Saturday, November 12, 2016

KIBONGE SEXY - 'MI NA CHID BENZ TUMEBAKI MARAFIKI TU...NAPOSTI *PICHA* ZA NUSU UTUPU KWA AJILI YA BIASHARA'


ALIYEKUWA mpenzi wa staa wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’, Bhoke ‘Kibonge Sexy’ kwa mara ya kwanza amefungukia uhusiano wao kuwa kwa sasa hawako kimapenzi kama zamani.

Akichonga na Global TV Online leo, Bhoke ambaye pia ni mwanamitindo na video queen mnene kuliko wote Bongo alisema, ni muda mrefu tangu awe na Chid kimapenzi na kilichobaki kwa sasa ni urafiki tu.

“Umebaki urafiki wa karibu, wa kumjulia hali na kuzungumza naye tu lakini si wapenzi tena,” alisema Kibonge Sexy.

Kibonge Sexy aliongeza tena, katika maisha yake hamuogopi mtu hivyo anavyoposti picha za nusu utupu anafanya biashara za nguo na hata kaka zake wawili wanajivunia na kutambua kitu gani anakifanya.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI