KUGOMBANA ni jambo ambalo
halikwepeki katika uhusiano wa kimapenzi. Upo
ugomvi ambao ni wa kawaida
na huisha kirahisi lakini upo ugomvi
ambao
huwa mkubwa na kama ukitokea na ukashindwa kujua nini cha kufanya
kuweka mambo sawa, husababisha ufa kwenye penzi lenu.
1. TAFAKARI
CHANZO CHA TATIZO
Kuna usemi kwamba ukitaka kulitatua vizuri tatizo ni lazima kwanza
ujue
chanzo cha tatizo lenyewe. Ukikugundua chanzo cha tati basi na
wewe unakuwa sehemu ya tatizo.
Utashangaa kwamba wapenzi wengi hugombana na mambo kuwa makubwa
kabisa
kwa sababu ya vyanzo vidogo ambavyo walishindwa kuvigundua mapema
na
matokeo yake vikazaa matatizo mengine.
Mfano rahisi, chanzo kinaweza kuwa mpenzi wako amekupigia simu
lakini
ukashindwa kuipokea kwa muda muafaka. Atakapopiga kwa mara
nyingine au
mkikutana, usitegemee atakufurahia kwa sababu atahisi umemdharau
kwa
kutopokea simu yake.Endapo ukifanya makosa ya kushindwa kuliona
kosa lako mapema na kushindwa kuomba radhi au kutoa maelezo yanayoeleweka kwa
nini hukupokea simu, matokeo yake utamjibu vibaya, naye atakujibu vibaya na
mwisho mtaikupigana au kuachana kabisa mkiwa mmeshatoka kabisa kwenye kosa la msingi.
Bila shaka msomaji wangu umeona jinsi chanzo kidogo kinavyoweza
kusababisha tatizo kuwa kubwa. Ndoa nyingi au uhusiano unaofika
mwisho
huwa umesababishwa na mambo madogo ambayo yalishindwa kutafutiwa
suluhu
mapema.
Katika kila ugomvi unaotokea, jambo la kwanza jipe muda wa
kutafakari
chanzo kilichosababisha mkagombana. Wakati mwingine wewe ndiyo
unaweza
kuwa chanzo cha tatizo lakini kama ukiyajua makosa yako mapema na
kukiri
kisha kuomba radhi kwa mwenzio, utakuwa kwenye nafasi nzuri ya
kurudisha
mapenzi kwa haraka.
2. MPE MUDA
HASIRA ZIISHE
Kila binadamu ameumbwa akiwa na hasira na kwa bahati mbaya ni
wachache
wanaoweza kuzidhibiti hasira zao. Ni rahisi mtu kutukana, kupiga
au
kuharibu vitu akiwa na hasira.Baada ya kugombana, kila mmoja
lazima
atakuwa na hasira na njia pekee inayoweza kuepusha matatizo zaidi,
ni
kujipa muda na kumpa muda mwenzako ili hasira zipungue.
Kama mpo sebuleni na umetokea ugomvi, ni busara kwenda chumbani au
nje
mpaka hasira zako zikiisha. Ni makosa kulazimisha suluhu wakati
kila
mmoja akiwa na jazba kwani mtaishia pabaya zaidi.
Ukishaona hasira zako zimetulia na mwenzako naye ametulia, unaweza
kuanzisha mada juu ya kilichosababisha mkagombana. Tumia lugha ya
upole
kwani endapo utakuwa ukifoka au kuzungumza kwa sauti ya juu,
matokeo
yake mtarudia tena kugombana.* *
3. MPE NAFASI YA KUZUNGUMZA
Huwezi kumuelewa mtu kabla hujampa nafasi ya kuzungumza na
kumaliza kile
alichokusudi kukisema. Endapo tatizo limetokea na upo kwenye hatua
za kusaka suluhu, mpe mwenzako nafasi ya kueleza dukuduku lililopo ndani ya
moyo wake.
Usimkatishe wala kumbishia chochote, muache aongee ulichomuudhi
mpaka
dukuduku lake liishe kisha na wewe jieleze kwa upole na sauti
tulivu.* *
4. OMBA MSAMAHA
Hakuna silaha nzuri inayoweza kukusaidia kuushinda ugomvi wowote
na
kutuliza mambo kabla hayajawa mabaya kama kuomba msamaha. Neno
‘samahani’ ni dogo lakini lina maana kubwa kwa yule mtu anayelitoa
na
anayelipokea.
Hata kama unaona dhahiri kwamba kosa siyo lako, omba msamaha
kwanza
kisha baada ya hapo anza kumuelewesha mpenzi wako kwa upole.
Lazima
mwisho na yeye atayaona makosa yake na kukuomba msamaha, mtaweza
kuepuka
kuukuza ugomvi huo na kurudisha hisia za mapenzi.* *
5. USIWEKE
KINYONGO
Endapo umeamua kuomba msamaha kwa mpenzi wako, au yeye amekuomba
msamaha, samehe kwa dhati kutoka ndani ya moyo wako na sahau kile
kilichotokea. Ni kosa kubwa kuweka kinyongo rohoni, yaani
unamwambia
kwamba umemsamehe wakati moyo wako bado una hasira naye. Ukisamehe
kwa
dhati, jifunze na kusahau kwani kusamehe kunaenda sambamba na
kusahau.
Wazungu wanasema forgive and forget. Elewa kwamba mpenzi wako ni
binadamu ambaye hajakamiwala si malaika.Lazima atakuwa akikosea
mara kwa
mara, endapo utakuwa ukilimbikiza vinyongo, unafuga matatizo
makubwa
kwani siku nyingine akikukosea hata jambo dogo, utakumbushia na ya
jana
na juzi na mwisho ugomvi utakuwa mkubwa sana.
0 comments:
Post a Comment