Thursday, October 16, 2014

MMILIKI WA FACEBOOK ANUNUA UPANDE HUU WA KISIWA CHA HAWAII *PICHAZ*

Kisiwa cha Hawaii
MMILIKI wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg amenunua sehemu kubwa ya kisiwa cha Hawaii iitwayo Kauai ambayo ni hekari 700 kwa dola za Kimarekani milioni 100 ambapo atakuwa anamiliki eneo kubwa ambalo litaendana na hadhi ya bilionea, jarida la Forbes limeripoti.
Hekari hizo 700 zitajumuisha beach resort, mashamba ya miwa na kilimo hai ambapo kwa sheria za Hawaii beach resort hiyo lazima iachwe wazi kwa matumizi ya jamii kwa sababu kisiwa hiko hakina sheria ya umiliki binafsi wa mchanga.
Zuckerberg ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 30 anamiliki dola za Kimarekani billion 33 na anakua ni bilionea wa pili kununua sehemu ya Hawaii.
Mwaka jana mwenyekiti wa Oracle Larry Ellison alinunua upande mzima wa Lanai, Hawaii kwa dola milioni 600 ambapo stori nyingine  zinasema Zuckerbug nae anaweza akawa na nia ya kuanzisha majengo upande huo wa Lanai baada ya kuonekana na mkewe Priscilla Chan kwenye maeneo hayo.
mark1
Mark Zuckerberg na mke wake Priscilla Chan 
Haya yatakua maendeleo mengine ya Zuckerberg kwani mwaka 2010 alikodisha jengo lake ambalo lipo karibu na makao makuu  ya office za Faceboook na mwaka uliofata aliongeza makazi yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 7 huko Palo Alto, California, Marekani ambapo pia baada ya muda mfupi alitumia dola milioni 30 kununua nyumba nne ambazo ziliunganishwa na makazi yake ya Palo Alto.
mark3
Nyumba ya Mark Zuckerberg
Alivyoulizwa kuhusu ripoti zilizotolewa hivi karibuni kuhusu matumizi yake ya pesa msemaji wa Facebook alisema ‘Hatuna chochote cha kusema kuhusu maneno ambayo hayana ukweli ila asante kwa kututafuta’

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI