WATU wawili walioiba pikipiki tatu na kumjeruhi kwa nondo fundi
pikipiki mmoja baada ya kumuibia moja kati ya pikipiki hizo wameuawa na
wananchi katika maeneo ya Mahiro kata ya Matogoro Manispaa ya Songea
mkoani Ruvuma huku waendesha Bodaboda wakipongeza kuuawa kwa wezi hao
kwani walikuwa wakipoteza maisha yao.
Taarifa za kuuawa wezi hao zimetolewa na kamanda wa polisi wa Mkoa
wa Ruvuma ACP Mihayo Msikhela wakati akizungumza na wanahabari ofisini
kwake na kubainisha kuwa wezi hao wameuawa baada ya kuiba pikipiki tatu
aina Sanlg zenye Namba T.5888, T.363bfl na T.445cjt ambazo zimeokolewa
baada ya wezi hao kuuawa.
Kwa upande wa waendesha bodaboda waliokusanyika kwenye Chumba cha
kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa ruvuma ilikohifadhiwa Miili ya
wezi hao wamepongeza hatua ya kuuawa wezi hao kwani walikuwa wakiwaua
waendesha Bodaboda na kupora Pikipiki zao.
0 comments:
Post a Comment