Thursday, November 20, 2014

MAJONZI YATAWALA MISS WORLD: MISS HONDURAS MARIA JOSE ALVARADO

MWILI wa mshiriki wa Miss World aliyepotea siku chache kabla ya kusafiri kwa ndege kwenda London kwaajili ya mashindano hayo umepatikana.
 Miss Honduras, Maria Jose Alvarado, 19, na dada yake Sofia Trinidad, 23, wamepatikana leo wakiwa wameuawa. Maria – aliyeshinda taji la Miss Honduras – alipotea akiwa na dada yake baada ya kuhudhuria sherehe ya siku ya kuzaliwa ya rafiki yao Alhamis iliyopita.
Watu wanne akiwemo boyfriend wa Sofia wamekamatwa. 
Honduras, nchini maskini yenye watu milioni nane pekee ni miongoni mwa nchi zenye uhalifu zaidi duniani.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI