Saturday, November 12, 2016

NDUGAI ALIMWAGIA SIFA BUNGE LA 9 LILILOONGOZWA NA MAREHEMU SITTA

Na Emmy Mwaipopo
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai,amekiri kwa kinywa chake kulisifia bunge la tisa lililokuwa likiongozwa na spika mstaafu, marehemu Samuel Sitta huku akisema lilikuwa ni bunge la tofauti.
Akizungumza Ijumaa hii Bungeni mjini Dodoma wakati bunge likitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa spika wa bunge hilo, Ndugai alisema kuwa kiongozi huyo aliweza kusimamia maboresho ya bunge la tisa.
“Samuel Sitta aliweza kusimamia maboresho katika bunge la tisa, tulikuwa na bunge makini lenye demokrasia ya ndani na lenye uwezo wa kuishauri na kuisimamia serikali, kutimiza wajibu wake kwa wananchi kwa misingi ya haki na ufanisi mkubwa,”alisema Ndugai.
Marehemu Sitta alifariki siku kadhaa zilizopita huko nchini Ujerumani alikokuwa ameenda kutibiwa.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI