Monday, November 3, 2014

SHERIA NGOWI AFUNIKA KATIKA MAONYESHO YA MAVAZI YA 'MERCEDES BENZ FASHION WEEK AFRICA 2014' AFRIKA KUSINI

Mbunifu wa kimataifa wa mavazi kutoka Tanzania, Sheria Ngowi akipita jukwaani na models wake huko Afrika ya Kusini.
******
Na Mwandishi wetu
MBUNIFU wa kimataifa wa mavazi kutoka Tanzania, Sheria Ngowi amedhihirisha kuwa yeye ni nguli katika ubunifu wa mavazi baada ya kufunika katika onyesho la mavazi la kimataifa la ‘Mercedes Benz Fashion Week Africa 2014’ lililofanyika ijumaa mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
Ngowi alionyesha mkusanyiko wa mavazi aliyoyaita 'PRIDE' yaani kujivunia, kama moja ya njia ya kumuenzi Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere pamoja na viongozi mashuhuri waliopigania uhuru Afrika.

Afrika kusini ilizizima na kuduwaa kwa muda usiopungua dakika 15 pale ambapo mavazi mbali mbali yaliyobuniwa na Ngowi yalipokuwa yakioneshwa katika ukumbi wa Melrose Arch.
Sheria Ngowi alionyesha mkusanyiko wa mavazi aina ya suti yenye ubunifu na ueledi wa hali ya juu kwa kutumia vitambaa vya kisasa na kale vilivyonakshiwa kwa maua na rangi za kuvutia kama nyekundu, zambarau, machungwa, nyeupe na nyeusi  huku mengine yakiwa bila maua lakini yaliyong'aa kwa kutumia rangi imara kama blu, kahawia na kijivu.

Mercedes Benz Fashion Week Africa 2014 ni onyesho la kimataifa linalofanyika nchini Afrika Kusini mara moja kwa mwaka likikusanya zaidi ya wabunifu wa mavazi 35 kutoka Afrika kwa ajili ya kuonesha ubunifu wa mavazi yao ambapo kwa mwaka huu Sheria Ngowi ni mbunifu pekee aliyechaguliwa katika onyesho hilo kutoka Tanzania.
Models mbali wakipita jukwaani kuonesha mavazi mbalimbali yaliyobuniwa na Mbunifu Sheria Ngowi. 



 Models mbali wakipita jukwaani kuonesha mavazi mbalimbali yaliyobuniwa na Mbunifu Sheria Ngowi.


 Models mbali wakipita jukwaani kuonesha mavazi mbalimbali yaliyobuniwa na Mbunifu Sheria Ngowi.

Onyesho hilo la Mercedes Benz Fashion Week Africa 2014 lilihudhuriwa na watu mbali mbali wakiwemo viongozi wa umma kutoka Afrika kusini, Balozi wa Tanzania Afrika Kusini, Radhia Msuya, wabunifu maarufu wa mavazi kutoka nchi za Afrika kama Taibo Bacar kutoka Mozambique, David Tlale kutoka Afrika Kusini, waandishi wa habari kutoka sehemu mbali mbali za dunia na wadau wa mitindo.
Sheria Ngowi anasifika kwa ubunifu wa mavazi aina ya suti, kanzu, sare za makampuni, mashirika, shule na hafla mbalimbali kama harusi. Mbunifu huyu alifungua rasmi ofisi zake zilizopo Masaki, mtaa wa Buzwagi mkabala na Ubalozi wa Angola mwaka mmoja na nusu uliopita ambapo alianza kazi kwa kuwatengenezea mavazi watu kutoka nchi mbalimbali duniani.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI