Thursday, October 30, 2014

GIZA NENE LATAWALA BONGO MOVIE BAADA YA KIFO CHA RAFIKI MKUBWA WA KANUMBA, MZEE MANENTO

RAIS wa shirikisho la wasanii Simon Mwakifwamba amethibitisha kufariki kwa Mzee Manento hapo jana na kusema kuwa msiba wake upo nyumbani kwake Kigogo/Mburahati jijini Dar es Salaam
Bado mtandao wa ULIMWENGU WA HABARI unafuatilia kwa karibu habari hizi na chanzo cha kifo cha mzee wetu huyu.
  Mzee Mnento atakumbukwa hasa kwa filamu alizocheza kiumakini na marehemu Kanumba. 
Hero of the church, Dar to lagos,fake pastor n.k pumzika kwa Amani
Mungu ailaze Roho ya maerehemu mahali pema peponi amina.

EXCLUSIVE HOT PICHAZ ZA WANAOWANIA TAJI LA MISS UNIVERSE 2014 ZIKO HAPA!!!










Wamevalishwa na designer Asia Idarous
Makeup: Ndibs
Picha na Ally Zoeb wa AZH Photography
Good Luck to all the girls.

Monday, October 27, 2014

UMESHAWAHI KUJIULIZA KWANINI MTOTO WAKO HANA AFYA NZURI SOMA HAPA KUJUA WAPI UNAKOSEA NA NINI UFANYE.


 Kiafrika Familia hukamilika pale wanandoa wanapopata mtoto au watoto,na furaha huitawala nyumba.Watoto hupendeza na kua na afya nzuri na wenyefuraha pale wanapokula vizuri wakashiba  na wakapata usingizi wakutosha .Leo nawamulika watoto wenye umri wa mwaka mmoja adi mine(1-4)

 Katika pita pita yangu na kuishi katika jamii yetu ya watanzania,nimegundua kwamba watoto wengi hawakui katika uwiano ulio sahihi,nikimaanisha umri,urefu na uzito haviwi katika uwiano ulio sahihi.wataalamu wa mambo ya afya wanakanuni  zao za kupima uwiano huu.chanzo cha tatizo hili ni Lishe mbaya kwa mtoto na mtoto kukosa usingizi wakutosha.



 Lishe mbaya kwa watoto husababiswa na ukosefu wa Elim na ufaham mzuri wa  vyakula  na lishe bora  wa wazazi,lakini kwa upande mwingine hali ya wazazi kutokujali watoto wao kwa sababu moja au nyingine pia huchangia tatizohili.Mtoto kukosa  usingizi wakutosha au kushindwa kulala vizuri pia huchangiwa sana na njaa,mtoto asiposhiba vizuri hawezi kulala vizuri.Kelele,kumchelewesha mtoto kulala na kukosa ratiba ya mtoto kulala pia huchangia mtoto kukosa usingizi wakutosha.

 Watoto wa mwaka mmoja adi mine(1-4)wanaitaji masaa 14 ya usingizi kila siku.wanatakiwa kupata usingizi wa mchana wa kati ya saa moja adi masaa matatu na nusu(1-3.5),usiku wanatakiwa kulala kati ya saa moja na saa tatu(1-3) na asubui  waamke kati ya saa kumi na mbili na saa mbili (12-2) Ni kosa kabisa mtoto kua macho baada ya saa tatu,endapo mtoto wako huwa macho baada ya saa tatu ni kiashirio kwamba anashida au tatizo Fulani.

 Asilimia kubwa sana ya watoto hawapati mboga na matunda yakutosha katika lishe zao.Watoto wenye ukosefu wa  vitamin muhim,madini mwili,na aside mafuta za muhim (essential fatty acids) huwa na akili zilizozubaa na hawafanyi vizuri darasani na wana asili ya ukali,watoto wengine huwa na unene wa ziada ambao pia husababishwa na lishe mbaya,Lakini kubwa kabisa mtoto huyo hawezi kukua katika uwiano ulio sahihi.

 Watoto wanapofikia umri wa kuanza kwenda madarasa ya awali ndio ule wakati ambao mtoto hurefuka na mwili wake huwa na nguvu nyingi,huu ndio wakati ambao wanaanza kujifunza kujitegemea na kutengeneza wasifu binafsi(personalities).Mtoto huanza kubagua chakula,na kuamua anapenda au apendi chakula kipi. Watoto wanaobagua chakula huwa kwenye hatari kubwa ya kukosa virutubisho maalum vinavyoitajika kuwezesha ukuaji wao,kwani virutubisho hivyo huchangia ukuaji bora wa akili,mwili,na hata hisia.

 Ukuaji sahihi wa mifupa na meno kwa watoto umekua ni changamoto kubwa  sana,kwani asilimia kubwa ya watoto hawapati vitamini muhim,madini mwili na asidi mafuta ya kutosha kuwezesha ukuaji wao.images
 Nini maana ya  Lishe Bora(balanced diet)?ni lishe yenye virutubisho vyote kwa kiasi sahihi na uwiano sahihi ili kuwezesha afya bora.Virutubisho vyote sita lazima viwepo: wanga,protini, mafuta ,vitamin, madini mwili na maji.kwa ujumla hii ndio maana ya lishe bora,lakini kitaalam zaidi,wataalam wa afya husema lishe bora hutofautiana kati ya makundi mbalimbali ya binadam kutoka na uhitaji wa miili yao katika kipindi Fulani,wakimaanisha inayoweza kua lishe bora kwa mtoto mchanga haiwezi kua lishe bora kwa mtoto wa miaka kumi na mbili kwani miili yao inauhitaji tofauti,au kilicho lishe bora kwa mama mjamzito hakiwezi kua lishe bora kwa mgonjwa wa Moyo kwani wao pia miili yao inauhitaji wa tofauti.
 Kwa mantiki hiyo basi ili lishe ya mtoto wa mwaka mmoja adi miaka  minne iitwe lishe bora,ni lazima iwe na virutubisho vifuatavyo

  • Wanga:ugali,wali,viazi,mkate
  • Mboga za majani na matunda kwa wingi-lenga kumpa mara tano kwa siku
  • Protini:nyama,samaki,mayai,maharagenjegere(angalao  ale samaki mara mbili kwa wiki)
  • Vyakula vyenye asili ya maziwa:maziwa,yoghurt,cheese (lazima ale kila siku)
  • Mafuta.sio mafuta ya wanyama  bali mafuta yatokanayo na mimea(saturated fats)

 Baada ya kujua lishe bora ya mtoto,tuangalie umuhim na kazi za Virutubisho tulivyoainisha hapo juu.

 Vitamini C 
 Mwili wa binadm hauwezi kujitengenezea vitamin C,hivyo ni lazima ipatikane katika lishe.Vitamini C huwezesha utendaji bora wa akili,huusika katika kuendesha hisia,pia huuwezesha mwili  kunyonya madini joto.kila siku mpe mtoto juisi ya machungwa au apple(isiwe kali)na apate Nyama au samaki.Vitamini C hupatikana kwenye machungwa,mboga za majani zenye rangi ya kijani mkoozo na Apples.

 Vitamini A
 Vitamin A hutengeneza Meno na Ngozi yenye afya nzuri na kufanya mtoto aone vizuri.inapatikana kwenye mayai,nyama,maziwa,cheese,karoti na mboga  za majani zenye rangi ya kijani mkoozo.
 karoti kubwa kama hizi moja huuzwa kati ya 200  na 300 Gengeni.lakini hizi zote apa kwenye picha nilinunua kwa 2000
Vitamin D
 Vitamini D huwezesha mwili kunyonya calcium,bila calcium mifupa haiwezi kukua katika uwiano sahihi wala kuwa na nguvu hivyo mtoto anaweza kupata matege na kua na mifupa dhaifu.Vitamini D nyingi hutoka kwenye mwanga wa jua,si lazima liwe jua kali.Ingawa vitamin D inapatikana pia kwenye Mayai na samaki wenye mafuta  ni vyema kuhakikisha mtoto anatoka nje kucheza kila siku ilia pate mwanga  wa jua ambao utampa vitamin D ya kutosha.
167
Madini  Chuma(iron)
 Madini chuma hutengeneza seli za damu,hasa seli nyekundu ambazo hutumika kusafirisha oxygen katika mwili wa mtoto:bila oxygen yakutosha mtoto hawezi kucheza,kama mtoto wako anachoka wakati wote kuna uwezekano mkubwa wa kua na upungufu wa madini joto.Madini joto hupatikana kwenye nyama,samaki,mbegu za maboga,brown bread,maharage na mboga za majani zenye rangi ya kijani mkoozo.
 061
 Folate (asili yake familia ya vitamin B)
 Huusika sana katika utengenezaji wa seli mpya,hutengeneza DNA,ni ya muhim sana katika ukuaji wa vichanga na watoto wadogo.Folate inapatikana katika mboga za majani zenye rangi ya kijani mkoozo,maharage,karanga ,korosho,hata ivyo spinachi ndio chanzo kikubwa kabisa cha folate.

 Asidi mafuta Muhim(Essential Fatty Acids-EFA’s)
 Mwili hauwezi jitengenezea kirutubisho hiki,ni lazima kipatikane kwenye lishe,kuna familia mbili za EFA’s-Omega 3 na omega 6_ambazo zinaitajika kuwezesha utendaji mzuri wa ubongo,utendaji bora wa kinga za mwili,na kuwezesha  afya akili kwa ujumla.hupatikana kwenye oily fish,na flax oil.Kamamtoto wako anashindwa kutulia darasani,anashindwa kukumbuka vitu,analala kwa shida au hapati usingizi vizuri  basi kuna uwezekano mkubwa wa mtoto huyo kua na upungufu wa Omegas.Nashauri matumizi ya Suppliments(dawa zinazobeba virutubisho) kwani  vyanzo vya omegas ni vichache.

 Calcium
 Madini ya calcium ni kwa ajili ya utengenezaji wa mifupa na meno na pia inaendesha mfumo wa mapigo ya moyo na inasaidia damu kuganda kwaharaka.Bila vitamin D,mwili hauwezi nyonya calcium.calcium inapatikana kwenye mboga za majani zenye rangi ya kijani mkoozo,karanga,maziwa ya Ng’ombe,na vyakula venye asili ya mbegu na katika maji(hard water)
 
Fibre(Nyuzi nyuzi)
 Fibre ni muhim sana katika usagaji wa chakula mwilini.watoto wengi hupata shida kupata aja kubwa (constipation )kwa ajili ya ukosefu wa fibre katika lishezao.ili kuepuka tatizo hili,hakikisha mtoto anapata fibre ya kutosha katika lishe yake.Matunda,mboga za majani,unga usiokobolewa na karanga ni vyanzo vizuri vya Fiber.
Maji
 Mtoto anatakiwa kunywa maji mengi,ili kuzuia constipation na kuepuka kuishiwa maji mwilini,apate kati ya glasi 6 adi 8 kwa siku.

 Kwa ujumla matunda na mboga za majani na matunda ni vyakula muhim sana kwa afya na ukuaji bora wa mtoto.Fanya matunda na mboga za majani sehem kubwa ya mlo wake.badala ya kumpa mtoto biskuti na soda anapotaka kitu cha kula kula,mpe matunda,au juice au smoothie au supu ya mboga.kwa kufanya hivyo unamuweka mtoto wako salama.

 Kwa kumalizia niwaseme wale wakinadada na kinamama wanajiita wa dot com, wanaodhani kumlisha mtoto chipsi na kuku,soseji,tambi,na vyakula vya makopo ndio uzungu.laaa!mnatia aibu.pika chakula kizuri na fresh nyumbani umpe mtoto,zingatia virutubisho ambavyo mtoto anaitaji.Pia niseme na wale kinadada na kinamama ambao wamekariri kua chakula cha mtoto ni uji,mtori,wali wa maziwa na maziwa.mtoto anapofikisha mwaka mmoja anakua katika uwezo wa kuanza kuonjeshwa vyakula vingine.Inashangaza pale unapomkuta mama bado anamsagia mtoto wa miaka mitatu chakula kama ndizi na viazi.Mpe mtoto chakula cha kawaida kabisa kama nyama,maharage,mayai,karanga,ugali,mboga za majani,ili mradi tu kiwe na virutubisho vyote mtoto anavyoitaji.

USIHIFADHI VITUNGUU MAJI NA VIAZI.. SOMA HAPA!!!

Viazi na vitunguu maji vimehifadhiwa pamoja
Pengine umewai kujiuliza kwanini ukiifadhi  viazi ulaya au viazi vitamu  nyumbani havikai muda mrefu vikiwa vizima ,naamini mara nyingi umehifadhi viazi vikaaribika kwa kutoa maji,kutengeneza rangi yakijani, kuanza kuota vikiwa stoo na wakati mwingine  kutengeneza rangi nyeusi na kijani  unapovipika
Viazi na vitunguu maji vimehifadhiwa pamoja

 Viazi na vitunguu maji huendana vizuri sana katika mapishi ,Lakini  ni maadui wakubwa inapofika katika suala zima la uhifadhi wake.Havifai kuhifadhiwa pamoja kwani vitunguu huozesha viazi kwa haraka sana
 Kwanini Vitunguu huozesha viazi
 Vitunguu vina gesi asilia aina ya Ethylene,gesi hii ndio huaribu viazi.Ethylene husababisha viazi vichuje maji yake ya asili, tendo hili hufanya viazi viharibike  au vioze kwa haraka.
kiazi kilichoharibika kwa kuchuja maji baada yakuhifadhiwa pamoja na vitunguu

kiazi kilichoharibika kwa kuchuja maji baada yakuhifadhiwa pamoja na vitunguu.

 Gesi ya Ehylene hupatikana kwa wingi kwenye aina mbalimbali ya matunda na mboga ,baadhi ya matunda hayo  ni pamoja na Ndizi mbivu,apples ,maembe na nyanya.
 Unapohifadhi viazi na vitunguu katika eneo moja au stoo moja hakikisha unavitenganisha na unaviweke mbalimbali.
 Namna sahihi ya kuhifadhi viazi
 Viazi ni chakula chenye asili ya mizizi.Ni moja kati ya vyakula visivyohifadhiwa frijini.Unaweza kuhifadhi viazi vibichi adi wiki nane vikiwa vizima endapo utazingatia kanuni za uhifadhi sahihi.
 Hifadhi viazi mahali pakavu ,penye hewa yakutosha na pasipokua na mwanga.Tandika karatasi juu ya chombo au mahali unapohifadhia viazi.
 Unyevuhuozesha viazi kwa haraka sana kwani hutoa hali nzuri ya bacteria waharibifu  kuzaliana kwa haraka
 Joto:Huozesha viazi,viazi huitaji sehemu yenye hewa yakutosha
 Mwanga:Mwanga huaribu viazi nakufanya vibadilike rangi  yake yaasili na kutengeneza rangi yakijani.Tunza viazi sehem ya giza au isiyokua na mwanga.
 Karatasi:Husaidia kutunza ukavu hivyo kutotengeneza mazingira ya bacteria waharibifu kuzaliana
 Usioshe viazi adi pale unapotaka kuvitumia,kuosha viazi kisha ukavitunza hufanya viazi viharibike haraka.Endapo kiazi kimoja kitaonyesha dalili yakuharibika kitoe haraka kwani kitaharibu na viazi vingine.
 Uhifadhi nwa viazi frijini
 Unaweza kuhifadhi viazi frijini endapo vimekwisha menywa ,uhifadhi huu niwamuda mfupi wa siku mbili au tatu.Unaweza kuhifadhi viazi kwakugandisha na vikakaa muda mrefu.Uhifadhi huu wa friji na kugandisha hubadili ladha ya viazi na viazi huwa rojo unapovipika.Ni vyema kujua kwamba uhifadhi huu pia unambinu zake
 Kuna njia yakienyeji yakuhifadhi vyakula vyenye asili ya mizizi,watu wa makabila ambayo ni wakulima wazuri wa viazi na mihogo hutumia sana njia hii.


Katika makala zijazo Tutaangazia zaidi juu ya gesi ya Ethyleme kwani inanafasi kubwa sana katika uhifadhi wa mboga na matunda .

FAHAMU KILO UNAZOWEZA KUPUNGUZA NDANI YA WIKI.

monique-

Mtu anaweza kupungua kilo ngapi kwa wiki ni swali ambalo watu wengihujiuliza.Hasa pale wanapotaka kuanza arakati za kupunguza uzito.Ni wazi kwamba watu wengi hupenda kufanya Dayati za muda mfupi na wapate matokea makubwa ya haraka.
 
Kiasi cha uzito unaoweza kupunguza kwa wiki hutofautiana kati ya mtu na mtu.Ingawa nia na juhudi binafsi huchukua nafasi kubwa katika hili,Kuna mambo engine  yanayoleta tofauti hizo
 1.Jinsi
 2.Umri
 3.Ukubwa wa mwili
 4.Vyakula unavyokula
 5.Mazoezi unayofanya

 Nguvu joto za chakula (calories)
 Nguvu za chakula yaani kalori(kwa kiswahilli), calories (kwa kiingereza) ni kiasi cha nguvu ambacho hupatikana au hutolewa na chakula kifikapo mwilini.vyakula vyote (vyote viendavyo kinywani) vinaidadi fulani ya calories isipokua maji tu ambayo hayana calories.

 Calories hufanya kazi mwilini kama ambavyo mafuta (petroli au dizeli) hufanya kazi kwenye gari.Ili gari iweze kutembea lazima mafuta yaungue ili kutoa nguvu ambayo hutumika kutembeza gari,na jinsi unavyozidi kutembea ndivyo ambavyo mafuta huzidi kuungua adi yanaisha
 Mwili wa binadam nao hufanya vivyo hivyo,nguvu unazopata kwenye chakula yaani calories,huungua ili kutoa nguvu ambayo inauwezesha mwili wako kufanya mambo mbalimbali kuanzia kupumua,kutembea,kukimbia,na yote ambayo mwiilihufanya.Kadri unavyofanya shuguli nyingi zitumiazo nguvu ndivyo ambavyo calories hupungua mwilini.

 Nusu kilo( 1/2 kg) ni sawa na calories 3500.Ili upunguze nusu kilo katika uzito wako nilazima utoe calories 3500 katika mwili wako.Unaweza kutoa  calories hizo katika mwili wako  kwa kupunguza kiasi cha calories unazokula kwa siku au kwakuongeza mazoezi au kufanya kazi zinazofanya utumie nguvu nyingi ili utumie nguvu za ziada ambazo mwili wako umetunza (unene wako)

 Makala yakitafiti  iliyoandikwa na NBC NEWS mwaka 2009 ilisema kwamba ,kupunguza calories (chakula) ni muhim zaidi kuliko kufanya mazoezi hasa kwa mtu mwenyenia ya kupunguza uzito.Pia ilisema mtu hupunguza uzito kwa haraka zadi endapo atapunguza kiasi cha calories anazokula na kufanya mazoezi ya mwili ili kuunguza calories ambazo mwili wake umetunza.

 Utofauti
 Jins ya mtu huchangia katika kuamua ni kiasi gani cha uzito anaweza kupunguza kwa wiki..Kwa kawaida wanaume wanamisuli mingi kuliko wanawake.Tafiti za Mayo clinic ya marekani zinaonyesha kwamba misuli hutumia calories nyingi hivyo uwepo wake katika mwili hufanya mtu aweze kupunguza uzito kwa haraka.Hii hufanya wanaume waweze kupunguza mwili kwa haraka kuliko wanawake.
 
 
Pia tafiti hizo huonyesha kwamba mtu mwenye uzito mkubwa anauwezo wa kupunguza uzito kwa hararaka kuliko  mtu mwemye uzito mdogo,hasa mwanzoni anapoanza kupungua.

 Mazoezi.
 Kiasi cha calories unazoweza kutoa mwilini unapofanya zoezi au shughuli nyingine hutokana na uzito wa mtu.Mtu mwenye uzito mdogo hutoa calories chache na mwenye uzito mkubwa hutoa calories nyingi kw akiasi kile kile cha mazoezi.
 workouts
 Mfano:mtu mwenye kilo 72.5 atatoa calories 986 kwa kukimbia kwa dakika 60,lakini mwenye kilo 108 atatoa calories 1,472 kwa kukimbia dakika hizo hizo 60
 Kadri unavyotoa  calories nyingi mwilini ndivyo uzito unavyozidi kupungua

 Dayati kali
 Dayati kali hulenga kumfanya mtu apunguze uzito mwingi ndani ya muda mfupi.Tafiti huonyesha kwamba asilimia kubwa ya uzito unaopotea unapofanya dayati kali ni uzito wa maji mwilini.
 011
 Ni  ngumu sana kwa mwili kutoa kilo 1 ya mafuta mwilini kwa wiki.Hata ivyo endapo utaendelea na dayati kali kwa muda mrefu basi unaweza kupunguza mafuta ya mwili na hivyo kupunguza mwili kwa haraka.

 Ukifanya dayati kali sana,ambayo inakufanya uingize calories chache sana mwilini basi kunauwezekano wa kupunguza kilo ndani ya muda mfupi.
 Magonjwa na matibabu
 Historia ya afya yako ni Sababu nyingine inayochangia katika kujua kiasi cha kilo unachoweza kupunguza kwa wiki.Magojwa yasababishwayo na homoni za mwili hufanya iwe ngumu sana kupunguza uzito wa mwili.
 
 Tafiti zinaonyesha kwamba baadhi ya madawa kama madawa ya kisukari na dawa za uzazi wa mpango hufanya  iwe ngumu kupunguza uzito.Baadhi ya madawa pia hufanya mtu ashindwe kabisa kupunguza uzito na madawa mengine hunenepesha mwili.

 Ushauri
 Endapo umekua ukifanya mazoezi na dayati kwa muda mrefu na hupungui uzito,ni vyema ukamuaona Daktari wako na kumuelezea hali hiyo ili aweze kutafuta chanzo cha tatizo hilo na kulitafutia ufumbuzi.
 Kama unafanya juhudi za kupunguza uzito basi punguza kiasi cha calories unazokula kwa siku na pia fanya mazoezi ili kuunguza calories za akiba mwilini.

 Hitimisho.
 Naamini umeelewa nikwanini hakuna kipimo maalum cha kiasi cha uzito ambao mtu anaweza kupunguza kwa wiki,kwani vigezo vyote hivi huchangia katika kupungua.
 Hata ivyo vitu kama msongo wa mawazo na kutokupata usingizi wakutosha,pia huweza kuchangia mtu kupungua uzito au laa kuongeza uzito.