameongeza kuwa kulikuwa na changamoto nyingi, ingawa anajipanga upya mwaka 2020 kugombea tena Ili kuweza kusaidi matatizo kama tatizo la maji, ujasiriamali, ajira, michezo na Afya

HAWA NDIO WABUNGE WATAKAOTINGA BUNGENI

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wabunge ambao wataingia Bungeni baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini kote Oktoba 25, 2015 ni kama ifuatavyo. 
Idadi kubwa ya wabunge hao ni kutoka chama tawala cha CCM, ikifuatiwa na Chadema na CUF na vyama vingine kama NCCR-Mageuzi na ACT-Wazalendo.

WABUNGE WALIOSHINDA KUPITIA CCM
Jimbo la Busega (Raphael Chegeni),
Nyamagana (Stanslaus Mabula),
Msalala (Ezekiel Maige),
Ngara (Alex Gashaza),
Kigamboni (Faustine Ndugulile),
Kishapu (Suleiman Nchambi) na
Kisarawe (Suleiman Jaffo).

Majimbo mengine ni
Bagamoyo (Dk Shukuru Kawamba),
Ilemela (Angelina Mabula),
Ilala (Mussa Azzan ‘Zungu’),
Singida Mjini (Mussa Sima),
Same Magharibi (Dk Mathayo David Mathayo),
Rungwe (Saul Amon),
Mbogwe (Augustino Masele),
Chalinze (Ridhiwani Kikwete),
Iramba Magharibi (Mwigulu Nchemba) na
Hanang (Dk Mary Nagu).

Aidha, majimbo mengine ni
Njombe Kaskazini (Joram Hongoli),
Dodoma Mjini (Antony Mavunde),
Mtama (Nape Nnauye),
Babati Vijijini (Jitu Soni),
Kahama Mjini (Jumanne Kishimba),
Sikonge (George Kakunda),
Nzega Mjini (Hussein Bashe),
Urambo (Margaret Sitta),
Mpanda Vijijini (Moshi Kakoso) na
Geita Mjini (Constantine Kanyasu).

Chama hicho pia kilijipatia ushindi katika majimbo ya Mbeya Vijijini (Oran Njeza),
Mafinga Mjini (Cosato Chumi),
Kalenga (Godfrey Mgimwa),
Isimani (William Lukuvi),
Songea Mjini (Leonidas Gama),
Mkalama (Allan Kiula),
Newala (George Mkuchika),
Kavuu (Dk Prudenciana Kikwembe) na 
Kwimba (Mansoor Shanif).
Mengine ni Bukoba Vijijini (Jason Rweikiza),
Nyasa (Stella Manyanya),
Kondoa Mjini (Edwin Sanda),
Kondoa Vijijini (Dk Kashatu Kijaji),
Chemba (Juma Nkamia),
Chamwino (Joel Mwaka),
Mtera (Livingstone Lusinde),
Bahi (Omar Baduel),
Mpwapwa (George Lubeleje),
Kibakwe (George Simbachawene) na
Kongwa (Job Ndugai).
CCM pia imepata Sengerema (William Ngeleja),
Maswa Mashariki (Stanslaus Nyongo),
Maswa Magharibi (Mshimba Ndaki),
Itilima (Njalu Silanga),
Bariadi (Andrew Chenge),
Meatu (Salum Hamis),
Muheza (Balozi Adadi Rajabu),
Kasulu Mjini (Daniel Nsanzugwanko),
Buhigwe (Albert Ntabaliba),
Handeni Vijijini (Mboni Mhita) na
Morogoro Mjini (Abdulaziz Abood).
Gairo (Ahmed Shabiby),
Rorya (Lameck Airo),
Ngorongoro (William Ole Nasha),
Mvomero (Suleiman Murad),
Morogoro Kusini Mashariki (Mgumba Omary),
Morogoro Kusini (Prosper Mbena),
Nkasi Kusini (Deuderius Mipata),
Nkasi Kaskazini (Ally Keissy),
Singida Kaskazini (Lazaro Nyalandu),
Singida Magharibi (Elibariki Kingu) na
Igunga (Dk Dalaly Kafumu).
Mengine yaliyoenda CCM ni Solwa (Ahmed Salum),
Katavi (Issac Kamwele),
Mpanda Mjini (Sebastian Kapufi),
Mpanda Vijijini (Moshi Kakoso),
Nsimbo (Richard Mbogo),
Ruangwa (Kassim Majaliwa),
Sumbawanga Mjini (Aeshi Hilaly),
Kyela (Dk Harrison Mwakyembe),
Ileje (Janeth Mbene) na
Mbarali (Pirmohamed Mulla).
Majimbo mengine yaliyochukuliwa na chama hicho ni Busokelo (Atupele Mwakibete),
Vwawa (Japhet Hasunga),
Lupa (Victor Mwambalaswa),
Songwe (Philipo Mulugo),
Madaba (Joseph Mhagama),
Peramiho (Jenista Mhagama),
Kilosa Kati (Mohamed Bawazir),
Kiteto (Emanuel Papian),
Mbulu (Paul Isaay) na
Karagwe (Innocent Bashungwa).
Kyerwa (Innocent Bilakwate), 
Nkenge (Dk Diodorus Kamala),
Muleba Kusini (Profesa Anna Tibaijuka),
Muleba Kaskazini (Charles Mwijage),
Biharamulo Magharibi (Mukasa Oscar),
Mwibara (Kangi Lugola),
Bunda Vijijini (Boniphace Getere),
Makete (Dk Norman Sigala),
Kibaha Vijijini (Hamoud Jumaa) na
Sumve (Richard Ndassa).
Magu (Kiswaga Destery),
Chato (Dk Merdad Kalemani),
Nzega Vijijini (Dk Khamis Kigwangallah),
Njombe Mjini (Edward Mwalongo),
Mwanga (Profesa Jumanne Maghembe),
Nyangh’wale (Hussein Kassu),
Newala Vijijini (Rashid Akbal),
Butiama (Nimrod Mkono),
Korogwe Vijijini (Stephen Ngonyani) na
Korogwe Mjini (Mary Chatanda).
Misungwi (Charles Kitwanga),
Busanda (Lolensia Bukwimba),
Manonga (Seif Gulamali),
Tabora Mjini (Emmanuel Mwakasaka),
Mlalo (Rashid Shangazi),
Kisesa (Luhaga Mpina),
Lindi Mjini (Selemani Kaunje),
Mkinga (Dustan Kitandula),
Mbinga Mjini (Sixtus Mapunda),
Mbinga Vijijini (Martin Msuha) na
Musoma Mjini (Vedastus Mathayo).
Mengine ni Geita Vijijini (Joseph Kasheku),
Kibaha Mjini (Silvestry Koka),
Bukombe (Dotto Biteko),
Shinyanga Mjini (Steven Masele),
Msalala (Ezekiel Maige),
Pangani (Jumaa Aweso),
Mufindi Kaskazini (Mahamoud Mgimwa),
Mufindi Kusini (Mendrad Kigola),
Kilolo (Venance Mwamoto) na
Maswa Mashariki (Stanslaus Nyongo).
Maswa Magharibi (Mashimba Ndaki),
Chilonwa (Joel Mwaka),
Mtwara Vijijini (Hawa Ghasia),
Nanyamba (Abdallah Chikota),
Tunduru Kusini (Daimu Mpakate),
Tunduru Kaskazini (Ramo Makani),
Bunda Vijijini (Boniface Mgetere),
Mkuranga (Abdallah Ulega) na
Mbulu Vijijini (Gregory Massay) nayo yameenda CCM.
Mengine ni Mbulu Mjini (Zacharia Paul),
Kilindi (Kigua Mohamed),
Namtumbo (Edwin Ngonyani),
Ushetu (Elias Kuandikwa),
Bumbuli (January Makamba),
Segerea (Bonnah Kaluwa),
Kalambo (Josephat Kandege),
Wanging’ombe (Gerson Lwenge),
Kigoma Kaskazini (Peter Serukamba),
Muhambwe (Justus Nditiye),
Kasulu Vijijini (Agustie Vuma) na
Kilolo (Venance Mwamoto).

WABUNGE WA CHADEMA
Kwa upande wa CHADEMA, hadi sasa kimejinyakulia majimbo 35 ambayo ni
Kibamba (John Mnyika),
Mikumi (Joseph Haule),
Bukoba Mjini (Wilfred Lwakatare),
Same Mashariki (Nagenjwa Kayoboka),
Rombo (Joseph Selasini),
Bunda Mjini (Ester Bulaya),
Hai (Freeman Mbowe) na
Mbeya Mjini (Joseph Mbilinyi).
Majimbo mengine ni Kawe (Halima James Mdee),
Longido (Onesmo Nangole),
Ukonga (Waitara Mwita),
Mlimba (Suzan Kiwanga),
Singida Mashariki (Tundu Lissu),
Ubungo (Said Kubenea),
Mbozi (Paschal Haonga),
Tunduma (Frank Mwakajoka),
Momba (David Silinde),
Kilombero (Peter Lijualikali) na
Karatu (Willy Qambalo).
Aidha, chama hicho kilishinda katika majimbo ya Simanjiro (James ole Millya),
Arumeru Magharibi (Gipson ole Meseyeki),
Tarime Mjini (Ester Matiko),
Siha (Godwin Mollel),
Buyungu (Kasuku Bilago),
Monduli (Julius Kalanga),
Arumeru Mashariki (Joshua Nassari),
Serengeti (Marwa Ryoba) na
Babati Mjini (Pauline Gekul).
Mengine ni Moshi Mjini (Jaffar Michael),
Tarime Vijijini (John Heche),
Iringa Mjini (Peter Msigwa),
Ndanda (Cecil Mwambe) na
Moshi Vijijini (Anthony Komu).
CUF yenyewe hadi sasa kina majimbo 17 ambayo ni Temeke (Abdallah Mtolea),
Mchinga (Hamidu Bobali),
Kilwa Kusini (Said Bungala),
Kaliua (Magdalena Sakaya),
Tandahimba (Ahmad Katani),
Mtwara Mjini (Maftaha Nachuma),
Kinondoni (Maulid Mtulia),
Kilwa Kaskazini (Vedasto Ngombale) na
Tanga Mjini (Musa Mbaruk).
Majimbo mengine ni Wawi, Chakechake, Ole, Ziwani, Kojani, Gando, Wete na Mgogono.

WABUNGE WENGINE KUPITIA CHADEMA, CUF, ACT WAZALENDO na NCCR MAGEUZI
Hai (Freeman Mbowe),
Vunjo (James Mbatia)
Kigoma Mjini (Zitto Kabwe),
Arumeru Mashariki (Joshua Nassari),
Kawe (Halima Mdee),
Ukonga (Waitara Mwita),
Kibamba (John Mnyika),
Ubungo (Said Kubenea),
Bunda Mjini (Ester Bulaya),
Tunduma (Frank Mwakanjoka),
Siha (Dk Godwin Mollel),
Tarime Vijijini (Esther Matiko),
Same Mashariki (Nagenjwa Kayoboka),
Kaliua (Magdalena Sakaya),
Mlimba (Suzan Kiwanga),
Iringa Mjini (Peter Msigwa).

#HabariLeo Online

ZILIZOSOMWA ZAIDI