Rostam Aziz
MFANYABIASHARA maarufu Rostam Aziz ametoa taarifa kujibu madai yaliyotolewa na aliyekuwa Katibu Mkuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Dk Wilbroad Slaa ambaye katika mkutano wake jana na waandashi wa habari alidai kupata vitisho dhidi ya maisha yake kutoka kwa Bwana Rostam wakati alipotoa orodha ya watuhumiwa wa ufisadi Mwembeyanga
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Bwana Rostam Azizi amekanusha tuhuma hizo ambapo amedai kuwa zinadhihirisha wazi hulka aliyodai kuwa ni ya upotoshaji ambao umekuwa ukifanywa mara nyingi na Dk Slaa, na kuongeza kuwa kama kweli angalikuwa ametoa visitisho hivyo inashangaza kwa nini mlalamikaji hkufikisha taarifa hizo polisi.
Bwana Rostam amemtaka Dk Slaa kujitokeza hadharani na kutoa ushahidi wake dhidi yake kuhusiana na tuhuma hizo na kutaka wananchi wapuuze kile alichokiita uzushi.
Aidha katika taarifa yake, Bwana Rostam amekanusha kauli ya Dk Slaa kwamba anaisadia Chadema ambapo pia amemtaka Dk Slaa kutoa ushahidi kuhusiana na suala hilo huku akikumbusha kwamba mwaka 2010 Dk Slaa alimtuhumu kwamba akiwa yeye, Rais Jakaya Kikwete na Edward Lowassa walikutana katika hoteli ya La Kairo Mwanza kupanga njamaza kumuibia kura zake za urais. madai ambayo hayakuwa na ukweli kwani aliweza kudhibitisha kuwa wakati huo alikuwa nchini Afrika Kusini, huku Rais Kikwete akiwa mkoani Lindi na Bwana Lowassa akiwa Arusha.
Bwana Rostam amehitisisha taarifa yake kwa kumtaka Dk Slaa kama mtu aliyekula kiapo cha upadri kuwa mtumishi wa Mungu kuepuka taarifa alizodai kuwa za upotoshaji zisizo na ukweli.
0 comments:
Post a Comment