PAMOJA na kua mtoto wa nyota wa zamani wa Manchester United, David Beckham kijana Brooklyn Beckham yuko njiani kuanza maisha kama mchezaji wa kikosi cha kwanza cha wapinzani wakubwa wa baba yake Arsenal ‘The Gunners’.
Kijana huyu mwenye umri wa miaka 15 anafahamika kama shabiki wa Arsenal kwa muda mrefu na alisaini kuichezea timu hiyo mwaka jana akianzia kwenye kikosi cha wachezaji wenye umri chini ya miaka 16.
Hivi karibuni Brooklyn alipakia picha kwenye mtandao wa Instagram akiwa na wachezaji wenzie akiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo vya uwanja wa mazoezi wa Arsenal.
Akiwa amekaa kwenye chumba hicho na wachezaji wenzie Beckham alionekana akiwa mwenye furaha kuwa na wachezaji wenzie na dalili zote zinaonyesha kuwa huenda atafuata nyayo za baba yake ambaye ni moja kati ya wachezaji waliopata mafanikio makubwa kwenye mchezo wa soka.
Brooklyn huko nyuma amewahi kufanya majaribio na timu za Chelsea, Manchester United, Fulham na Queens Park Rangers na alifanya majaribio na Arsenal ambao wamemsainisha mkataba tangu mwezi mwezi novemba mwaka jana.
Cha kushangaza kuhusu familia ya Beckham ni kwamba watto wake wote wa kiume ni mashabiki wa Arsenal na hakuna yoyote aliyechagua kufuata nyayo za baba yao ambaye ni shabiki na gwiji wa Manchester United.
Sio kushabikia tu bali watoto hawa wamekwenda mpaka hatua ya kujiunga na timu hiyo ambapo Cruz mwenye umri wa miaka 9 anachezea kikosi cha vijana wa Arsenal chini ya miaka 10 na Romeo mwenye umri wa miaka 12 anachezea kikosi cha The Gunners kwa watoto chini ya miaka 13 na kaka yao Brooklyn anachezea kikosi cha vijana chini ya miaka 16.
0 comments:
Post a Comment