Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kufagia na baadhi ya wananchi wakazi wa eneo lake la Oysterbay Karume Raod, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo Dec 9, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuzoa taka
na baadhi ya wananchi wakazi wa eneo lake la Oysterbay- Karume Raod,
wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais
Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii
leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili eneo la
Kituo cha Daladala cha Morocco, kwa ajili ya kuendelea kushiriki na
wananchi wa eneo hilo kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais
Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiingia kukagua eneo
la kuhifadhia Taka lililopo eneo la Kituo cha Daladala cha Morocco,
wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kuendelea kushiriki na wananchi
kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya
Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli,
ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuzoa taka
na baadhi ya wananchi wa eneo Morocco, wakati wa zoezi la kufanya usafi
wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa
Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo
zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Mungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wananchi na wasanii mbalimbali waliojitokeza
kushiriki naye katika zoezi hilo baada ya kuhitimisha zoezi la usafi
eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoka eneo la
Morocco, baada ya kushiriki zoezi hilo na wananchi wa eneo hilo la
kufanya usafi wa mazingira leo.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
leo ameshiriki katika zoezi la kufanya usafi katika maeneo ya Mtaa wa
Oysterbay na Morocco stand katika wilaya ya Kinondoni katika kuadhmisha
miaka 54 ya uhuru wa Tanzania Bara.
Akizungumza
na wananchi waliojumika katika maeneo ya Morroco stand Makamu wa Rais
amewaagiza viongozi wa wilaya za mkoa wa Dar es salaam kutoa taarifa za
wazabuni wa kufanya usafi ili ziweze kufuatiliwa.
“Haya
makampuni yanapewa fedha kwa ajili ya kazi ya kufanya usafi; lakini
inaonyesha hayafanyi kazi ipasavyo kwa sababu mji bado ni mchafu,”
Alisema Mhe. Samia.
Alielezea
kufurahishwa kwake kwa jinsi wananchi walivyojitokeza katika zoezi hilo
ambalo alisema ni endelevu na kuwataka Wakuu wa wilaya na wenyeviti wa
serikali za mitaa kupanga siku maalum kwa ajili ya kufanya usafi katika
maeneo yao.
Makamu wa
Rais alisema Watanzania hawawezi kujivunia miaka 54 ya uhuru ikiwa miji
ni michafu na kuwataka wananchi kushirikiana kutekeleza kauli mbiu ya
uhuru na kazi kwa kila mmoja kufanya kazi bidii mahali alipo aweze
kuongeza tija ambayo italiwezesha Taifa kupata madawa na elimu bora.
Pamoja na
wananchi waliojumuika na Makamu wa Rais kufanya usafi katika Mtaa wa
Oysterbay, kwa upande wa Morocco stand walikuwepo pia wafanyakazi wa
benki ya DTB, Radio ya EFM na wasanii mbalimbali
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment