Wednesday, August 6, 2014

WAFAHAMU NYOKA WENYE SUMU KALI NA MADHARA YAKE

TAIPAN WA ARDHINI
1. Nyoka huyu ni  wa kwanza kuwa na sumu kali duniani, anaeishi ardhini tu. aking'ata kitu chochote hutoa sumu kiasa cha milligram110 iliyo na uwezo wa kuua binadamu 100 au panya 250,000.
NYOKA WA BRAUNI KUTOKA MASHARIKI
2. Nyoka huyu anayepatikana kwa wingi Australia anashikilia nafasi ya pili kwakuwa na sumu kali sana ambayo 1/14,000 ya tone la sumu humuua mtu mzima kwa muda mfupi, anasifika pia kwa kuwa na spidi sana ya kukimbia.
KRAIT WA BLUU
3. Nyoka huyu anayepatikana Kusini mashariki mwa bara la Asia na indonesia anashika nafasi ya tatu kwa kuwa na sumu kali, 50% ya kung'ata kwake husababisha kifo au kuparalyse na ni vigumu kupona hata kwa matumuizi ya dawa ya kumaliza makali sumu ya nyoka(Antivenin). 
Nyoka huyu pia ana sifa ya kuwashambulia na kuwauwa nyoka wenzake hata wa jamii yake.
TAIPAN
4. Nyoka huyu anaeshikilia nafasi ya nne anaptaikana nchini Australia, ana sumu kali iliyo na uwezo wa kuua nguruwe wa guinea 12,000, pia katika ung'ataji wake husababisha kifo ndani ya lisaa limoja.
BLACK MAMBA
5. Nyoka huyu anayepatikana sehemu nyingi ya Africa anashika nafasi ya tano huku akiwa anaogopeka sana kwa ukali wa sumu yake na ushambuliaji wake. 
Ana uwezo wa kushambulia kwa kurusha sumu hadi mara 12 kwa wakati mmmoja ambayo huweza kuuwa binadamu 10 hadi 25 kwa wakati mmoja. 
Ung'ataji wake mmoja hutoa sumu kiasi cha milligram 100 hadi 120. 
Huwa anasifika sana duniani kwa kuwa nyoka wa kwanza mwenye mbio ardhini akiwa na uwezo wa kukimbia kilometa 20 kwa lisaa limoja.
Takwimu hizi zimechapishwa kutoka Listver

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI