Saturday, November 12, 2016

MAANDAMANO YA KUMPINGA TRUMP YAINGIA USIKU WA TATU

MAANDAMANO yameendelea nchini Marekani dhidi ya Donald Trump katika miji kadhaa ya Marekani kwa usiku wa tatu mfululizo.

Mjini portland katika jimbo la Oregon polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya mamia ya waandamanaji waliyokuwa wakiandamano kutoka kila upande wa barabara za mji huo.

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Vanderbilt mjini Tennessee, wamekuwa wakiimba nyimbo za uwanaharakati wa kutetea mageuzi na kufunga barabara ya Nashville kwa mda.

Maandamano hayo hata hivyo yalikuwa ya amani huku mengine zaidi yakitarajiwa kuendelea katika jimbo la chicago baadaye leo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI