Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Michael John akitoa tamko kuhusu Siku ya Soko la Afya iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la GIZ , itakayofanyika Oktoba 2 katika ukumbi wa Diammond Jubelee jijini Dar es salaam.
Naibu
Meneja wa Miradi ya Afya wa GIZ Bw. Christian Ptleiderer akizungumza na
waandishi wa habari kutoa wito kwa mashirika mengine yanayotoa huduma
za afya nchini kuendelea kusaidia na kusambaza huduma zao katika maeneo
yenye changamoto ya miundombinu na uhaba wa watumishi wa afya.Kulia ni
Mtaalam na Mawasiliano wa shirika la GIZ nchini Bi. Vida Mwasalla.
********
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
30/9/2014. Dar es salaam.
WIZARA
ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema kuwa itaendelea kushirikiana na
Shirika la Ujerumani la GIZ katika uanzishaji na uendelezaji wa programu
mbalimbali za utoaji wa huduma za afya zinazolenga kupunguza vifo vya
watoto walio chini ya umri wa miaka 5.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Michael John
ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akitoa tamko kuhusu Siku
ya Soko la Afya nchini iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na
Shirika la Ujerumani la GIZ itakayofanyika Oktoba 2, jijini Dar es
salaam.
Amesema
Tanzania na GIZ zimekuwa zikishirikiana katika uboreshaji wa miradi
mbalimbali ya afya kwa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi
kuanzia ngazi ya taifa, mikoa na Halimashauri za wilaya.
Ameeleza
kuwa mikoa ya Lindi, Mbeya, Mtwara na Tanga imeendelea kunufaika na
miradi mbalimbali ya ushirikiano chini ya shirika hilo inayolenga
kuimarisha miundombinu ya kutolea huduma za afya katika maeneo hayo,
uimarishaji wa mifuko ya Afya ya Jamii na ushiriki wa moja kwa moja
kusaidia upatikanaji na uendelezaji wa wataalam wa kutoa huduma za afya
maeneo ya vijijini.
Ameongeza
kuwa GIZ imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
katika kuhakikisha kuwa jamii inamudu huduma bora za afya kupitia Mifuko
ya Hifadhi ya Afya ya Jamii iliyopo katika maeneo yao.
Aidha,
amebainisha kuwa maonyesho ya siku ya Soko la Afya yatakayowahusisha
wadau mbalimbali na mashirika yanayotoa huduma za afya nchini yanalenga
kuwakutanisha wadau hao ili waweze kujadili changamoto za utoaji wa
huduma za afya nchni, kujifunza mafanikio yaliyopatikana katika baadhi
ya maeneo na kuweka mikakati ya kuyafikia maeneo mengi zaidi.
Kwa
upande wake Mtaalam na Mawasiliano wa shirika la GIZ nchini Bi. Vida
Mwasalla ameeleza kuwa maonesho ya mwaka huu yazilenga Wizara, Taasisi ,
Washirika wa Maendeleo, Makampuni, Mashirika binafsi na Wakala
zinazojihusisha na utoaji na uendelezaji wa sekta ya afya nchini.
Amesema
katika maonesho hayo GIZ kwa kushirikiana na Wizara ya Afya itaonyesha
mikakati mbalimbali ya kuwaokoa watoto wadogo wenye matatizo ya afya,
namna walivyofanikiwa kuwapata watumishi wa afya katika maeneo ya Lindi
na Mtwara, maeneo ambayo hapo awali walikuwa hawakai katika vituo vyao.
Ameongeza
kuwa mbali na Siku ya Soko la Afya kuhusisha huduma za utoaji wa elimu,
vipimo, machapisho mbalimbali inalenga kuwaweka pamoja wadau hao ili
waweze kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya kuchangia maendeleo
ya sekta ya afya hapa nchini.
Naye
Naibu Meneja wa Miradi ya Afya wa GIZ Bw. Christian Ptleiderer ametoa
wito kwa mashirika mengine yanayotoa huduma za afya nchini kuendelea
kusaidia na kusambaza huduma zao katika maeneo ambayo bado yanakumbwa na
changamoto mbalimbali za miundombinu na uhaba wa watumishi wa afya.
Amesema
wao kama GIZ kwa kuanzia wameanza na mikoa 4, na wanaendelea kujenga
uwezo wa kuyafikia maeneo mengi zaidi kwa kushirikiana na Serikali ya
Ujerumani na Tanzania.
0 comments:
Post a Comment